Msanii wa filamu ambaye ni mama wa mtoto mmoja, Aunt Ezekiel katika usiku wa siku ya wapendanao alifunguka na kuzungumzia kitu ambacho kilimuuza katika mahusiano yake na Mose Iyobo.
Akiongea na Bongo5 usiku wa jana katika show ya Valentine’s Day iliyoandaliwa na Irene Uwoya, Aunt amedai kitu ambacho kilikuwa kinamsumbua ni kuambiwa anatoka na mkata viuno.
“Kusema kweli kuna mambo mengi yanatokea kwenye mahusiano lakini mimi hakuna kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza kama watu kuniambia natoka kimapenzi na mkata viono, nilikuwa naumia sana kusema kweli,” alisema Aunt Ezekel “Lakini baadaye nikawa nashangaa wao ambao wanadai natoka na mkata viuno wakaanza kumtumia meseji Mose kwamba wanamtaka,lakini nashukuru sikukata tamaa mpaka sasa nipo na Mose na tunapenda sana,”
Muigizaji huyo amedai amevumilia vingi mpaka sasa ambapo anafurahia maisha yake akiwa Mose Iyobo ambaye ni dansa ya Diamond Platnumz.