Mtunzi ni Jimmy Luoga
EPISODE:5
Ilipoishia wapenzi wasomaji tuliona wosia ulioachwa na mzungu Andrew Reuben ukionyesha mrithi wa mali zake ambaye ni Erick, Je Allen ambaye alitoka nje ya kikao mara baada ya kusikia kuwa Erick ndiye mrithi wa mali za marehemu Andrew alilidhika?. Ungana nami katika simulizi ya aina yake kutoka kwa kijana Daniel aliyebadili jina na kujiita Erick.
SASA ENDELEA...............
Mara baada ya kikao kumalizika nilimkabidhi faili Mwanasheria wa marehemu Baba yetu mlezi na kumuomba kuendelea na wadhifa huo wa kuwa Mwanasheria wangu, yule Mwanasheria alinishukuru sana kwani moja kwa moja alijua kifo cha Andrew ndio ulikuwa mwisho wa kibarua chake.Baada ya kuwatambulisha wale mameneja wa kampuni mbalimbali zilizoachwa na marehemu Andrew kuwa huyo Mwanasheria ataendelea na wadhifa wake kama Mwanasheria wangu mkuu nilihairisha kikao, kisha niliwahaidi kuwa jumatatu yake ningesitisha zoezi la kwenda chuoni kisha ningetembelea kampuni hizo.Baada ya wale mameneja pamoja na yule mwanasheria wangu aliyejulikana kwa jina la Denilson kuondoka pale nyumbani nilienda mpaka pale nilipomuacha Allen ambaye sikumkuta, nilijaribu kumfuata mlinzi na kumuuliza alinijibu kuwa Allen aliondoka na gari, nilipomuuliza kama alimuaga alisema kuwa hakumuaga.Niligeuza kisogo na moja kwa moja niliingia ndani huku nikiwa na lundo la mawazo kichwani, moja kwa moja nilijitupa kwenye kochi kubwa nikajilaza chali huku nikijiuliza maswali kadha wa kadha likiwemo swala la Andrew kunirithisha mali zake zote mimi na sio Allen, nilijikuta nikishindwa kupata jibu kwanini alifanya hivyo, baada ya kuwaza kwa muda mrefu kwa mbali usingizi ulianza kuninyemelea na mwisho nikawa kwenye njozi nzito.Ndoto hiyo ilianza hivi; mimi nilikuwa natoka darasani pale chuoni Muhimbili, ghafla nilimuona Allen akiwa ananiita ndani ya gari kupitia dirisha, nilienda haraka kisha akaniambia alikuja kunichukua anipeleke kwa yule msichana niliyegongana naye pale chuoni kwao siku tatu zilizopita, hivyo kwa kuwa nilipenda sana kumuona huyo msichana nilikubali haraka.Safari ilianza na ghafla nilishangaa Allen akielekea kwenye pori ambalo sikuweza kulitambua lilikuwa wapi, nilipomuuliza kulikoni tulielekea huko alinijibu kuwa huko ndiko alikokuwa anaishi huyo msichana, nilishindwa kupinga kwani tukiwa kwenye mwendo mkali ghafla alisimamisha gari kisha akanitolea bastola na kuniamuru nishuke haraka kisha nisimame katikati ya barabara, kwa hofu na woga nilifanya hivyo, alininyooshea bastola kwenye paji la uso wangu kisha akaniuliza ni mahali gani niliweka nyaraka muhimu za kampuni, mara baada ya kumjibu alifyatua risasi na kunifanya nishtuke toka usingizini nikiwa napiga kelele, nilishtuka kumuona Allen akiwa kasimama pembeni yangu huku mkononi akiwa ameshika kisu kama vile mtu aliyetaka kunidhuru, Macho ya Allen yalibadilika rangi na kuwa mekundu kama mtu aliyevuta bangi "Erick kwanini umedhurumu haki yangu?" swali la Allen akiwa kakunja sura ilinishtua na kukumbuka ndoto niliyoota muda mfupi "hapana Allen hizi mali ni za sisi sote" nilijaribu kumuomba Allen atulie kwani niliamini kuwa hilo lilikuwa swala la maafikiano kati yangu na yeye.Nilimuona Allen akitupa kile kisu chini kisha akarudi nyuma mpaka kwenye sofa lililokuwa nyuma yake akaketi kisha akaanza kulia kama mtoto huku akiniomba msamaha "Erick mdogo wangu naomba nisamehe" nilimuuliza kwanini nimsamehe kisha akajibu kuwa wakati wote nilipokuwa nimelala alipata hisia za kutaka kuniua kwa kuona kuwa mimi nilipendelewa na Baba yetu mlezi.Nilisimama kisha nikamfuata Allen alipokuwa ameketi kisha nikaketi pembeni yake na kumueleza Allen kuwa mali zile zilikuwa ni za kwetu sote, nilimhakikishia kuwa bega kwa bega katika kuendesha miradi katika kampuni hizo.Taratibu nilimuona Allen akipunguza hasira kisha akarudi katika hali yake ya kawaida, baada ya maongezi ya hapa na pale niliweza kuona tabasamu la Allen likirejea katika kinywa chake.Tokea siku hiyo mimi na Allen tulishirikiana katika uendeshaji wa kampuni hizo kupitia usimamizi wa wale mameneja, maisha yetu yalibadilika zaidi na kutufanya tuheshimike vyuoni hata kwa watu mbalimbali nchini, siku moja nikiwa nimeketi nje ya nyumba yetu nikibarizi upepo mwanana wa bahari ghafla honi ya gari ilisikika getini, upesi mlinzi alifungua geti na gari liliingia likiwa linaendeshwa na Allen huku pembeni yake alikuwa mtu ambaye sikuweza kumuona vizuri.Mara baada ya gari kuegeshwa mahali pake wote waliokuwemo ndani ya gari waliteremka, nilipigwa na butwaa nilipowaona wasichana wawili waliovalia suruali zilizowakaa vema na blauzi nzuri huku vichwani mwao wakiwa wameshonea nywele nzuri kama za kishombeshombe almaarufu kwa lugha ya kiingereza weaving, kadiri walivyonikaribia ndivyo nilivyoweza kuitambua sura moja.Mapigo ya moyo wangu yalizidi kunienda mbio nilipoweza kumkumbuka yule msichana mmoja ambaye niligongana naye pale Chuo kikuu Mlimani, nilinyong'onyea kwani niliwaza kuwa kama msichana huyo alikuwa ni mchumba wa Allen ningeumia kisaikolojia.Taratibu walijongea mpaka pale nilipokuwa nimeketi mimi, nilisimama kisha nikawakaribisha viti nao wakaketi huku wakiongozwa na mwenyeji wao Allen.Macho yangu yaligongana na yule msichana ambaye kwa kasi ya ajabu aliyakwepeshea pembeni huku akiachia tabasamu zuri mdomoni pake. "Leo mdogo wangu nimemleta shemeji yako umtambue" nilishuka kwani nilijua tayari nilishapigwa kanzu na Allen baada ya kutoa kauli hiyo, nilimuomba Mungu wangu kati ya wasichana wale wawili asinitambulishe msichana yule ambaye nilitokea kumpenda kuwa ndie shemeji yangu, "huyu anaitwa Liz na huyo pembeni anaitwa Letisia, je unaweza kunitajia kati ya Liz na Let yupi ni shemeji yako?" lilikuwa swali gumu kwangu kwani Liz ndio alikuwa yule msichana ambaye aliutesa moyo wangu, nilijikaza kiutu uzima kisha nikataja kuwa Liz ndiye alikuwa shemeji yangu, wote kwa pamoja waliangua kicheko, kicheko ambacho kilinifanya niweze kugundua kitu "yani Erick pamoja elimu ya Saikojia uliyosomea kugundua mgonjwa huyu anaumwa nini umeshindwa kugundua yupi shemejio?" pale pale nilijikuta nikiangua kicheko cha nguvu mpaka mchozi ukanitoka, sasa ilikuwa zamu yao kunishangaa mimi na kuniuliza kwa nini nilicheka hivyo, nilitulia kidogo kisha nikamjibu Allen kuwa nimefurahi tu namna alivyoniweza.Baada ya utambulisho niliomba niwaagizie vinywaji toka kwa mfanyakazi wetu ambaye alikuwa zamu siku hiyo, mara baada ya vinywaji kuletwa tulianza kunywa huku tukizungumza hili na lile, baada ya dakika kadhaa kupita ndipo Allen na mpenzi wake Letisia walipotuaga kuwa waliingia ndani kwa faragha zaidi, ilikuwa ni nafasi kubwa kwangu kwani kutokana na mvinyo aina ya Whysk niliyokuwa nakunywa niliamini ningeweza kumueleza ukweli yaliyo moyoni mwangu juu yake msichana huyo.Liz pamoja na kutumia kinywaji aina ya Seminor Off lakini alionekana kuwa mpole zaidi huku akirembua macho yake makubwa yenye mvuto, nilimuita jina lake kisha nikamuuliza kama alikuwa tayari nimuulize maswali kadhaa, Liz alinikata jicho kisha akanijibu kuwa alikuwa tayari...................
Je ni maswali gani Erick anataka kumuuliza mrembo Liz? Ungana nami toleo lijalo uweze kujua hatma ya simulizi hii.
Usisahau kutoa maoni

No comments:
Post a Comment