Showing posts with label SAIKOLOJIA. Show all posts
Showing posts with label SAIKOLOJIA. Show all posts

Thursday, 26 January 2017

MPENZI HASOMESHWI, HUPASWI KUBEBA MSALABA AMBAO SIO WAKO

Leo imenibidi niongelee kuhusu swala la Mapenzi kutokana na Kuona na kusoma post na comments za watu kuhusiana na Kijana Fredy aliyejikatisha maisha kisa binti aitwaye Rose kuchukuliwa na rafiki yake ambaye ni bosi wake bila shaka..

Hata katika Vitabu vitakatifu vinatuambia Kuwa "Kila mmoja ataubeba Msalaba wake Mwenyewe" na kama ambavyo ilivyo kuwa" “Kila mmoja wetu atatoa hesabu kwa Mungu kwa ajili yake mwenyewe.”—WAROMA 14:12. Iweje wewe leo ukaubebe Msalaba wa Mzazi wa Mwenzio wakati sio Jukumu lako? Una mgharamia wewe ni nani yake? Haya yote yanafanywa endapo tu tayari umeshaingia kwenye agano la Ndoa. Na agano la Ndoa huwa linaanzia pale unapomwambia binti kuwa "Nitakuoa" au Binti anapokwambia "Nitaolewa na Wewe" Hili ndio agano la kwanza ambalo ukinena mbele ya dunia na Mbinguni linakuwa limenenwa na ukiliandika Duniani basi na Mbinguni linakuwa limeandikwa kama ilivyo kuwa Kila lifunguliwalo duniani na Mbinguni limefunguliwa... Sasa wewe hukutamka kuoa au kuolewa na mtu fulani maana yake hakuna agano lolote au haukuniwia kufanya hivyo basi yote yatakayo tokea ni bure kabisa.

Na ndio maana Mwanaume unaposema au kumwambia mwanamke kuwa nitakuoa na bahati mbaya hukumuoa huyo bila kutubu na kuvunja agano hilo kabla ya kumuoa huyo mwingine basi tegemea mambo mengi kukutokea kwenye hiyo ndoa yako mpya kwasababu uliposema nitakuoa maana uliliandika Duniani na kila kinachoandikwa duniani basi na Mbinguni kimeandikwa. Kwa hiyo Kabla ya Kuoa mwingine basi tunapaswa kuvunja maagano hayo kwanza kwasababu Kuongea ni Lango Mojawapo.

Sasa ewe Kijana unayetaka kumsomesha, kumgharamia kwa kila kitu wakati hata kwao hukujitambulisha wala kwenu hakujitambulisha unataka nini? Huo ni msaada tu unakuwa umeutoa na sio lazima akubaliane na wewe... Ungekuwa ushalipa mahali hapo sawa tungeongea mengine ila kwasasa HUPASWI KUBEBA MSALABA AMBAO SIO WAKO... KILA MMOJA ATABEBA MSALABA WAKE MWENYEWE... WAPENZI HAWASOMESHWI NA MPENZI SIO KAZI YAKO HIO WEWE....

KUHUSU KUJIKATISHA MAISHA.

Ni kweli mapenzi yanaumiza tena sana tu na kila mmoja wetu anayesoma hapa alishawahi kuumizwa na mapenzi lakini inategemea baada ya kuumizwa nini kilifuata. Lakini kijana Fredy asionekane mjinga wala Mwendawazimu kwa kitendo cha kukatisha uhai wake laasha bali alikosa watu wa Karibu sana katika kumfanya aone tatizo lililompata sio lake peke yake ni tatizo lililowapata wengi na pia litaendelea kuwapata wengine wengi zaidi.

Sababu iliyopelekea Fredy kujiua sio Mapenzi bali ni hisia kali juu ya Yule aliyempenda kwa imani kuwa Hakuna faida ya kuishi bila ya Rose.Hii kisosholojia tunasema HIGH BELIEVE ndiyo iliyopelekea huyu kijana kujiua.

Kwa vijana wengine Eleweni kuwa tatizo kama hili likitokea kwako tena wewe sio wa kwanza wala wa mwisho na maisha yana maana kubwa sana kuliko Mapenzi.

Muda wote tunapaswa kushukuru kwa Mungu kwa kila Jambo... Tungekuwa tunafata kanuni hii ya Mungu kuwa twapaswa kushukuru kwa Kila Jambo naamini kuwa Kijana Fredy asingejitoa uhai wake mwenyewe maana angeshukuru na Maisha yakaendelea. Na kingine Mungu anatukumbusha katika Zaburi 113:7-9 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.Hapa Fredy ndio ilikua nafasi yake ya kuwa mnyonge mbele za Mungu na yeye angempandisha kutoka jaani ambapo jaani kwake ni kwenye Mapenzi ya dhati.

Lakini muda mwingine tukumbuke kuwa Unyonge mwingine ni wa kishetani kataa kuwa mnyonge kwa jina la Yesu na uwinuke kutoka mavumbini Zaburi 136:23 Aliye tukumbuka katika unyonge wetu kwa maana fadhili zake ni zamilele, Ninaposema mavumbini nikuwekwa chini katika kudharauliwa huku ukikanyagwa na kila mtu iwe kazini au kwenye biashara. Mungu huwainua wanyonge na kuwaaibisha wenye nguvu.

Kwa Leo tuishie Hapa.

Imeandikwa na Josephat Lukaza.

Wednesday, 25 January 2017

Sifa 7 za Wachumba wa Kufanikiwa


Kwanza 
Upo tayari kuingia katika mkataba wa maisha na rafiki yako wa jinsia nyingine? Kabla ya kufaulu kuingia kwenye ndoa, wewe na mwenzio mnapaswa kuwa na sifa za ukomavu zinazoweza kuwahakikishia ndoa imara. Wachumba waliotayari kwa urafiki wa milele huwa na sifa nyingi za kupevuka, lakini kuu kati ya hizo ningependa kushiriki nawe.

1. Kila mmoja anajua anachohitaji na atakachochangia katika ndoa 

Ni dalili ya utu uzima kung’amua kuwa “si vema” ubakie mwenyewe. Unaonesha umekomaa unapohisi uhitaji wa mwingine maishani mwako ili uwe kamili (Mwanzo 2:18). Unapotambua mahitaji yako ya kihisia, kiroho, kijamii, na hata kimwili unakuwa tayari kumkaribia mwenzako ili ukamilike. Ukiwa na utambuzi huo huoni sababu ya kuficha hisia zako. Huna aibu kufungua moyo wako mbele ya macho ya mwenzako. Unamtaka mwenzio ajue umeanza safari ya kumkaribia ambayo kilele chake ni “mwili mmoja”— ngozi kwa ngozi, moyo kwa moyo (Mwa 2:24-25) .

Mkaribie mwenzako na moyo mkunjufu tayari kukamilishwa na mtazamie mwenzako kukutana nawe akiwa na moyo ulio wazi tayari kujazwa na wewe. Kama mikono miwili inapoingiliana inaposhikamana ndivyo wewe na yeye mtakavyokamilishana mnakapokutana. Ulipokuwa mtoto hukujua hilo. Ulidhani wazazi na ndugu zako wapo ili kukukamilisha, kukidhi mahitaji yako tu. Upeo wa kujua mahitaji ya wengine huja na miaka inaposonga. Kama kila mmoja wenu anajua kutoa na kupokea, kupokea na kutoa basi mmeiva katika ushirikiano. Maana ndoa ni ushirikiano,“nakupa unipe”.

2. Kila mmoja humpenda mwenzake kama anavyojipenda binafsi

Wapenzi walioiva kwa ndoa wanajua fika upendo wa ushirikiano baina yao umewezekana kwa kuwa kila mmoja ameshiriki nafsi yake na mwingine. Kama kila mmoja angedharau nafsi yake angewezaje kushiriki zawadi aliyoidharau na rafiki ampendaye? Wapendanao wanajua Bwana hakukosea aliposema “mpende jirani yako kama nafsi yako.” (Walawi 19:18; Mark 12:31).

Kila mmoja wenu asipojipenda mwenyewe; yaani, asipojisikia vizuri, salama, na jasiri kama alivyo, ni vigumu kupendana ninyi kwa ninyi. Usipojikubali ulivyo hutamuamini mwenzako akikuambia amekukubali ulivyo. Tambua unapopanda mashaka nafsini utavuna hofu katika uhusiano. Hofu ya kukataliwa itatia ganzi miguu yako hata ushindwe kumkaribia mwenzako ipasavyo. Kumbuka palipo na hofu hakuna ukaribu wala upendo (1Yoh 4:18). 

3. Wote hufurahi wanapokutana na vile vile wakitengana 

Kama ilivyo kwa uhusiano wowote chini ya jua, ndoa inahitaji ukaribu na umbali; Sulemani anauita,  “Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia” (Mhu 3:5). Uhusiano unaoleta watu karibu pasipo kuwaachia nafasi ya kila mmoja kuwa kama alivyo una hatari zake. Mojawapo ni kumfanya mshirika wa uhusiano huo kuwa sehemu ya nafsi ya mwingine. Matokeo yake ni kutawaliwa na kukinaiwa.

Awali wanandoa walipokuwa hawana hatia kila mmoja alisimama pembeni ya mwingine kwa umbali wa uhuru na ukaribu  wa kutegemeana. Adamu na Hawa walifurahia uhuru wa kila mmoja kama nafsi na utegemezi wa kila mmoja kama washirika wa “mwili mmoja” (Mwa 2:28) Mambo yaliharibika dhambi ilipovamia uhusiano huo na tamaa ya mwanamke ikawa kwa mumewe na
mumewe akamtawala (Mwa 3:16 ). Tangia dhambi iingie duniani tamaa iliyokuwa mnyoro wa kuwaleta wapendanao pamoja imegeuka kuwa mnyororo wa utumwa.--sasa anayependa anapoteza umbali wa kuwa huru kama alivyo na anafanywa zezeta wa kutumikia matakwa ya bwana/bibi ake.
Ikiwa kama ndoa yenu itaeupukana na “udikteta wa upendo” mtajifunza kupeana nafasi ya kuwa nafsi katika uhusiano wenu wa sasa. Kila mmoja awe huru pasipo wivu kufurahia maburudisho ambayo mwenzake hana hamu nayo, au kuwa na marafiki wengine bila kuwa na hofu ya kuvunja uchumba. Kila mmoja awe huru kutumia talanta na vipaji alivyopewa bila ya kuwa na wasiwasi kuwa kwa kufanya hivyo anahatarisha mahusiano. Furahieni upweke wa kuwa mwenyewe na ushirika wa kuwa pamoja. Aganeni kisha rudianeni. Tenganeni kisha ambataneni. Ni kwa kutengana ndipo kila mmoja wenu ataona uthamani wa mwingine; na ni kwa kuwa pamoja ndipo kila huyo ataona haja ya kuwa na  mwenyewe. Wapenzi waliozama kwenye penzi la kweli wanajua hilo na kulikubali kama uhalisia wa maisha chini ya jua.

4. Wachumba wako huru na wazi wao kwa wao kuhusiana na kila mmoja alivyo

Uhusiano wa karibu kama wa wanandoa unawataka wahusika wajianike nafsi kila mmoja kwa mwenzake pasipo kuona haya au hofu. Ndivyo wanandoa wa kwanza walivyokuwa. “Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya” (Mwa 2:28). Hawakuwa na sababu ya kujisikia haya kwa kuwa hawakuwa na kibaya cha kuficha. Unaposhindwa kufikia kuwa huru kwa mwenzako ni kwa sababu unahofu una mabaya yanayopaswa kutojulikana. Hivyo unaishia kujilinda na kujihami ili makosa na kasoro zako zisifahamike. Lakini kwa kuwa utupu unaoulinda upo mbele ya macho yako daima, utaishia kuuona uchi wako kwa mwenzako; makosa yako utamsukumia yeye, kasoro zako utamlaumu yeye. Ni vigumu kujenga mahusiano ya wazi na mtu msiri.

Mruhusu mwenzako ajue ulikotoka, familia yako, uzoefu wako wa utotoni mpaka ujanani. Mfahamishe vidonda na makovu uliyoyapata ili akuelewe. Mueleze uliyojifunza kupitia uchumba au urafiki uliokuwa nao. Mwachie atazame kurasa za historia ya maisha yako, ukurasa mmoja baada ya mwingine. Mruhusu akusome ili akuelewe. Uhuru na uwazi wa aina hiyo utawaleta pamoja; maana, hata hivyo, hakuna ukuta kati yenu.

5. Kila mmoja wao anaweza kujieleza anataka nini kwa uwazi na upole
Hata kama wachumba wamesomana na kufahamiana kwa kitambo bado wanao umuhimu wa kila mmoja kujua namna ya kujieleza. Ni Mungu pekee anayejua yaliyomo ndani ya moyo wa mtu. Pasipo uwezo wa kujieleza mwenzako hatafahamu unataka nini; yeye si Mungu. Wachumba wanaojitambua kuwa kila mmoja ni kiungo kwa mwingine wanachukua kwa uzito ushauri wa Paulo aliposema, “uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake” (Waef 4:25).

Bila kupiga chenga onesha uhitaji wako wa msaada wa mwenzako: huruma yake, usikivu wake, faraja yake, au uwepo wake. Tumia maneno, “nilikuwa naonelea kwamba…’, “honey ningefurahi..”, au “Mpenzi nilisikitika…” Mwalike mwenzako achungulie moyo wako ulivyomhitaji badala ya kumnyoshea kidole moyoni mwake na kumtoa makosa. Hakika, “Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.” (Mith 15:1).

Hivyo, acha kujifanya mshitaki, vua joho la uhakimu, vua uongo, bakia na uso wa rafiki wa kusaidiwa (maana ndiyo uso wako halisi) uone kama mwenzako hataguswa na akusaidie. Jifunze kujieleza pasipo kumshambulia mwenzako. Usiruhusu namna unavyopeleka ujumbe uharibu ujumbe wenyewe. Kumbuka maneno yanaweza yasivunje mfupa lakini yakavunja moyo. Jitahidi kujieleza kwa uwazi uliochanganyikana na upole ili ufaidi msaada unaoutazamia. 

6. Kila mmoja anatafuta kutimiza mahitaji ya mwenzake

Wapenzi walioachana na utoto hawaendekezi “umimi” katika mahusiano yao. Hawajifikirii wao tu. Hawana mashindano tena ya “mwamba ngoma”; isipokuwa, wamejifunza kila mmoja kumhesabu “mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake” na badala ya kila mtu kuangalia mambo yake mwenyewe kila mtu huangalia mambo ya mwenzake (Wafil 2:3,4). Alichosema Paulo ndicho kinachothibitishwa na wanandoa wengi leo: unapojali mahitaji ya mwenzako, mwenzako anavutwa kujali mambo yako.

Utajua upo tayari kwa ndoa kama uko tayari kumtimizia mahitaji mwenzako. Hakika utafaidi ndoa wewe mtoaji kuliko hata mpokeaji. Maana ni ukweli mtupu kwamba, "ni heri kutoa kuliko kupokea" (Matendo 20:35)

7. Kila mmoja ana uwezo wa kujitegemea kiuchumi 
Uwezo wa kutegemeza familia kiuchumi ni muhimu kwa kila mchumba kuwa nao. Una afya, talanta, ajira, na ujuzi wa kukusaidia kujitegemeza kifedha? Kama ndiyo basi upo tayari kwa ndoa.  Uchumi unapokuwa mzuri wa kutosha kuwahakikishia ndani chakula mezani, mavazi ya kuwasitiri, na pango la kuwahifadhi, basi ninyi wapendanao mna hakika ya kuwa na muda kuendeleza pendo lenu.

Mahitaji ya msingi kama chakula, mavazi na malazi yasipotafutiwa ufumbuzi ndoa haibakii salama. Na kama mahitaji ya msingi sio shida ila wachumba wanauchu wa utajiri bado mahusiano yao yatakuwa hatarini. Badala ya kuwa na muda wa mahusiano, kila mmoja atakuwa barabarani “kujitafutia”.

Maisha ya ukristo na hasa ya ndoa ya kikristo yanapaswa yawe ya kuridhika na vilivyo vya muhimu maishani. Paulo alikazia wazo hilo aliposema, “Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.” (1Tim 6:7-9; Mith 30:8).  Ndoa si mali na mali si ndoa.

Wachumba ambao hawajalewa na mvinyo wa mahaba hawatakimbilia ndoa pasipo maandalizi ya kujitegemea kiuchumi. Na wapenzi ambao hawajatekwa na ndoto za utajiri hawatachelewesha mipango ya ndoa kwa kisingizio “hatuko tayari”.

SAIKOLOJIA YA MWANAUME KATIKA MAHUSIANO NA JINSI MWANAMKE ANAVYOWEZA KUITUMIA KULETA AMANI NYUMBANI


Kuna msemo unasema kuwa "mapenzi yanaongoza dunia" kila mtu anayo haki ya kupenda kwa mujibu wa taratibu mbali mbali za dunia hii. 

Mapenzi ni mazuri kama utazingatia mambo muhimu yaliyo halali mbele za Mwenyezi Mungu. Fahamu njia mbadala za wewe msichana zitakazokusaidia kumfahamu mwanaume ambaye ni chaguo lako; 

1. Wanaume wenye heshima ni walinzi na pia watauhifadhi moyo wako, kulinda hisia zako, kulinda heshima yako na watakupatia msaada wa kiroho, kiakili na ustawi wa kimwili. 

2. Wanaume wasiokuwa na heshima, huchukulia tendo la ndoa kama mchezo tu na kiburudisho, na hivyo wanawake kuwa kama tunzo. Kamwe usiruhusu hali hii ikutokee. 

3. Usihukumu vitendo au tabia ya mwanaume mmoja aliyekutenda kuwa hiyo ni tabia ya wanaume WOTE, labda kama unataka wanaume WOTE wawahukumu wanawake WOTE kwa tabia mbaya ya mwanamke mmoja. 


4. Wanaume wengi hupenda mama zao, hivyo usiongee kitu chochote kibaya kitakachomuhusu mama yake. 


 5. Kama kweli mwanaume anampenda msichana basi atafanya juu chini ili mambo yote yawe rahisi kwa msichana, kwasababu anaupendo wa dhati kwake. 
 

6. Jihadharini!!! Mwanaume anaweza kueneza uvumi kama moto na msichana bila kuchelewa anaweza kuusambaza haraka zaidi.7. If a guy likes a girl ,he will always tend to tease her or find a way to talk to her. 


 8. Ili kumuelewa mwanaume, unahitaji kumsikiliza kwanza 
 

9. Wanaume hupenda wasichana wenye uzuri na akili kuliko wasichana wenye uzuri na vinguo vifupi tu. 
 

10. Kama hutumia muda mwingi kumuelezea mwanaume siri zako, basi punguza kwasababu wanaume huwa hawatunzi kumbu kumbu nzuri kama wasichana.

 Muhimu: Njia hizi zinatumika kwa wale wasio katika ndoa, yani kwa wale walioko katika mchakato wa uchumba. Endelea kutembelea site yetu, utajitambua zaidi

Hasara 5 za ushauri wa rafiki kimapenzi


Watu wengi wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.

Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi. Unapokerwa na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.Je, umeshawhi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu ungana nami wiki hii ili nikumegee kidogo hasara za ushauri.

UTAKUPOTOSHANi wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.Uchunguzi unaonyesha kuwa, wapenzi wengi sana hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vema kuwa makini unaposhauriwa.

UTARAHISISHA MAMBOMara nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi kwao kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi. “Vipi kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana, unayeachana ni wewe anayekushauri.“Mkubali tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba, unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.

UTAKUGEUZAUlimwenguni kuna aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa staili zake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo. Uzoefu unaonyesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini je ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?Jibu ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze aamue na apende kama staili yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke ghafla awe kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu lakini upime kama unalingana na matakwa yako.
UTAKUONDOLEA UJASIRI“Kwa maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha, ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”Huu ni ushauri ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake mbaya.Ushauri huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri atakapolipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi. Ikumbukwe kuwa anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi alikuwa mlevi lakini sasa kaacha pombe.
UTAKUNYIMA FURSAKwenye mapenzi kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa mtu wa kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa usimame wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea.

Wednesday, 7 December 2016

ZISOME HIZI KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MWENZA WAKO



Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani.

Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na Mwenzako. 

Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia:

1. Kucheka Pamoja

Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. 

Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika Kila Kitu. 

 Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote.





2. Jifunzeni Kutiana Moyo

Kila Mmoja Awe Msaada Na Tegemeo Kwa Mwenzake. Jifunze Kumtia Moyo Na Kumwezesha Mwenzako. Sikiliza Na Kufuatilia Vile Mwenzako Afanyavyo Au Apendavyo. 

Onyesha Heshima Katika Vitu Hivyo Pia. Kila Upatapo Nafasi Mpongeze Mbele Za Watu Au Hata Unapokua Nae Peke Yenu. Mjenge Mwenzako Mbele Ya  wengine Na Kubali Pongezi Zote Za Mafanikio Yenu Zimwendee Yeye. Mruhusu Mpenzi Wako Ajue Kuwa Una Mkubali Katika Kila Afanyalo. Zaidi Tunavyo Wainua Wapenzi Wetu Ndivyo Wanavyotuthamini Na Kutunyanyua Na Sisi Pia.

3. Jifunzeni Kupenda Kugusana

Nguvu Ya Mguso Wa Ukaribu Kamwe Haiwezi Kulinganishwa Na Chochote. Lazima Mjifunze Kujenga Tabia Ya Kugusana Mara Mpatapo Nafasi Sio Tu Mnapokuwa Mmelala. Kugusana Huku Ni Pamoja Na Kushikana Mkono Mkiongea Au Mkitembea, Kukumbatia Bega, Kugusa Au Kuchezea Nyewele Za Mwenzako Na Njia Nyingine Zozote Za Kuonyesha Ukaribu Kimwili. Wengi Wetu Huweza Kufanya Haya Kidogo Tunapokuwa Peke Yetu Na Kamwe Sio Mbele Ya Watu, Je, Ni Aibu, Nidhamu Mbaya? Dhambi?
Kugusana Ndiyo Mwanzo Wa Kuamsha Hisia Za Kuhitajiana, (Hebu Jiulize Kisirisiri, Lini Uligusana Na Mwenzako Nje Ya Chumba?). Kumgusa Umpendaye Hukuzuia Kutowaza Kumgusa Yeyote Katika Ulimwengu Uliojaa Wengi Walio Wapweke.

Mguso Huu Wa Upendo Haumaanishi Mguso Wa Tendo La Ndoa, Ingawa Pia Ni Vyema Kujifunza Kuijenga Lugha Ya Mguso Wa Tendo La Ndoa Katika Uhusiano Wenu.



 4. Zungumzeni Hisia Zenu

Kati Ya Vikwazo Vikubwa Katika Ustawi Wa Uhusiano Mengi Hususan Ya Wanandoa Ni Kutokuwepo Kwa Majadiliano. Lazima Wapenzi Wajifunze Kuzungumza Kuhusu Hisia Zao. Kama Vile Maisha Yasivyo Na Ukamilifu, Uhusiano Na Hata Ndoa Pia Hazina Ukamilifu. Mpenzi Wako Hayuko Kamili Na Wala Wewe Pia Siyo Mkamilifu. Jifunze Kuzungumza Na Umpendaye Jinsi Unavyojisikia Na Nini Kinachokusumbua. Kuendelea Na Migogoro Isiyosuluhishwa Husababisha Moyo Kuwa Baridi Juu Ya Mwenzako. Jiwekeeni Muda Kila Wiki Wa Kutoka Ili Kuzungumza Mambo Yenu. Mwambie Umpendaye Yapi Yanayojiri Kila Siku Na Zipi Ni Changamoto Zako Mkiweza Kujifunza Kuwekeza Katika Muda Wa Kuwa Pamoja Taratibu Hata Muda Wenu Wa Maongezi Ya Simu Utaongezeka.

5. Samehe Na Kubali Kusamehewa

Kamwe Tusiache Maumivu Na Machungu Yatawale Uhusiano Wetu. Lazima Tujifunze Kuwasamehe Tuwapendao Na Kujisamehe Sisi Pia. Kutofautiana Katika Uhusiano Kupo Sana, Na Lazima Tuwape Tuwapendao Nafasi Ya Kuelezea Vile Vinavyowaudhi Dhidi Yetu. Kila Hisia Za Mmoja Wetu Zina Umuhimu. Huwezi Kujiona Vile Ulivyo, Mruhusu Mwenzako Akwambie Yanayomuumiza Na Msameheane.

6. Linda Mwonekano Wa Mpenzi Wako

Mara Nyingi Hatari Hii Hutokea Tunapokuwa Katika Mizunguko Ya Huku Na Huko. Ukaribu Na Mpenzi Wako Hauendelezwi Tu Bali Unalindwa. Mwonekano Wetu Lazima Uwe Halisi Na Siyo Bandia . Vile Tunavyoviona Katika Tamthiliya Na Filamu Siyo Ukaribu Ulio Halisi. Kama Tunataka Tuonekane Sawa Na Vile Tunavyowaona Wengine Wanavyopendana Basi Tunakosea Na Kujizuia Kuwa Na Mtazamo Bora Katika Uhusiano Wetu. Ukianza Kupata Ukaribu Wa Kweli Baina Yako Na Mwenzako, Utapoteza Hisia Ya Kuhitaji Ukaribu Huo Na Mwingine Yeyote, Na Badala Yake Utaanza Kuulinda Ukaribu Mlionao.

Lengo Liwe Kuvitafuta Vile Vyote Mpenzi Wako Alivyonavyo Ambavyo Ni Kukuza Ukaribu Wenu. Mwenzako Awe Ndiyo Mtu Wa Muhimu Kuliko Wote Katika Maisha Yako.


MWANAMKE ANAHITAJI NINI........



Mwanamke Ana Upendo 98.8999% Kwa Mwanaume…Mwanamke Mpaka Kufikia Hali Ya Kukubaliana Na Wewe Na Akakuheshimu Kwa Kukuvulia Kilakitu Alichonacho Yeye Kwa Kukupa Kile Wewe Unachohitaji Kutoka Kwake Na Amekupa Heshima Wewe Kama Mpenzi Wake Umtumie Unavyokata Na Kutokana Na Mapenzi Anayokupa Anaamua Kukuamini Na Kukupa Siri Zake Zote Wewe Kama Wake Mpenzi Na Mpaka Anawatambulisha Rafiki Zake Kuwa Wewe Ni Shemeji Yao Na Hawezi Ambiwa Chochote Juu Yako Kibaya Akaacha Kukwambia, Then Leo Hii Unamdharau “Aahgghr! Hana Lolote Huyo Kwanza Malaya Tu” …(Mbaya Sana Hii, Jifunze Kuishi Kiutu Uzima Hata Kama Ana tofauti Usiwe Na Hofu Kumweleza Na Ninaimani Atakuelewa)

Usimtese Kijinsia , Usije Thubutu Kumuacha Na Kasoro Zake , Ninamaanisha Kwamba Kama Anatatizo Au Wakati Wa Mambo Yetu Yale Kuna Kitu Unataka Ufanyiwe Na Yeye, Labda Yawezekana Hajui Au Anajua Lakini Ana Walakini Kukifanya, Basi Ni Lazima Umweleze, Muweke Wazi Kumbuka Huyo Ni Mpenzi Wako Ukiwa Kimya Ukasubiri Raha Ukapewe Na Kimada Wa Nje Basi Utajikuta Siku Ya Mwisho Unaleta Ugonjwa Ndani Au Wewe Kukusababishia Kukosa Nguvu Za Kiume Unapokutana Naye Mara Nyingi Kwa Sababu Ni Chanzo Kingine Cha Kusababisha Kukosa Nguvu Unapotembea Na Wanawake Wasiohesabika, Ukikutana Naye Mara Inalala Hii Ni Kutokana Na Uchapaji Wa Too Much Nje, Kwa Sababu Unapokuwa Naye Huwezi Ku Feel Kuwa Naye. Na Badala Yake Utaanza Kuwawaza Wengine Wa Nje Ambao Hawatakusaidia Katika Kujenga Uhusiano Mwema Na Mpenzi Wako. (Kumbuka: Hata Ukibadilisha Kuni, Moto Ni Ule Ule)
Mwanamke Akikupenda Usimdharau Kama Yeye Ni Malaya… Na Mwanamke Mpaka Ukiona Hajatulia Basi Jua Tatizo Lako Wewe, Fanya Juu Chini Ili Kuweza Kumbadilisha Kwa Sababu Kumbadilisha Mwanamke Ni Kitu Kidogo Sana Kwa Sababu Umekaa Naye Muda Mrefu Na Ni Lazima Utajua Tu Umguse Wapi Aweze Kuwa Kama Mwanzo, Kama Umeshanifuatilia Kwa Mada Zangu Ninazokupa Kupitia Hapa . Na Usijeomba Mwanamke Akulilie Machozi Mbele Zako, Ameshindwa Kumlilia Baba/Mama Yake Aliyemzaa Na Amekuja Kukulia Wewe… Wewe Una Nini? Epukana Na Hili Na Utunze Heshima Yake Na Umpe Penzi Lako, Hakuna Mwanamke Mbaya/Malaya/Kicheche Ila Wewe Ndio Utafanya Awe Hivyo… Wengi Wao Wameshawahi Kufanya Haya Na Sasa Wanalia Na Kusaga Meno Kwa Sababu Walijisahau Na Mwishowe Sasa Hawajielewi Kutokana Na Maisha Wayoishi Ya Kutokua Na Chaguzi Zilizo Za Halali…

Mwanamke Anapenda Kupendwa! Mara Nyingi Wanawake Ndiyo Hasa Huwa Na Mapenzi Ya Dhati Zaidi Kuliko Wanaume. Mwanamke Anapoamua Kuwa Na Mpenzi Wake, Humpenda Kwa Moyo Wake Wote, Hivyo Hupenda Kuwa Salama Katika Penzi La Dhati Kwako.

Anapenda Uhuru, Anapenda Kujisikia Wazi Kwako Mahali Popote. Mwanamke Anajisikia Vibaya Sana Anapokuwa Hana Uhuru Hata Wa Kukushika Mkono Mnakuwa Barabarani Pamoja. Anapenda Penzi La Uwazi!

Maana Mwingine Utakuta Akikutana Na Rafiki Yake, Badala Ya Kumtambulisha Vizuri Kama Mpenzi Wake, Anaanza Kupatwa Na Kigugumizi. Utamsikia Akisema: “Ah! Huyu Ni Rafiki Yangu Bwana, Anaitwa Latipha....”Hili Ni Kosa Kubwa Linalofanywa Na Wanaume Wengi Bila Kujua Ni Kosa.

Mwanamke Anakosa Amani Ya Moyo Kutokana Na Unavyomtafsirisha Mbele Ya Rafiki Zako. Anahisi Hayupo Salama. Lazima Atajiuliza Maswali, Kwanini Hataki Kunitambulisha? Kwanini Anashindwa Kusema Mimi Ni Mpenzi Wake? Sifananii? Sina Mvuto Au Nina Tatizo Gani?

Hayo Yanaweza Kuwa Maswali Yatakayomuumiza Sana Kichwa Mpenzi Wako, Ambaye Si Ajabu Akafanya Maamuzi Ambayo Hutayapenda. Kidonda Hiki Hubaki Moyoni Mwa Mwanamke, Huwa Vigumu Sana Kuonyesha Wazi Kwamba Amechukia Kutokana Na Uliyomfanyia, Lakini Atabaki Akiugulia Moyoni Mwake Kwa Uchungu.
Hata Hivyo, Kinachokuja Akilini Mwake Ni Kutafuta Mwanaume Mwingine Ambaye Atakuwa Wazi Kwake Ili Aweze Kufurahia Mapenzi Badala Ya Kuendelea Kuumia Moyoni Mwake. Ni Dhahiri Kwamba Uamuzi Huu Hautaufurahia Hakika.
1. UNAVYOJALI...
Mwanamke Anapenda Awe Wa Pekee Kwako, Umsikilize, Umjali Na Umpe Kipaumbele Katika Kila Unachokifanya . Wanawake Wengi Wanapenda Kudekezwa, Lakini Hawapendi Kuweka Hilo Wazi Kwa Mwanaume Wake. Kwa Kumtazama Tu Utagundua Mpenzi Wako Anahitaji Nini Zaidi Kwako!

Wakati Mwingine Anaweza Kukupa Mitihani Ili Kupima Kiwango Cha Penzi Lako. Anaweza Kukuambia Anaumwa Au Anauguliwa Na Mtu Wake Wa Karibu, Lengo Ni Kuangalia Ni Jinsi Gani Unakuwa Makini Anapokuwa Na Matatizo.

Vile Utakavyochukulia Tatizo Lake Kwa Ukaribu, Uchungu Na Kuona Kama Lako, Ndivyo Utakavyomfanya Aone Thamani La Penzi Lako Kwake, Ikiwa Vinginevyo Basi Humuacha Na Machungu Moyoni, Huku Akijutia Kuwa Na Mpenzi Wa Aina Yako.

Hii Ni Siri Ambayo Si Rahisi Mwanamke Wako Akueleze Moja Kwa Moja. Atatumia Lugha Ya Ishara Kuonesha Jinsi Ambavyo Anahitaji Kuwa Wa Pekee Kwako.

2. JIFUNZE SIRI HIZO.....

Hapa Ndipo Mwanaume Mwerevu Anatakiwa Kuwa Makini, Ni Lazima Ufahamu Siri Zilizopo Moyoni Mwa Mpenzi Wako. Jifunze Kusoma Hisia Za Mpenzi Wako Kwa Nje, Kabla Ya Kufanya Kitu, Fikiria Mara Mbili, Lakini Baada Ya Kufanya, Msome Kupitia Uso Wake.

Analifurahia Au Umemchukiza? Ni Vizuri Kugundua Hilo Ili Uweze Kufunga Hisia Za Kumfanya Aanze Kufikiria Kukusaliti. Hata Mnapokuwa Faragha Ni Vizuri Kuwa Makini Na Kila Unachokifanya! Chunguza Kama Anafurahia Penzi Lako Na Manjonjo Yote Unayomfanyia.

Kumbuka Kwamba Ni Vigumu Sana Mwanamke Kukueleza Moja Kwa Moja Kwamba Hujamfurahisha Au Kuna Kitu Umekikosea, Hii Husababishwa Na Hofu Ya Kuogopa Kukufanya Ujisikie Vibaya.

Kwa Maneno Mengi WEWE Mwanaume Ndiye Mwenye Kazi Ya Kuangalia Mwanamke Wako Anapenda Nini Na Nini Hapendi Ili Uweze Kuwa MWANAUME Wake Bora, Maana Hata Hisia Zake Za Ndani Utakuwa Unazifahamu. Ni Rahisi Sana, Soma Kupitia Macho Yake Kila Unachomfanyia, Utaujua Ukweli. Unajua Hata Ukimwita Kwa Jina Ambalo Hana Msisimko Nalo Lakini Ukiwa Unamtazama Usoni Ni Rahisi Sana Kugundua Kitu Fulani, Kama Hajakipenda Utaona Kwenye Macho Na Akikipenda Pia Utaona.

Unapokuwa Naye Faragha, Tumia Uwezo Wako Wote, Lakini Kumbuka Kwamba Si Kila Utakachokifanya Utamfurahisha. Hii Inamaanisha Kwamba, Baada Ya Kumchunguza Jinsi Anavyosisimka, Utaweza Kugundua Wapi Kuna Msisimko Zaidi Kuliko Sehemu Nyingine.

Hapo Sasa Unaweza Kuibuka MSHINDI Maana Utakuwa Umeziweka Siri Zake Hadharani, Kwa Maneno Mengine Kama Yeye Aliona Siri, Basi Umeweza Kuzigundua Na Angalau Umeanza Kuzifanyia Kazi. Nawapenda Sana Rafiki Zangu, Ndio Maana Nawapeni Mambo Mazuri Na Yenye Sifa Ili Msiweze Kusababisha Kitu Kinaitwa..."UMENITENDA/AMENITENDA" (KUTENDANA NI DHAMBI KUBWA SANA) NIWATAKIE SIKU NJEMA..

WAZO LA LANGU LEO:

WANAWAKE: Napenda Kuwashauri Wanawake Wote Ambao Wapo Katika Mahusiano Ya Kimapenzi Wajaribu Kuwa Wabunifu Katika Mapenzi, Mpe Mpenzi Wako Mapenzi Yote Toka Moyoni Mwako. Usidanganywe Kuwa Mapenzi Ni Mitishamba Hakuna Dawa Ya Mapenzi Kwa Mganga Ila Dawa Unayo Wewe Mwenyewe Mridhishe Mpenzi Wako Kwa Kumpa Vitu Vipya Katika Mapenzi Halafu Uone Je, Penzi Lako Kwa Mwenza Wako Utachangia Na Wenzako?!

WANAUME: Siku Zote Uwapo Katika Mapenzi Fahamu Kuwa Unapaswa Kumridhisha Mpenzi Wako Katika Tendo Mfanye Ajisikie Raha Pindi Muwapo Chumbani Inakubidi Uwe Mwanamke Wa Kileo Ujitahidi Kuwa Mbunifu Katika Mapenzi Kwa Kujituma Pindi Mnapokuwa Chumbani Na Mpenzi Wako, Jaribu Kushughulika Tumia Viungo Vyako Vya Mwili Katika Kuamsha Hisia Za Mwandani Wako Kabla Ya Kuanza Nae Kufanya Mapenzi Ili Kuhakikisha Mpenzi Wako Anapata Raha Na Inakuwa Ni Njia Nzuri Ya Wewe Kumfanya Mpenzi Wako Ahisi Kuwa Wewe Ni Muhimu Kwake

MATESO KATIKA NDOA/MAHUSIANO....KUFUJWA KWENYE NDOA NI NINI?




Ifuatayo ni habari ya mwanamke ambaye aliwahi kuja kwangu kwa ushauri kuhusu ndoa yeke: Mama Kotilda Mkatah aliolewa mwaka 1980 na mume msomi aliyekuwa na wadhifa mkubwa kwenye taasisi moja ya fedha ya serikali.
Ndoa hii ilifungwa kwa sababu, Kotlida hakuwa na njia, lakini anasema, tangu wakiwa kwenye uchumba, alikuwa tayari na wasiwasi kama ndoa yao ingekuwa ni ya amani. Anasema, wakati bado wachumba, huyo bwana aliwahi kumpiga kibao kwenye kituo cha UDA kwa kosa la kuchelewa kufika kituoni kama walivyokuwa wamekubaliana.
Ndoa ilikuwa ni ya mateso makubwa hata kabla haijafungwa, Mwezi mmoja baada ya ndoa, mume alimwachia mkewe kazi kwa kwenda kufanya fujo ofisini kwa bosi wake kwa madai kuwa bosi huyo alikuwa na uhusiano na mkewe. Kotilda alianza kuishi kwa masharti. Hakuna kutoka, hata kwenda kwa jirani bila kuomba ruhusu na kutoa maelezo marefu kwa nini aende huko.
Kusimangwa, kukosolewa, kuitwa mjinga na mbumbumbu, ikaanza kuwa ni sehemu ya maisha ya mama huyu. Hali iliendelea hivi na kotilda akawa anajiambia, kuna siku hali itabadilika. Lakini, kwa bahati mbaya, hali haikubadilika. Wakati anakuja kwangu, alikuwa ameshaanza kuamini kwamba ni kweli alikuwa anastahili kutendewa vile na mumewe.
Huku ndiko tunakoita kufujwa. Mpenzi mmoja anapomuumiza mwingine kwa kauli zake au kimwili, mara kwa mara, tunasema hapo kuna kufujana.
Mpenzi mmoja anapokuwa na mamlaka aliyojipa dhidi ya uhuru na haki ya mwenzake, tunasema hapoimekuwa kufujana. mara nyingi, wanaofuja ni wanaume. Miongoni mwa matatizo ya ndoa ambayo mtu hashauriwi kuendelea kuyavumilia ni kufujwa. Ndoa ya kufujwa kuna maumivu makubwa ya hisia na mwili.
Ni vizuri hata hivyo, nikasema kwamba, neno kufuja ni mimi ambaye nimelibuni keelezea hali hii, ambapo mtu mwingine angeweza kuita mateso katika ndoa, kuonewa katika ndoa au kutumia istilahi yoyote.
Nimeipenda habari hii nikaona si mbaya nanyi wenzangu msome kwani tusinyimane elimu.
Chanzo: kitabu cha Mapenzi kuchipua na kunyauka na marehemu Munga Tehenan.

FANYA HAYA 6 KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU

FANYA HAYA 6 KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU


Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.  Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.

1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:  Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.

2. Upekee wa mambo:  Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.

3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua. 

4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza  kuzitumia kupata suluhu ya tatizo. 

5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu:Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine. 

6. Kuweni peke yenu: 

Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni  kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi.  Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao  kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.

7. Nenda ‘darasani’ :  Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu.