*Dkt. John Pombe Magufuli-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.*
#Mimi ni mwalimu, sijabadilika, shida na raha za ualimu nazifahamu.
#Sisi vongozi ndani ya serikali hatuwezi tukawaangusha, walimu ni jeshi kubwa.
#Nashukuru Viongozi wa Chama cha Walimu kwa uamuzi wa kuufanyia Mkutano huu Mkoani Dodoma.
#Nitaendelea kuwa mtumishi wa watanzania wote,sitawabagua kwa Dini wala Vyama
#Sekta ya Elimu ni Nyeti na muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote.
#Natoa pongezi kwa viongozi watangulizi wataifa hili kwa jitihada walizofanya katika kuiendeleza sekta ya elimu.
#Natoa pongezi kwa walimu kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwaelimisha watanzania.
# Tumeongeza Fedha za elimu bure kutoka Tzs 18.77 Bil. Hadi kufikia Tzs Bil. 23.868 kwa mwezi na mpaka sasa tumetumia Tzs Bil. 535.
# Serikali ya Awamu Tano imejenga na kurabati shule za Msingi na Sekondari 365 mpaka sasa.
#Mwaka huu tumegawa vifaa vya maabara katika Shule za Msingi za sekondari 1696.
#Walimu wanapomaliza masomo wafanye kazi kwenye vituo wanavyopangiwa.
#Walimu wanaopewa Posho za Madaraka wazitumie vizuri, na wanaotoa madaraka watoe bila upendeleo kwa walimu wanaojituma kwa ajili ya watanzania.
#Serikali imelipa Tzs Bil. 56.92 kwa ajili ya kulipa madeni ya walimu.
#Haya Madeni ya walimu tutayalipa yote, mara baada ya kazi ya uhakiki wale wote walioomba madai halali watalipwa.
#Viongozi niliowateua akiwemo Makamu wa Rais ni watetezi wakubwa wa walimu.
#Tumeongeza bajeti katika sekta ya afya kutoka Tsz bil. 31 hadi Tzs Bil. 239.
#Mnapokaa katika vikao vyenu kumbukeni kuuliza madai ya fedha zenu ikiwemo kutoka Benki ya Walimu.
#Serikali inapaswa kuhakikisha kile kinachopatikana kinapelekwa katika sekta zote, kile kinacholetwa kwenu na serikali naomba mkipokee.
#Udahili wa wanafunzi umeongenzeka kutoka Mil. 1 hadi Mil. Moja na Laki 9 kutokana na elimu bure na kwa sekondari udahili umeongezeka kwa asilimia 31.
#Serikali imetoa ajira 3462 kwa walimu wa sayansi na niwaahidi walimu, wanafunzi ajira zipo.
#Mamlaka husika angalieni kwa makini suala la mgawanyo wa walimu Mijini na Vijijini, lakini isiwe mwanya wa kuhamisha bila kufuata utaratibu.
#Usihame kama hujalipwa pesa yako, hakuna atakayekufukuza kazi kama hajakulipa pesa ya uhamisho.
#Tumekuwa na hifadhi za Jamii nyingi zisizofuata taratibu za hifadhi za jamii, ndio maana tunataka tuwe nazo mbili, moja ya Serikali nyingine ya sekta binafsi.
#Tunataka tuwe na hifadhi za jamii zinazojali watu wake na zitakazojenga viwanda.
#Tunaziunganisha Hifadhi za sekta za jamii kwa lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
#Natambua umuhimu wa posho ya kufundishia kwa walimu ili kuwapa motisha walimu
#Uchumi wa nchi yetu upo vizuri na ndio maana ipo miradi tunayoitekeleza kwa fedha zetu.
#Serikali inafahamu umuhimu wa kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwaongezea uwezo.
#Katika uchaguzi wenu, msichague watu kwa maslahi yao wala kwa rushwa, viongozi watakaowapeleka mbele na kwa ajili ya maslahi ya walimu.
#Vyombo vya dola vinavyohusika na rushwa vinafanya kazi.
#Viongozi mliopo chambueni madai ya walimu katika mikoa yote na mkiridhika nayo yapelekeni kwa waziri mkuu, haiwezi kumaliza mwezi mmoja nitayalipa yote.
*Mwl. Simoni Keha-Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)*
#Chama cha walimu kimefanya vikao kadhaa na serikali, ambazo hoja zetu zimepokelewa tunaamini zitafanyiwa kazi kwa maslahi wa walimu.
#Tunapongeza Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa uamuzi wa kuwajengea walimu nyumba.
#Tunaishukuru Serikali kwa Umamuzi wa kupeleka Bungeni sheria ya mabadiliko ya Hifadhi ya Jamii
*Mwl. Leah Ulaya Kaimu Rais-Chama cha Walimu-(CWT)*
#Juhudi zako na Serikali zinaonekana wazi, Watanzania na walimu tumeanza kuiona Tanzania Mpya.
#Walimu tunaimani sana na serikali yako, walimu wako ni wazalendo.
#Watumishi wote nchini tuungane kwa pamoja kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli ili aendelee kututumikia.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*