Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Wednesday, 15 February 2017
*Kauli 17 za mtu asiye na malengo wala uthubutu*
1)Sina mtaji
2)Sina Connection
3)Nitaanza rasmi kesho
4)Mimi ni wa hivihivi tu
5)Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
6) Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo
7)Kupata ni majaliwa
8)Usilazimishe mambo
9)Kuna watu special siyo mimi.
10)Sina bahati
11) kupata si uhodari nami nitapata tu.
12) Mimi ni fungu la kukosa tu.
13) muda wangu bado nitapata tu
14) mungu hajapanga hata vidole mkononi havilingani.
15) wapo waliopangiwa sisi wasindikizaji
16) Familia yetu hakuna tajiri nianze mimi?
17) hata wanaotafuta mbona wapo vilevile...fulani namjua mbona yupo tu kama mimi au namzidi.
*KAA MBALI NA HUYO MTU. NI HATARI KWA NDOTO ZAKO!!!!*
Tuesday, 31 January 2017
Breaking News: Matokeo ya Kidato cha Nne 2016 Yametoka......Bofya Hapa Kuyatazama
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.
Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali
Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang'ing'ombe pia zikiibuka vinara
Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam

********
WANAFUNZI 10 BORA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016
Sunday, 29 January 2017
Atakayeshindwa kuwasilisha sifa zake za elimu, kujifukuzisha kazi ifikapo machi 1 / 2017.
Mtumishi wa Umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itakapofika tarehe 1 Machi, 2017 atakua kajiondoa kazini mwenyewe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alibainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali jijini Dar es salaam.
“Watendaji Wakuu ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki” Waziri Kairuki alisisitiza.Aliongeza Serikali ilisitisha ajira mpya ili kupisha zoezi la kuondoa Watumishi hewa, zoezi ambalo limefika ukingoni na siku za karibuni ajira zitarudishwa.
Waziri Kairuki aliwataka Watendaji Wakuu kuweka mikakati ya kuepuka watumishi hewa na kusimamia kwa dhati kwasababu jambo hilo limeumiza na kupoteza rasilimalifedha nyingi za Serikali.
Alisema anatambua kuna Wakala zenye upungufu wa Watumishi hivyo zinaingia gharama kubwa za kuajiri wafanyakazi wa mikataba, hata hivyo alielekeza kila Mtendaji Mkuu ajiridhishe kwa kuandaa taarifa ya mahitaji halisi ya Watumishi.
Waziri Kairuki, pamoja na hilo alielekeza Wakala zenye Watumishi wa mikataba zifanye tathmini na kuhakiki kama kweli watumishi hao wanahitajika kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye ajira za mashaka kwa baadhi ya Taasisi.
Waziri Kairuki aliongeza kuwa yapo malalamiko kuhusu suala la maadili na uwajibikaji yanayozigusa Wakala za Serikali. Aliainisha masuala hayo ni pamoja na Watumishi hewa, taarifa chafu za Watumishi, matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za Umma, kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji kazi na wakati mwingine kutotekeleza majukumu ya msingi ya wakala.
Alifafanua kuwa amegundua kupitia taarifa mbalimbali kuwepo kwa changamoto ya mawasiliano hafifu kati ya Wizara mama na Wakala zilizo chini yao ambapo taarifa kutoka katika Wakala hazichambuliwi inavyostahili na hata zinapochambuliwa na wizara mama, hazitoa mrejesho kwenda katika Wakala.
Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro alizitaka Wakala za Serikali kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuimarisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania.
Alisema matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha Wakala za Serikali zinapunguza utegemezi kwa Serikali kwa kujitegemea kimapato kutokana na vyanzo vyake vya ndani hasa kwa Wakala zinazoingiza mapato makubwa kutokana na huduma zinazotoa.
Serikali ilianzisha Wakala kwa lengo la kuzifanya vyombo vya kutekeleza majukumu kwa niaba ya Serikali kwa tija na ufanisi zaidi, pia kupunguza urasimu na hivyo kutoa huduma bora kwa wakati kwa wananchi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Wednesday, 11 January 2017
UGONJWA WA KIFUA KIKUU NA DALILI ZA KIFUA KIKUU
Kifua kikuu ni ugongwa unaosababishwa na vimelea vidogo vidogo aina ya bakteria viitwavyo Microbacteria tuberculosis. Ugonjwa wa kifua kikuu unaenezwa kwa njia ya hewa kutoka katika mtu ambaye anaugua na hajaanza matibabu, mtu huyu akipiga chafya, kukohoa au kutema makohozi ovyo anaweza kuambukiza watu wengine.Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, pia kinaweza kuathiri sehemu yeyote ile nyingine ya mwili ikiwemo mifupa, tumbo na mgongo.
Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kukohoakwa wiki mbili au zaidi mfululizo, homa za mara kwa mara kwa wiki mbili au zaidi, kutokwa na jasho jingi hasa nyakati za usiku, kukohoa makohozi yenye damu, kupungua uzito zaidi ya kilo 3 ndani ya wiki 4 au kukonda pamoja na kukosa hamu ya kula.Kifua kikuu hugundulika kwa kupima makohozi na ikibidi x-ray na matibabu yake ni bure katika hospitali zote za serikali na binafsi.
Unapoona mtu ana dalili mojawapo kati ya hizi au wewe mwenyewe mshauri awahi kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na tiba au awasiliane na mratibu wa kifua kikuu na ukoma aliye karibu nae kwani mtu mmoja huweza kuwaambukiza watu kati ya 10 hadi 15 kwa mwaka kama hajapata matibabu. Wastani wa watu 176 huugua kifua kikuu kila siku nchini Tanzania na wastani wa watu 12 hufariki dunia kila siku .
Ikitokea umegundulika kuwa una kifua kikuu usihofu kwani kinatibika na mamilioni ya watu duniani kote wameugua na kupona. Unachotakiwa kufanya ni kufatisha masharti utakayopewa na daktari kama; kunywa dawa kila siku kwa muda uliopangiwa ili kupona kabisa.
Matibabu yake huchukua kati ya miezi sita hadi minane.Endapo umegundulika kuwa na kifua kikuu kumbuka kufunika mdomo na pua unapo kohoa au kupiga chafya, ili usiambukize watu wengine na pia usiteme mate ovyo.Pumzika kiasi cha kutosha, kula chakula bora na uwafahamishe ndugu na marafiki kwamba unaugua kifua kikuu na uko kwenye matibabu, na ukisha kamilisha matibabu nenda kwa mhudumu wa afya kwa uchunguzi ili kuthibitisha kama umepona.Kumbuka ni muhimu kuendelea kutumia dawa mpaka mwisho hata kama unajisikia vizuri ili usipate kifua kikuu sugu ambacho matibabu yake ni magumu.
Mara kwa mara kifua kikuu kimekuwa kikihusishwa na ugonjwa wa ukimwi kwani asilimia 50 ya watu wenye kifua kikuu wana VVU. Kama umethibitika una kifua kikuu ni muhimu kupata ushauri nasaha na kupima virusi vya UKIMWI, kwani asilimia 10-15 ya watu wanaoishi na VVU wanaugua kifua kikuu, hivyo ni muhimu kuchunguzwa kama una kifua kikuu ili kuboresha na kuokoa maisha yako kwani kifua kikuu kinatibika kabisa hata kama una maambukizi ya VVU.
Ni mimi Archandramu Mbungu
Mwanasoikolojia
Mtoa Ushauri Nasaha
Subscribe to:
Posts (Atom)