Showing posts with label MAISHA. Show all posts
Showing posts with label MAISHA. Show all posts

Tuesday, 14 February 2017

MKASA : HIVI NDIVYO UZURI WA HOUSEGIRL ULIVYOMPONZA MKE


#inasikitisha sana

Mke alimhisi mmewe kuwa anatembea na housegirl wao, hii ni kutokana na ukweli kuwa housegirl alikuwa mzuri mno kimuonekano, umbo na sura, alifikiri kumfukuza ila mme aligoma kutokana na uchapakazi wa binti yule hivyo hakuona sababu ya msingi ya kumfukuza. 
Hakika housegirl alikua akizidi kumnyima usingizi  mke wa boss, yaani housegirl kadri siku zilivyozidi kwenda alizidi kumeremeta, kila nguo anayovaa inampendeza, kila mkao anaokaa unaonekana ni wa kimitego, hofu ilitanda kwa mke wa boss.
Mke alizidi kuhisi, 
Mbaya zaidi kila siku usiku wakati mmewe akiaga kuwa anaenda kuangalia mpira sebuleni baada ya muda mfupi huwa mke anasikiaga miguno chumba cha housegirl, hivyo akajua itakua tu ni mmewe ananyataga na kumuingilia housegirl wao ndio maana mme shughuli chumbani siku za karibuni imemshinda anachoka haraka mno.
Jumamosi iliyopita aliamua kumtuma housegirl kijijini kwa safari ya siku 2 bila kumjulisha mumewe wala mtu yeyote pale nyumbani. Usiku ule wa Jumamosi mme alimwambia mkewe utaratibu wake wa kawaida kuwa, "Mke wangu mpenz ngoja nkaangalie mpira sebuleni kwenye tv leo Arsenal wanacheza" mke akakubali, mme akaenda sebuleni.
Mke taratibu aliingia chumbani kwa housegirl akajilaza kitandani uchi kama alivyozaliwa, kama kawaida alisikia mlango ukifunguliwa taratibu, mtu akaingia, akapanda kitandani bila kuuliza akavua nguo akaanza kula tunda, baada ya goli la 5, mke akasema, "INATOSHA NIMEKUKAMATA, KUMBE HIVI NDIVYO UNAVYOFANYAGA NA HOUSEGIRL, UKIWA NAMI GOLI 2 TU UNASEMA UMECHOKA KUMBE HUU NDIO MCHEZO WAKO, UNAMALIZIA NGUVU KWA HOUSEGIRL UKIJA CHUMBANI KWETU UNASEMA UMECHOKA WAKATI HAPA TAYARI 5 NA UNATAKA UENDELEE LOOOH!"

Ghafla kwa MSHTUKO mwanaume alijibu, "SAMAHANI mke wa boss sikujua kama ni wewe, ni mimi houseboy wenu mkata majani nisamehe tafadhali"
Mke alishtuka akapiga kelele kwa kupaniki maana anamjua houseboy wao tena ni mwathirika hata kumuajiri pale kwao walimuajiri kwa kumsaidia maana yeye na mme wake wanamjua ni kijana yatima aliyekuwa amezaliwa na UKIMWI wazazi wake walipofariki alitengwa na ndugu ndipo wakamsaidia wakamuajiri kuwa houseboy wao mkata majani, kuzibua vyoo n. k
Kelele alizopiga mama zilimkurupusha mmewe sebuleni na kuwasha taa za nyumba nzima kisha akaelekea chumba cha housegirl kujua nini kimemsibu mkewe, kuingia hakuamini macho yake MKEWE ALIKUA UCHI WA MNYAMA KITANDANI NA HOUSEBOY WAO AKIMBEMBELEZA UCHI KAMA WALIVYOZALIWA.
WIVU MBAYA JAMANI
Yaani Ama kweli umdhaniaye ndie siye, na usilolijua ni usiku wa giza, maskini mama mwenye nyumba kajiponza kisa wivu, alijua mmewe anatembea na housegirl kumbe baba wa watu hana shida na mtu yuko busy na mambo yake. Sasa yamemkuta makubwa mama huyu aibu hii atamuelewa nani mbaya zaidi houseboy ni mwathirika je! Kama ameambukizwa ukimwi itakuaje hakika familia na nyumba nzima imekumbwa na giza nene. NAAMINI WENYE TABIA ZA KUHISI NA KUAMINI TETESI BILA KUTHIBITISHA MTAKUA MMEJIFUNZA KITU.
JE! UNGEMSHAURI MME ACHUKUE MAAMUZI GANI?

Tuesday, 3 January 2017

*HAYA NDIO MAKABILA 125 YA TANZANIA




1. Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
2. Waakiek
3. Waarusha
4. Waassa
5. Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang’ati)
6. Wabembe
7. Wabena
8. Wabende
9. Wabondei
10. Wabungu (au Wawungu)
11. Waburunge
12. Wachagga
13. Wadatoga
14. Wadhaiso
15. Wadigo
16. Wadoe
17. Wafipa
18. Wagogo
19. Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
20. Wagweno
21. Waha
22. Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na Watindiga)
23. Wahangaza
24. Wahaya
25. Wahehe
26. Waikizu
27. Waikoma
28. Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
29. Waisanzu
30. Wajiji
31. Wajita
32. Wakabwa
33. Wakaguru
34. Wakahe
35. Wakami
36. Wakara (pia wanaitwa Waregi)
37. Wakerewe
38. Wakimbu
39. Wakinga
40. Wakisankasa
41. Wakisi
42. Wakonongo
43. Wakuria
44. Wakutu
45. Wakw’adza
46. Wakwavi
47. Wakwaya
48. Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
49. Wakwifa
50. Walambya
51. Waluguru
52. Waluo
53. Wamaasai
54. Wamachinga
55. Wamagoma
56. Wamakonde
57. Wamakua (au Wamakhuwa)
58. Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
59. Wamalila
60. Wamambwe
61. Wamanda
62. Wamatengo
63. Wamatumbi
64. Wamaviha
65. Wambugwe
66. Wambunga
67. Wamosiro
68. Wampoto
69. Wamwanga
70. Wamwera
71. Wandali
72. Wandamba
73. Wandendeule
74. Wandengereko
75. Wandonde
76. Wangasa
77. Wangindo
78. Wangoni
79. Wangulu
80. Wangurimi (au Wangoreme)
81. Wanilamba (au Wanyiramba)
82. Wanindi
83. Wanyakyusa
84. Wanyambo
85. Wanyamwanga
86. Wanyamwezi
87. Wanyanyembe
88. Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
89. Wanyiha
90. Wapangwa
91. Wapare (pia wanaitwa Wasu)
92. Wapimbwe
93. Wapogolo
94. Warangi (au Walangi)
95. Warufiji
96. Warungi
97. Warungu (au Walungu)
98. Warungwa
99. Warwa
100. Wasafwa
101. Wasagara
102. Wasandawe
103. Wasangu (Tanzania)
104. Wasegeju
105. Washambaa
106. Washubi
107. Wasizaki
108. Wasuba
109. Wasukuma
110. Wasumbwa
111. Waswahili
112. Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
113. Watongwe
114. Watumbuka
115. Wavidunda
116. Wavinza
117. Wawanda
118. Wawanji
119. Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
120. Wayao
121. Wazanaki
122. Wazaramo
123. Wazigula
124. Wazinza
125. Wazyoba