HESLB KUKUTANA NA MAAFISA MIKOPO VYUO VYA ELIMU YA JUU
Maafisa mikopo zaidi ya 80 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu (HLIs) nchini watakuwa na kikao kazi cha siku mbili ili kuboresha huduma za utoaji wa mikopo kwa wanufaika wanaoendelea na masomo.Kikao hicho cha siku mbili kitafanyika kesho tarehe 16 na 17 Machi 2017 katika Chuo Kikuu Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano Dkt. Cosmas Mwaisobwa ambaye anaratibu kikao hicho, amesema kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka, kinalenga kuwapa maafisa mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu mikakati mipya ya jinsi ya kusimamia madawati ya mikopo kulingana na mabadiliko ya kimifumo na kiutendaji kuhusiana na utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Kikao hicho pia kitatumika kama njia ya kupokea mrejesho wa maafisa mikopo wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa watendaji wa Bodi ya Mikopo.
No comments:
Post a Comment