Baraza la kwanza la mawaziri liloundwa na Raisi Nyerere kufuatia kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi, Baraza hili lilikuwa na wizara 26 Kama ifuatavyo :
Makamu wa Rais alikuwa, Ndugu Aboud Jumbe (M. B. L. M) Zanzibar
Waziri mkuu alikuwa Ndugu Edward Moringe sokoine, kutoka Monduli
Na mawaziri walikuwa ni wafuatao na wizara zao :
1,waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa alikuwa Mh, Rashidi M. Kawawa kutoka Liwale
2,waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi alikuwa Ndugu, Amir H. Jamal kutoka morogoro mjini
3,waziri wa Nchi, Ofsi ya Rais ustawishaji wa makao makuu Ndugu, Alhaji Hasnu makame, kateuliwa Zanzibar
4,waziri wa viwanda Ndugu Cleopa D. Msuya kateuliwa
5,waziri wa kilimo Ndugu, John S. Malecela kutoka Dodoma vijijini
6,waziri Asiye na wizara maalumu Ndugu, Alfed C. Tandau kutoka mbinga
7,waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Ndugu Hassan Nassoro Moyo kutoka Zanzibar
8,waziri wa Sheria Ndugu, Julie C. Manning, kateuliwa
9,waziri wa Biashara Ndugu, Alphonce Rulegura kutoka Sengerema
10,waziri wa Elimu ya Taifa Ndugu,Nicholas kuhanga huyu alikuwa mbunge wa Taifa
11,waziri wa Afya Ndugu, Dr. Leader Stirling huyu nae alikuwa mbunge wa Taifa
12,waziri wa maliasili na utalii Ndugu, S. A. Ole saibul kutoka Arusha
13,waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya mijini Ndugu, Tabitha siwale. Kateuliwa
14,waziri wa kazi na ustawi wa jamii Ndugu, Crispin Tungaraza mbunge wa Taifa
15,"waziri wa maji, umeme na madini Ndugu, Anoor kassum, kateuliwa
16,waziri wa Nchi, ofsi ya waziri mkuu Ndugu, H. R. Shekilango kutoka korogwe
17,waziri wa Habari na utangazaji Ndugu, Isaac A. Sepetu, kateuliwa Zanzibar
18,waziri wa fedha na mipango Ndugu, Edwin Mtei, kateuliwa
19,waziri wa mambo ya Nchi za Nje Ndugu, Benjamin Mkapa, kateuliwa
20,waziri wa Maendeleo ya Watumishi Ndugu, Abel K. Mwanga kutoka Musoma mjini
21,waziri wa Nchi Ofsi ya Rais Ndugu, Abdalla S. Natepa mbunge kutoka Zanzibar
22,waziri wa Nchi, Ofsi ya makamu wa Rais Ndugu, Ali mzee Ali mbunge kutoka Zanzibar
23,waziri wa Nchi Ofsi ya waziri mkuu Ndugu, Jackson M. Makweta kutoka Njombe
24,waziri wa utamaduni wa Taifa na vijana Ndugu, Chediel Y. Mgonja kutoka pare
25,waziri wa ujenzi Ndugu, Samwel J. Sitta kutoka Urambo na
26,waziri Asiye na wizara maalumu Ndugu, Daniel M. Machemba kutoka mwanza.