Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

Saturday, 15 April 2017

UGONJWA WA FANGASI UKENI KWA WANAWAKE

Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.
Njia za Maambukizi
Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya;
Vyoo vichafu
Kuchangia nguo za ndani na taulo
Uwezekano wa kupata fangasi ya uke au fangasi ya uke kujirudia rudia unaongezeka pale ambapo mwanamke ana;
Kisukari
Ujauzito
Anatumia antibiotics kwa muda mrefu
UKIMWI
Joto, unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu haumbukizwi kwa njia ya ngono.
Dalili
Fangasi ya ukeni inaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wagonjwa wenye maambukizi;
Kuwashwa sehemu za siri hasa wenye uke na mashavu ya uke.
Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya.
Maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.
Matibabu
Matibabu ya fangasi ya uke hutumia dawa za kuua fangasi (antifungals). Mara nyingi dawa za kuingiza kwenye uke (vaginal pessaries) hutumika kwa muda wa siku 3 mpaka 6. Wakati mwingine dawa za kunywa zinaweza kutumika kutibu fangasi hii.
Onana na daktari kwa ajili ya uchunguzi, dawa na dozi sahihi.Cotrimazole na ketoconazole ni kati ya dawa zinazotumika mara kwa mara.
Pamoja na matibabu kuna hatari ya maambukizi ya fangasi hawa kujirudia, hivyo ni muhimu kupata tiba hospitali na kurudi unapoona inajirudia. Vitu vingine muhimu kuzingatia ni;
Usafi wa nguo za ndani; kuvaa safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).
Vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.
Vaa nguo za ndani zilizotengezwa kwa pamba (hupunguza joto na hivyo hatari ya fangasi kuzaliana)
Usafi wa sehemu za siri na kujikausha viruzi baada ya kuoga.
Usafi wa choo
Kwa mawasiliano na Ushauri tembelea 
Wasap:0766245554
Email:mbunguarchandramu@gmail.com

Friday, 14 April 2017

ugonjwa wa fangasi ukeni kwa wanawake

Ugonjwa wa fangasi ukeni ambao ni common hususani kwa wanawake,
maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua ni tatizo kubwa sana Duniani 75%ya wanawake wote Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili
maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS, maambukizi haya pia hujulikana kama YEAST INFECTIONS /THRUSH
CANDIDA ALBICANS hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia Chakula (PHARYNX), kibofu cha mkojo, uume au katika uke pia.
~bacteria Hawa huishi katika sehemu hizo Bila kuleta madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika, yanapobadilika, MFANO mabadiliko katika Hali ya PH tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0_4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile MATUMIZI YA MADAWA YA ANTIBIOTICS kama AMPICILLINE, CIPROFLAXINE, AMOXYLINE, DOXYCYCLINE, ERTHROMYCINE, NK pia kupungua kwa Kinga kutokana na magonjwa mbalmbali .
~maambukizi ya fangasi ukeni yamegawanyika katika sehemu KUU mbili nazo ni ÷
(1)MAAMBUKIZI YASIYO MAKALI (UNCOMPLICATED THRUSH)
~katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi Mara moja hadi nne kwa mwaka pia Dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS
(2)MAAMBUKIZI MAKALI (COMPLICATED THRUSH)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi Zaidi ya Mara nne au Zaidi kwa mwaka pia Dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakua yametokea kipindi cha UJAUZITO, ugonjwa wa VVU, ugonjwa wa sukari nk



VIHATARISHI VYA MAAMBUKIZI YA FANGASI KATIKA UKE

·         Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambazo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri

·         magonjwa ya saratani ya tezi koo la Chakula (thyroid cancer)

·         wanawake wenye umri wa miaka 20_30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira na vitu wanavyotumia

·         upungufu wa Kinga mwilin kutokana na magonjwa hatar ya saratani, kisukari, ugonjwa wa mononucleosis nk

·         matumizi ya vidonge vya majira

·          msongo wa mawazo

·          kujamiana kwa njia ya kawaida Mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex)

·          matumizi ya glycerin wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia

·         kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy)
~ujauzto (husababisha kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini
~kuwa na utapiamlo (malnutrition
~kuvaa nguo za ndani ziszo kauka vzur
~kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehem za siri

             DALILI ZA UGONJWA WA FANGASI UKENI

·         kuwashwa sehem za siri

·         kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana (superficial dysapareunia)

·         kuhisi kuwaka moto sehemu za siri Mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation

·         kupata vidonda ukeni (soreness

·         kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje wa uke (labia minora

·         kupata maumivu wakati wa kukojoa

·         kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa MWEPESI au MZITO au majimaji
NOTE :Dalili na viashiria hivi huwa mbaya Zaidi mwanamke anapokua mwezini


MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA FANGASI UKENI
Matibabu ya ugonjwa huu wa fangasi hupatikana kwa urahisi Tanzania na tiba hupatikana na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi na majibu yalivyotoka pamoja na hayo matibabu ya ugonjwa huu hospital sio ya uhakika kwasababu dawa za hospital hazitibu chanzo cha tatizo hivyo ndio maana tatzo hili huwa Linajirudia baada ya muda fulani, pamoja na hayo ugonjwa huu unaweza kujiknga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kufanya mambo yatakayotusaidia kutopata ugonjwa huu kwa kuzingatia kanuni ya afya na USAFI


·         Vaa chupi ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri epuka kutumia chupi aina ya synthetic underwear.

·          epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya

·         kula mlo wenye virutubsho muhimu

·         epuka kuoga maji ya moto sana (Hot baths) tumia maji ya uvuguvugu

·         osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji Safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa Safi

·         epuka mavazi yote ya kubana ukeni.

·         tumia ped na pantiliner zenye anions chip zenye uwezo wa kufyonza haraka zenyewe zinaitwa NEPLILY SANITARY PADS ambazo mara nyingi hazipatikani  madukani, hvyo basi tujulishe tuweze kukutumia pale ulipo.

·         kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture Mara kwa Mara yatakusaidia kuepusha maambukizi ya fangasi ukeni

·         epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys, diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni

·          epuka kutumia sabuni za kemikali/dawa kuoshea ukeni nakushaur utumie lady intimate sabuni ya asili isiyo na kemikal na inayoboresha uke wako .

Friday, 7 April 2017

Dalili za mtoto wa jicho


Dalili za mtu mwenye mtoto wa jicho au ukungu kwenye jicho huwa ni kati ya zifuatazo


  • Kuona ukungu au vitu vimefifia
  • Kupata shida kuona wakati wa usiku
  • Kuumizwa macho kwa mwanga au miali ya mwanga ambapo mtu wa kawaida haoni kwamba ni tatizo
  • Kuona nusu duara au duara ya mwanga unaongaa kwenye miali ya mwanga kama vile upinde wa mvua unayokaa
  • Kubadilisha mara kwa mara kwa lensi ya miwani kutokana na hali ya macho kuwa mbaya
  • Kuona rangi zimefifia au rangi ya vitu kuwa njano
  • Kuona kitu kimoja kwamba ni viwili katika jicho moja
Mara ya kwanza ukungu kwenye ukungu kwenye lensi ya jicho unaweza kudhuru sehemu ndogo san ya jicho kiasi kwamba hautapata dalili zozote, muda unapoendelea na ukungu huu kutanda kwenye sehemu kubwa ya lensi ya kicho ndio utakapoanza kupata dalili hizo
Wakati gani uonane na dakitari?
Fanya mipango ya kuonana na dakitari endapo unaona kuna mabadiliko yoyote katika macho yako kama kuona kitu kimoja kuwa marambili kuona ukungu n.k


Friday, 10 February 2017

Fuhamu MADHARA yatokanayo na simu yako na JINSI YA KUYAPUNGUZA.


Simu yako ni HATARI SANA kwenye Afya yako.
Simu tunazozitumia hutoa mionzi (radiations) hatari sana ijulikanayo kama "Electromagnetic waves" wakati wa kupiga/kupokea simu, kuperuzi Internet, nk..

Madhara ya Mionzi hii;

1. Husababisha Saratani ya Ubongo (Brain Cancer) na ngozi (Skin Cancer).
2. Husababisha hitilafu kwenye Ubongo na hii hupelekea kupoteza kumbukumbu, uwezo mdogo wa kupambanua mambo na umakini (Concentration).
3. Husababisha upungufu wa mbegu za kiume na hata utasa (Impotence) kwa wanaume.
4. Huongeza shinikizo la damu.

Jinsi ya kupunguza Athari zitokanazo na Mionzi hii hatari;

1. Weka vifaa maalum vya kupunguza mionzi (Radiation absorbers) kwenye simu yako. Vinapatikana madukani.
2. Usipende kuweka simu mfukoni endapo huitumii. Wakati wa kulala weka mbali angalao SM 30 kutoka ulipo.
3. Simu iwapo mfukoni, upande wa Vitufe na kioo cha simu ndio kielekee mwili wako!
4. Tumia "headsets" au "Kipaza sauti (Loud Speaker). Hii hukusaidia kuwa mbali na mionzi wakati wa kupiga/kupokea simu.
5. Usiitumie simu yako iwapo ina "bar" moja au mbili za "network" (Low Network Signal). Wakati huu simu inafanya kazi kupita kiwango cha kawaida hivyo huongeza wingi wa mionzi.
6. Wakati wa kupiga simu, subiri ipokelewe ndio uisogeze karibu ya mwili (mf. Masikioni).
7. Iwezekanapo, penda kuwasiliana kwa ujumbe wa maneno (text msg) kulipo kupiga simu.

Simu ni muhimu sana katika Maisha yetu ya sasa. Hutuunganisha na ulimwengu uliogubikwa na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Sanjari na hili, tunapaswa kuwa makini katika juhudi za kujaribu kuepuka Madhara yatokanayo na simu kama ilivyoainishwa hapo juu.
      #plusJrPositeveMimd
            NOTE:  Share kwa wengine wajifunze.

Saturday, 21 January 2017

NJIA RAHISI ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUACHA KUVUTA SIGARA


Na Archandramu Mbungu.
MATUMIZI ya tumbaku yamethibitika kisayansi kudhuru karibu viungo vyote vya mwili na kusababisha magonjwa kama vile saratani na kifo. Mbali ya kuwa ina madhara kiafya, tumbaku inasababisha uharibifu wa mazingira, hekta takribani 1200 za misitu zinamalizwa kila mwaka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni za kukaushia tumbaku.
Mataifa mengi yamefanya jitihada nyingi ili kupambana na janga hili la kiafya, mazingira na uchumi. Kufikia Agosti, 2012 nchi 175 zilikubaliana kuchukua hatua kukomesha matumizi ya tumbaku. Hata hivyo, kuna mambo yanayoendeleza mazoea hayo. Kila mwaka, kampuni za kutengeneza tumbaku hutumia fedha nyingi katika matangazo ya kibiashara ili kuvutia wateja wapya, hasa wanawake na vijana katika nchi zinazoendelea.
KWANINI NI VIGUMU KUACHA KUVUTA TUMBAKU?
Vitu vinavyotengenezwa kutokana na tumbaku vinaweza kumfanya mtu awe mraibu (Addicted) kama ilivyo katika kutumia dawa za kulevya.
Pia mtu anapovuta nikotini, inaingia ndani ya ubongo baada ya sekunde saba tu. Nikotini ina asili ya sumu isiyoachika ndani yake.
Mara nyingi kuvuta tumbaku huwa ni sehemu muhimu ya maisha ya mtu kwa kuwa anaivuta anapokula, anapokunywa, anapozungumza, anapotaka kuondoa mfadhaiko na kadhalika.
Vile vile wavutaji hawajajikubali kwamba sigara ni haramu na si nzuri kiujumla.
Ili uweze kuacha kuvuta sigara kwa urahisi zaidi kuna mambo kadhaa ambayo unapaswa kuyafuata.

Andika sababu zinazokufanya uache

Maandishi hayo unapaswa kuwa nayo karibu ili iwe rahisi kwako kuangalia pale unaposhawishika kuvuta.
Mara nyingi unywaji wa pombe huzuia jitihada za kuacha kuvuta tumbaku. Unapaswa kupunguza kiwango cha pombe utakachokunywa pale utakapoacha kuvuta sigara endapo utashindwa kuacha kabisa. Pia unashauriwa kunywa maji mengi na maji ya matunda.
Uchunguzi unaonyesha kwamba nikotini huongeza kiwango cha homoni zinazomfanya mtu afadhaike. Hisia zozote zinazokudanganya kuwa mfadhaiko wako hupungua unapovuta sigara zinaweza kuwa zinasababishwa tu na athari za kuacha kuvuta sigara.
Watu wanapoacha kuvuta tumbaku, uwezo wao wa kunusa na kuonja unaboreka na kwa kawaida wana kuwa na nguvu zaidi na sura yao inapendeza zaidi.


 Panga tarehe mahususi ya kuacha kuvuta
Baadhi ya wataalamu hushauri kuacha taratibu ingawa utafiti unaonyesha kwamba endapo mvutaji atavuta sigara chache tofauti na mwanzo basi kuna uwezekano wa kuvuta mpaka mwisho kila moja ya sigara hizo, hali hii huchangia kiwango cha nikotini kuwa juu karibu na ilivyokuwa mwanzo. Hivyo, ni bora zaidi kuacha mara moja ikifika tarehe iliyopangwa.
 Imarisha azimio lako
Ukitaka kuacha kuvuta sigara unapaswa kuazimia kabisa kuacha. Fikiria jinsi utakavyo faidika pindi utakapoacha kuvuta sigara ikiwa ni pamoja na kuokoa fedha, afya yako inaweza kuwa nzuri zaidi, pia utampendeza Muumba wako
Tafuta msaada
Watafute wale ambao wamefaulu kuacha mazoea hayo kwa kuwa huenda zaidi ya kuelewa hisia zako, wanaweza kukusaidia. Marafiki na washiriki wa familia mara nyingi hutoa ushirikiano kwako ili uweze kutimiza azma yako.
Kama kuna wenzako unaoishi nao wanavuta tumbaku washawishi waache pamoja nawe kwa kuwa nguvu za pamoja ni tofauti na nguvu ya mmoja kupambana na tatizo hili. Usipowashawishi kuacha wanaweza kukushawishi kurudia tabia yako ya uvutaji tumbaku hata kama uliazimia kuacha.
 Teketeza vitu vyote vinavyokufanya uvute
Ni muhimu kutekeza vitu ambavyo vinakushawishi kuvuta sigara kama vile kiberiti cha kuwashia tumbaku na vinginevyo.
Jiandae kukabiliana na madhara
Uchunguzi unaonyesha kwamba karibu asilimia 90 ya wale wanaojikwaa hurudia kuvuta. Unapoacha kuvuta unaweza kupatwa na dalili za ajabu mfano hamu ya kutumia nikotini, kichefuchefu, kujisikia mgonjwa, kichwa kuuma, kushuka moyo, kutokuwa na subra na kujisikia vibaya tu.
Dalili hizi hutokea kutokana na mwili kukosa nikotini iliyokuwa ya kawaida mwilini. Dalili hizi hupamba moto saa 12 hadi 24 baada ya kuacha kuvuta tumbaku na taratibu huacha kati ya wiki ya mbili hadi sita.
Mambo yanayoweza kukusaidia ni pamoja na kulala kwa muda mrefu zaidi, kunywa maji mengi au maji ya matunda, kula chakula chenye lishe, kufanya mazoezi ya kadiri na kuvuta pumzi kabisa na uwazie hewa safi ikijaa ndani ya mapafu yako.
Tegemea kupata kikohozi
Ni kawaida kupatwa na kikohozi pale unapoacha kuvuta tumbaku kwa sababu njia za hewa zinaanza kurudi katika uhai wake. Watu wengi hudai kikohozi hufanya hali kuwa mbaya na kuwashawishi kurudia kuvuta tumbaku. Jitahidi kujizuia kwa kuwa kikohozi hiki hupotea chenyewe kadri muda unavyopita.
Zitambue hali zote zinazokufanya uvute
 Zikumbuke siku zote unazofanikiwa kutovuta
Weka alama kwenye kalenda kwa siku zote unazofanikiwa kuacha kuvuta na ziangalie pale unaposhawishika kuvuta, huku ukijiambia sipaswi kuanza tena upya.
Kuwa mwenye mawazo chanya
Unaweza kuwaambia wengine huvuti, utakuwa na harufu nzuri. Baada ya wiki chache utajisikia vizuri zaidi, utapata ladha nzuri ya vyakula na hutokohoa. Pia utakuwa na fedha zaidi kwa kuwa hukutumia kununua tumbaku.
Vyakula vinavyotakiwa kwa wanaojaribu kuacha
Watu wengine huwa na hofu ya kunenepa wakiacha kuvuta sigara kwa kuwa hamu na ladha ya vyakula huwa bora zaidi pindi wanapoacha kuvuta tumbaku. Yapaswa utegemee kuongezeka kwa ladha na hamu ya vyakula ila jitahidi kutokula vyakula vya wanga na mafuta kwa wingi badala yake ule vyakula vingine na matunda.
 Usikate tama pale unaposhindwa
Chunguza ni kwanini ulishindwa wakati uliopita na jirekebishe. Kwa wastani watu waliofanikiwa kuacha kuvuta wamewahi kujaribu kuacha mara tatu hadi nne wakati uliopita.
Tembelea kliniki za kuzuia uvutaji
Madaktari wanaweza kukupa msaada unaouhitaji endapo unafikiri ni vigumu kuacha kuvuta tumbaku.
 Dawa mbalimbali zinaweza kukusaidia
Utafiti mmoja ulibaini kuwa asilimia 88 ya watu waliofaulu kuacha kuvuta sigara wanasema walifanya hivyo bila kutumia dawa zozote. Dawa hizo huhusisha dawa mbadala ya nikotini na huwa katika mifumo tofauti kama vidonge au bazoka. Pia kuna sigara za kieletroniki (e-cigarette) ambazo zimetengenezwa na hukufanya ujisikie kama unavuta sigara ya kawaida.
 Chagua marafiki
Epuka kuwa na watu wanaovuta tumbaku wanaoweza kukupa sigara. Pia waepuke watu wanaojaribu kuvuruga jitihada zako za kuacha kuvuta tumbaku, labda kwa kukudhihaki.
Dhibiti hisia zako
Katika uchunguzi mmoja karibu asilimia 66 ya wale walio anza tena kuvuta sigara walifanya hivyo baada tu ya kufadhaika au kupandwa na hasira. Ukipatwa na hisia fulani inayokuchochea kuvuta sigara, jikengeushe fikra labda kwa kunywa maji, kutafuna bazoka au kutembea. Jaribu kufikiria mambo yanayofaa.
 Epuka kusema ninavuta mara moja tu
Ukweli ni kwamba kuvuta mara moja tu kunaweza kutosheleza takribani asilimia 50 ya vipokezi vya nikotini kwenye ubongo kwa saa tatu. Matokeo yatakuwa kwamba utaanza tena kuvuta sigara.
Ukweli kuhusu kuvuta sigara husaidia kutuliza mfadhaiko
Ni kweli kwamba athari za kuacha kuvuta sigara zina nguvu, lakini zitapungua baada ya majuma machache tu.
Ikiwa unatibiwa tatizo lako la akili, kama vile mshuko wa moyo au schizophrenia, mwombe daktari akusaidie uache kuvuta sigara. Bila shaka atajitahidi kukusaidia labda hata atabadili matibabu yako ili yasiongeze ugonjwa wako au kuathiri dawa unazotumia.
FAIDA
Utafurahia maisha zaidi.
Utaokoa fedha, afya yako inaweza kuwa nzuri zaidi, utajiamini zaidi.
Familia yako na marafiki watafaidika. Utampendeza muumba wako.

Njia ya kupanga uzazi kwa kutumia Kalenda/ Kuzuia Mimba Kwa Njia ya Kalenda


Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. 
Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  

Nani anaweza kutumia njia ya kalenda

Moja, Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo.

Pili, Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki.

Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana. 

Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua lini mayai yake yalipevuka.  Njia hii inamsaidia zaidi mwanamke aliye na mzunguko wa hedhi wa siku 28, na hutegemea kufahamu kuwa yai la mwanamke hupevuka siku 14 kabla hajaingina kwenye hedhi. 

Kwa mfano; 
1. Kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni (na una mzunguko wa hedhi wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 29 Juni.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 14 kabla kwenye tarehe 15 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi karibu na tarehe hii, kuanzia tarehe 14 Juni hadi 16 Juni.  Kwa hiyo kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Lakini lazima ukumbuke kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke kwa siku 7, kwa hiyo ili kuwa na uhakika Zaidi ya kuepukana na kupata mimba, una takiwa kutokufanya mapenzi kuanzia tarehe 8 hadi 16 Juni. 

2. Katika mfano mwingine, kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 13 Juni (na una mzunguko wa hedhi wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 11 Julai.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 14 kabla kwenye tarehe 28 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 27 Juni na 29 Juni.  Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 21 hadi 29 Juni. 

3. Katika mfano mwingine, kama baada ya kuandaa kalenda kuonesha mzunguko wako wa hedhi wa miezi 3 hadi 6 iliyopita, unagundua kuwa mzunguko wako ni wa siku 33 badala ya siku 28, basi kifuatacho ni kweli:  kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 4 Julai.  Kwa hiyo yai lako litapevuka kwenye tarehe 20 Juni (Siku 14 kabla ya  tarehe 4 Julai).  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 19 na 21 Juni. Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 13 hadi 21 Juni. 

4. Katika mfano mwingine, kama baada ya kuandaa kalenda kuonesha mzunguko wako wa hedhi wa miezi 3 hadi 6 iliyopita, unagundua kuwa mzunguko wako ni wa siku 26 badala ya siku 28, basi kifuatacho ni kweli:  kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 27 Juni.  Kwa hiyo yai lako kitapevuka kwenye tarehe 13 Juni (Siku 14 kabla ya  tarehe 27 Juni).  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi kati ya tarehe 12 na 14 Juni.  Ili kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Kwa usalama zaidi, usifanye mapenzi kuanzia 6 hadi 14 Juni.

Faida ya kutumia njia hiyo
MOJA, Haina madhara yeyote ya kimwili.
 
Matatizo yanayoweza kujitokeza
MOJA, Njia ya kalenda si kinga dhidi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.
PILI, Njia hii ni ngumu na inahitaji wanawake kuwa wastadi katika hisabati, na kuwa waangalifu sana kuandika au kukumbuka tarehe ya kuanza kipindi chao cha hedhi cha mwisho.

TATU, Huchukua muda mrefu (miezi 3 hadi 6) kufahamu urefu wa mzunguko cha hedhi.

TATU, Mzunguko wa hedhi huweza kubadilika wakati wowote kufuatana na mabadiliko katika mwili.  Hii huweza kusababisha tarehe ya yai kupevuka kuwahi au kuchelewa, kwa hiyo mwanamke huweza kujiweka katika hatari ya kupata mimba bila kufahamu.
NNE, Ili njia hii iwe na uhakika, mwanamke hawezi kufanya mapenzi katika siku zake 9 kila mwezi ambapo kuna uwezekano wa yeye kupata mimba.  Kwa hiyo njia hii inahitaji uwezo mkubwa wa kujidhibiti na hufanya kazi vizuri iwapo mwanaume namwanamke wamekubaliana kufanya hivyo kwa pamoja, na mwanaume anamsaidia mwanamke kuhesabu au kuandika urefu wa mzunguko wake wa hedhi.

 TANO, Kwa sababu urefu wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke huweza kubadilika ghafla bila kutegemea, hata kama inatumika inavyotakiwa, njia hii si nzuri kama njia nyingine zilizotajwa kuzuia mimba na kupanga uzazi.

Thursday, 19 January 2017

Magonjwa hatari yatokanayo na kujamiiana


Na Archandramu Mbungu.
Nitakuwa nayachambua magonjwa mbalimbali hatari yatokanayo na kujamiiana ambayo kitaalam huitwa Sexually Transmitted Diseases (STD) ili tuweze kujiepusha nayo na wale ambao wanasumbuliwa na magonjwa hayo waweze kuyatibu na kujiepusha kuwaambukiza wengine.
Ifahamike kuwa magonjwa yote ya zinaa huathiri wanawake na wanaume lakini baadhi ya magonjwa hayo huwa na madhara zaidi kwa wanawake, hii ni kwa sababu pale mjamzito anapokuwa na ugonjwa wa zinaa, baadhi ya magonjwa hayo huweza pia kumuathiri mtoto atakayezaliwa.
Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukiza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono.
Vitendo hivyo vya ngono ni kujamiiana, vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral-genital sex), kujamiiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe kwa mwanaume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators).
Magonjwa ya zinaa huathiri zaidi watu walio na umri wa kati ya miaka 15 hadi 30 lakini pia yanashuhudiwa kwa wingi kwa watu wengine walio na umri wa chini au zaidi ya huu niliotaja.
Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya 20 yanayotambulika duniani, yakiwemo haya:- Kisonono au gono (Gonorrhoea), Chlamydia, Kaswende (Syphillis), ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa na Virusi vya Human Papilloma (HPV), Ukimwi yaani Upungufu wa Kinga Mwilini au HIV/AIDS na kadhalika.
Upo pia ugonjwa wa zinaa unasababishwa na virusi aina ya Herpes au Herpes Virus, Trichomoniasis, ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa na bakteria yaani Bakteria Vaginosis, chawa kwenye nywele sehemu za siri na Chancroid.
Tunapaswa kufahamu kuwa magonjwa mengi ya zinaa au STD’s yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba kama vile Ukimwi, HPV nk.
Sababu zinazofanya watu kupatwa na magonjwa ya zinaa hufanana, kwa hivyo hapa tutaashiria kwa jumla visababishi vya magonjwa ya zinaa.
Kuanza vitendo vya ngono mapema au wakati wa umri mdogo au kuwa na wapenzi au washiriki wengi wa ngono, tukimaanisha kufanya ngono na watu tofauti ni moja ya sababu ya watu kuambukizwa maradhi haya.
Kufanya ngono zisizo salama au ngono zembe pia huchangia kusambaa kwa magonjwa haya.Maambukizi kupitia michubuko au sehemu zilizokatika kwenye ngozi kwa kugusana na majimaji ya aina yoyote kama damu, mate na kadhalika yanayotoka kwa mtu mwenye ugonjwa wa zinaa ni sababu ya kuenea magonjwa haya.
Ni mimi Mwanasaikologia wenu Na Mtoa Ushauri Nasaha kwa rika lote na matatizo ya kiafya, kifamilia, kazi, na mahusiano.
Kwa mawasiliano piga simu hizi 
+255766245554
+255658245554

Thursday, 12 January 2017

PAMPASI ZINAMADHARA KWA MTOTO


Uchunguzi umebaini madhara hayo hutokea kwa kuwa pampasi zina uwezo wa kuhifadhi choo cha mtoto baada ya kujisaidia bila ya kupenya au kuvuja kwa upande wa pili kama ilivyo kwa nepi za kawaida.
 Hivyo, hali hiyo huweza kusababisha magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.
Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na daktari wa magonjwa ya kina mama na watoto, Mr. Bujiku Constantine ambaye alieleza kuwa watoto wengi huugua magonjwa mbalimbali kutokana na matumizi ya pampasi, kama magonjwa hayo hayatatibika mara moja huweza kusababisha vifo kwa watoto.
Akifafanua baadhi ya magonjwa hayo, Dr. Bujiku alisema kuwa mtoto anayevalishwa pampasi huwa katika hatari ya kupata U.T.I (Urinary Tract Infections), Dermatitis (ugonjwa wa ngozi), Fangasi na Mabadiliko ya PH (kiwango cha tindikali) hasa katika sehemu za haja kubwa na ndogo, kutokana na unyevunyevu unaokaa kwa muda mrefu ndani ya pampasi hizo mara baada ya mtoto kujisaidia.
Akizungumza kwa msisitizo Dr. Bujiku alisema mtoto ambaye huvalishwa pampasi huwa katika hatari zaidi kuliko yule ambaye hutumia choo cha moja kwa moja.
“Magonjwa yote niliyoainisha hapo juu huweza kusababisha madhara tofauti kwa watoto ndani ya siku chache za matumizi ya pampasi.
“Kwa mfano U.T.I husababisha uchovu, maumivu ya mgongo, kuharibika kwa viungo vya uzazi, kuharibika kwa mfumo wa mkojo na kushindwa kufanya kazi kwa figo. Fangasi yenyewe, husababisha muwasho wa mara kwa mara, kuchubuka kwa ngozi na mara nyingine fangasi hao husambaa sehemu zote za siri za mtoto na kuingia ndani ya utumbo na kusababisha tatizo la fangasi tumboni.
“Dermatitis husababisha muwasho na harara katika sehemu za siri za mtoto hasa sehemu ambazo hufunikwa na pampasi hiyo. Hivyo kama  magonjwa yote hayo hayatapatiwa tiba ya haraka, mtoto anayeugua anaweza kuwa katika hatari ya kifo,”
alisema Dr. Bujiku.

Wednesday, 11 January 2017

FAHAMU CHANZO CHA TATIZO LA KUATHIRIKA TEZI DUME, DALILI NA TIBA




TATIZO LA TEZI DUME.

Ni ile hali ya tezi dume kuathirika kutokana na vyanzo mbalimbali mfano, bacteria n.k,kuathirika kwa hii tezi dume kunaweza sababisha hata utendaji kazi wake kupungua,na inapatikana chini ya kibofu cha mkojo kazi yake kubwa ni kuzalisha manii kwa ajili ya kurutubisha na kusafilisha mbegu za kiume kutoka kwenye korodani,tatizo hili lina waathiri wanaume bila kujali lika lakini wanaume kuanzia miaka 50 wameonekana kuathirika zaidi na hili tatizo


CHANZO CHA TATIZOChanzo kikubwa cha hili tatizo ni kushambuliwa kwa tezi dume na bacteria mbalimbali ambao wanaweza kuwa ni visababishi vya magonjwa mbalimbali ya zinaa mfano,kaswende,kisonono,pangusa n.k au bacteria wanao shambulia mfumo wa mkojo(UTI)wanaweza kupenya na kuifikia tezi dume na kuishambulia,vyanzo vingine ni kushuka kwa kinga za mwili na ajali zinazopelekea kuumia katika eneo ambalo tezi dume ipo pia kunamazingira hatarishi yanayo pelekea mwanaume kuathirika na hili tatizo;Kama mwanaume alishawahi kuwa na hili tatizo na hakupata matibabu sahihiKuwa na maambukizi katika kibofu cha mkojo au mrija unao tiririsha mkojo (urethra)Kutokunywa maji ya kutoshaKuwa na wapenzi wengi na kushiriki tendo la ndoa na mpenzi mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa na HIV/AIDS







DALILI ZA HILI TATIZOMaumivu wakati wa kutoa haja ndogo au kuhisi kama mkojo ni wa moto na maumivu wakati wa kufika kileleniKwenda haja ndogo mara kwa maraMtiririko wa mkojo kuwa dhaifuMaumivu chini ya kitovuMaumivu ya kiuno na chini ya mgongoMaumivu ya sehemu ambayo ipo katikati ya korodani na sehemu ya kutolea choo kubwaMaumivu ya korodani na uumeMwanaume mwenye tatizo hili anaweza akawa na homa




MATIBABUMatibabu ya hili tatizo yanategemea na chanzo chake hivyo kwa mwanaume yeyote mwanye dalili zinazofanana na zilizo tajwa hapo juu awahi mapema kutibiwa au atembelee VICTORIA THERAPIES iliyoko mtoni kijichi DSM kwa ajili ya vipimo,matibabu pamoja na ushauri jinsi ya kuondokana na hilo tatizo




MADHARA ENDAPO MATIBABU YATACHELEWAKusambaa kwa bacteria mbalimbali katika damu(bacteremia)Kuwa na jipu kwenye tezi dume(prostatic abscess)Ugumba kutokana na kuathirika kwa manii,mbegu za kiumePia tatizo hili linaweza likasababisha kansa ya tezi dume(prostate cancer ).

Ni mimi Archandramu Mbungu.
               Mwanasaikologia
               Mtoa Ushauri Nasaha
 Namba ..0766245554
                0658245554

UGONJWA WA KIFUA KIKUU NA DALILI ZA KIFUA KIKUU




Kifua kikuu ni ugongwa unaosababishwa na vimelea vidogo vidogo aina ya bakteria viitwavyo Microbacteria tuberculosis. Ugonjwa wa kifua kikuu unaenezwa kwa njia ya hewa kutoka katika mtu ambaye anaugua na hajaanza matibabu, mtu huyu akipiga chafya, kukohoa au kutema makohozi ovyo anaweza kuambukiza watu wengine.Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, pia kinaweza kuathiri sehemu yeyote ile nyingine ya mwili ikiwemo mifupa, tumbo na mgongo.





Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kukohoakwa wiki mbili au zaidi mfululizo, homa za mara kwa mara kwa wiki mbili au zaidi, kutokwa na jasho jingi hasa nyakati za usiku, kukohoa makohozi yenye damu, kupungua uzito zaidi ya kilo 3 ndani ya wiki 4 au kukonda pamoja na kukosa hamu ya kula.Kifua kikuu hugundulika kwa kupima makohozi na ikibidi x-ray na matibabu yake ni bure katika hospitali zote za serikali na binafsi. 





Unapoona mtu ana dalili mojawapo kati ya hizi au wewe mwenyewe mshauri awahi kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi na tiba au awasiliane na mratibu wa kifua kikuu na ukoma aliye karibu nae kwani mtu mmoja huweza kuwaambukiza watu kati ya 10 hadi 15 kwa mwaka kama hajapata matibabu. Wastani wa watu 176 huugua kifua kikuu kila siku nchini Tanzania na wastani wa watu 12 hufariki dunia kila siku .






Ikitokea umegundulika kuwa una kifua kikuu usihofu kwani kinatibika na mamilioni ya watu duniani kote wameugua na kupona. Unachotakiwa kufanya ni kufatisha masharti utakayopewa na daktari kama; kunywa dawa kila siku kwa muda uliopangiwa ili kupona kabisa.





Matibabu yake huchukua kati ya miezi sita hadi minane.Endapo umegundulika kuwa na kifua kikuu kumbuka kufunika mdomo na pua unapo kohoa au kupiga chafya, ili usiambukize watu wengine na pia usiteme mate ovyo.Pumzika kiasi cha kutosha, kula chakula bora na uwafahamishe ndugu na marafiki kwamba unaugua kifua kikuu na uko kwenye matibabu, na ukisha kamilisha matibabu nenda kwa mhudumu wa afya kwa uchunguzi ili kuthibitisha kama umepona.Kumbuka ni muhimu kuendelea kutumia dawa mpaka mwisho hata kama unajisikia vizuri ili usipate kifua kikuu sugu ambacho matibabu yake ni magumu. 





Mara kwa mara kifua kikuu kimekuwa kikihusishwa na ugonjwa wa ukimwi kwani asilimia 50 ya watu wenye kifua kikuu wana VVU. Kama umethibitika una kifua kikuu ni muhimu kupata ushauri nasaha na kupima virusi vya UKIMWI, kwani asilimia 10-15 ya watu wanaoishi na VVU wanaugua kifua kikuu, hivyo ni muhimu kuchunguzwa kama una kifua kikuu ili kuboresha na kuokoa maisha yako kwani kifua kikuu kinatibika kabisa hata kama una maambukizi ya VVU.

Ni mimi Archandramu Mbungu
              Mwanasoikolojia
               Mtoa Ushauri Nasaha

Wednesday, 28 December 2016

JINSI YA KUZUIA MIMBA KWA NJIA ZA ASILI


Njia ya asili ya kuzuia mimba ni mbinu pekee ambayo wanamama wa miaka ile kabla ya madawa ya kisasa(kizungu) kugunduliwa. 

Njia hii inauhakika wa asilimia 96-mpaka 98 kama zilivyo njia nyingine za kuzuia mimba kama vile vidonge, sindano, patch, Coil. 

Njia nyingine asilia ni kumwaga nje(withdrawn), lakini hii unahitaji zaidi ushirikaino wa mpenzi wako, mawasiliano wakati wa tendo kwani akijisahau au kuchelewa ujue kitu na box.


Mipira (Condoms) ndio kinga pekee inayozuia mimba na magonjwa yote ya ngono kwa asilimia 99 na ile moja iliyobaki ni kwa ajili ya sababu za kisheria kulinda Makampuni incase mtu akatumia vibaya na kushika mimba au gonjwa la zinaa. Vilevile Kinga hii (Condom) ndio pekee ambayo ham-badilishi mwanamke kihomono au kimaumbile.

Njia ya asili ya kuzuia mimba hutumiwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine hawataki kutumia madawa ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya miili yao kama vile kunenepa, kutokwa na majimaji ukeni na pia kuna tetesi kuwa yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata Saratani ya Kizazi na Matiti.

Kuzuia mimba kwa kutumia tarehe inauhakika ikiwa mzunguuko wako ni uleule na sio mrefu (siku 32-35) wala mfupi (siku 18-24) bali ni ule wa kawaida ambao ni siku 28. 
 
Ili kutumia mtindo/mbinu hii ya kuzuia mimba unapaswa kuanza kuhesabu siku zako sasa na fuatilia kwa karibu mzunguuko wako na kuhakikisha kuwa una siku 28 sio chini wala juu ya hapo.
 
Kwa kawaida unaaza akufuatilia kwa miezi mitatu hadi sita (kama umewahi kutumia madawa ya kuzuia mimba) kabla hujaanza kuitumia njia hii.

Namna ya kuhesabu 
Ili kuwa na uhakika na urefu au ufupi wa mzunguuko wako unapaswa kuhesabu siku ya kwanza utakayo ona damu mpaka utakapo ona damu ya mwezi utakao fuata.

Mfnleo tarehe 9 mwezi wa nanendio umeanza hedhi basi hedhi ya mwezi ujao itakuwa tarehe 7 mwezi wa tisa.....hii ni kama mzunguuko wako usiobadilika (sio mrefu au mfupi) ambao ni siku ishirini na nane tu.

Siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya tisa ni salama na huwezi kushika mimba.
 
Baada ya hapo mpaka siku ya kumi na nne (yai linapevuka) unakuwa hatarini.
 
Siku ya kumi na saba mpaka siku yaishirini na mbili unakuwa salamatena mpaka siku ya ishirini na tatumpaka ishirini na saba (yai pevu linashuka) hatarini 
 
Lakini ile ya ishirini na nane siku ya hedhi nyingine unakuwa salama tena......

Ili kuwa na uhakika kuwa uko kwenye mstari kuliko kuegemea kwenye tarehe tu unatakiwa kujua mabadiliko ya mwili wako.
 
 Unapokuwa hatarini kushika mimba mara nyingi utahisi nyege zaidi n avilevile utoko wako utabadilika na kuwa mlaini zaidi (kama lotion) na wakati mwingine utahisi ute unatoka (ule kama udenda/mlenda)....ukiona hivyo hakikisha unatumia Condom vinginevyo utashika mimba.

Unapokuwa salama mara nyingi hamu ya kungonoka inakuwa haipo sana unless "uchokozwe", vilevile utoko wako unakuwa mzito (kama cream/mafuta mazito)na mweupe sana yaani hata wakati wa kujiswafi inakuwa taabu na inaweza kukuchukua muda mrefu zaidi. 
 
Hali ikiwa hivi ujue uko salama  kusex bila kinga ya kuzuia mimba.