Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Monday, 13 February 2017

Yapo Mengi Lakini Haya ni Matukio Matano Yaliyoishangaza Dunia

KUNA mambo mengi yamekuwa yakitokea duniani, yanashangaza na wakati mwingine mtu kujiuliza kwamba inawezekanaje jambo hilo kutokea? Tangu dunia ilipoumbwa, kuna mambo mengi yalitokea kuanzia karne ya 18 mpaka karne hii ya 21.
Yapo yaliyotokea kwa makusudi lakini pia yapo yaliyotokea kwa bahati mbaya kabisa ambayo kwa kifupi tungesema Mungu alitaka hayo yatokee ili iwe fundisho kwa watu wanaoshuhudia au akusikia. Haya hapa ni baadhi ya mambo matukio matano ambayo yaliishangaza dunia.
Kulipuliwa kwa Majengo ya Biashara (WTC) jijini New York
Ilikuwa asubuhi ya tarehe 11/09/2001. Wafanyakazi walikuwa ndani ya majengo mawili ya biashara (WTC) wakiendelea na kazi zao kama kawaida. Ghafla waliiona ndege ya kwanza ikienda kwa kasi katika jengo leo.
Walipiga kelele, walishangaa kwani haikuwa kawaida kwa ndege kutoka uwanja wa ndege na kulifuata jengo moja na kuligonga. Walikufa watu wengi na wengine kuachwa majeruhi. Wakati watu wakijiuliza ni kitu gani kilitokea, ghafla ndege ya pili ilionekana ikilifuata jengo jingine ambalo ni pacha ya lile la kwanza na kuligonga.
Kwa taarifa za CIA, hii haikuwa bahati mbaya, lilikuwa ni tukio lililopangwa, la kigaidi ambalo lilifanywa na Kundi la Kigaidi la Al Qaeda lililokuwa chini ya Osama Bin Laden. Katika tukio hilo kubwa, liliua watu 2996 na kujeruhi watu 6000 na kuleta hasara ya dola trilioni 3.

Kulipuliwa kwa Miji ya Nagasaki na Hiroshima.
Ni mwaka 1945 ambapo Vita vya Pili vya Dunia (WWII) vilikuwa vimepamba moto. Mataifa mengi yakaungana kwa ajili ya kushambuliana huku Ujerumani iliyokuwa chini ya Adolf Hitler ikiwa imeungana na Italia, Japan na nchi nyingine.
Zilikuwa zikipambana na kundi jingine lililokuwa na nchi kama Uingereza, Ufaransa na nchi nyinginezo. Vilikuwa vi vita vikali, walipambana kwa nguvu kubwa na ndiyo ilikuwa vita pekee ambayo Marekani aliitumia kutengeneza nchi yake.
Wakati wenzake wakiwa kwenye vita, kazi yake ilikuwa ni kuitengeneza nchi, alikuwa akiwauzia Waingereza na wenzao nguo, chakula na silaha. Vita viliendelea mpaka pale ndege ya Marekani ilipolipuliwa na Japan kitu kilicholeta mtafaruku mkubwa kwamba kwa nini Japan ailipue ndege hiyo, huku japan akiinuka na kusema kwamba kwa nini Marekani awauzie Waingereza silaha na chakula na wakati yeye hakuhusika kwenye vita hivyo?
Japan hakubaki kimya, alidhamiria kumuingiza Marekani katika ugomvi huu kwa kushambulia miji kadhaa nchini Marekani. Hapo ndipo rais wa Marekani Harry S. Truman alipouliza kuhusu silaha walizokuwanazo na kuambiwa kwamba walikuwa na mabomu mawili ya nyuklia na yalikuwa hatari sana. Akaagiza hayohayo yaende kushambulia Miji ya Nagasaki na Hiroshima nchini Japan. Kilichotokea huko, hakika Wajapan hawatokisahau na kuanzia siku hiyo, hawakutaka tena vita.

Kifo cha John F Kennedy
Ni mwaka 1963 ambapo Rais wa 35 wa Marekani, John F Kennedy alikuwa kwenye msafara wake uliokwenda kutembelea Jiji la Dallas, Texas. Wakati akiwa na mkewe kwenye gari lililokuwa wazi kwa juu, jamaa mmoja aliyeitwa Lee Harvey Oswald (Mdunguaji) alikaa kwenye ghorofa akiwa na bunduki yake kisha kumpiga risasi Kennedy kwenye kichogo na kufariki hapohapo.
Huyo alikuwa rais wa mwisho wa Marekani kuuawa na tangu siku hiyo wakatangaza kwamba hakutokuwa na rais wao yeyote atakayeuawa, hivyo wakaongeza ulinzi maradufu. Kwa muuaji Oswald, alikamatwa ila kabla ya kupewa hukumu yake, akauawa gerezani kwa kitu kilichohusishwa kwa kupoteza ushahidi.
Mwanadamu wa kwanza kufika mwezini
Hebu usiku toka ndani na kwenda nje, kisha angalia angani, bila shaka utauona mwezi, si upo mbali, basi nataka nikwambie kwamba katika matukio yaliyowahi kuishangaza dunia ni kitendo cha binadamu wa kwanza kufika huko.
Ilikuwa mwaka 1968, Mmarekani, Neil Armstrong alipoamua kufika mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11. Ilionekana kama kushindikana lakini mwisho wa siku mtu huyo alifika huko na kukaa kwa saa 21. Alipofika, kwanza hakutoka nje ya chombo hicho kwa muda wa saa sita, alibaki ndani huku akijiuliza kama alitakiwa kutoka au la, ila mwisho wa siku akatoka.
Dunia iliweka historia, kila mtu akamuona Armstrong kuwa shujaa mkubwa ambaye alifanya kile ambacho binadamu wengine waliona kwamba isingewezekana hata kidogo. Baada yake, kulikuwa na watu wengine waliokwenda. Kwa sasa, watu wanafikiria kwenye sayari ya Mars.

Kuzama kwa meli ya Titanic
Ilikuwa mwaka 1912 siku ambayo meli ya Titanic ilitakiwa kuanza safari yake kutoka Southampton nchini Uingereza na kwenda New York nchini MArekani.
Ilikuwa meli kubwa na watu walioitengeneza walijivunia kwa kusema kwamba isingeweza kuzama kwani ilikuwa imara sana, tena sana.
Meli hii ilibeba abiria 2224 na ilipozama siku nne baadaye iliua abiria 1635. Mara baada ya taarifa kutangazwa, watu wengi walishtuka kwani waliamini kwamba kwa ukubwa wa meli hiyo, uimara wake usingeweza kuzama hata mara moja na waliamini kwamba ingefanya safari ndefu kuliko meli zote.
Meli hiyo ilizama baada ya kugonga mwamba wa barafu katika Bahari ya Atlantiki inayotenganisha Marekani na Bara la Ulaya.

Sunday, 29 January 2017

Breaking News!! TRENI YA MWENDO WA HARAKA - DELUX YAANGUKA LEO PWANI IKITOKA KIGOMA KWENDA DAR


TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma  kwenda jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani leo jioni Jumapili Januari 29, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 kati ya 20 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.

Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.

“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.

Mkataba ujenzi treni ya umeme kusainiwa wiki mbili zijazo


Dar es Salaam. Serikali imesema itasaini mkataba na mkandarasi baada ya wiki mbili kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati itakayotumia treni ya umeme, kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ambayo itatumia saa 1:30 kwa safari.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema hayo jana alipokuwa anahutubia wahitimu kwenye mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
“Naomba kwa sasa msiniulize ni mkandarasi gani atasaini ila wakati ukifika kila kitu kitakuwa hadharani, reli hii haitatumia gari moshi ni umeme,” alisema Profesa Mbarawa.
Alisema reli hiyo itakuwa na mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa.
Januari 26 mwaka huu, Rais John Magufuli alipokuwa anazindua mradi wa magari yaendayo haraka (BRT) maarufu kama mwendokasi alisema Serikali inapitia zabuni ili kumpata mkandarasi atakayejenga reli hiyo yenye urefu wa kilometa 200.

BREAKING NEWS: Geita Nyarugusu waokoaji wafanikiwa kuwaokoa watu waliofukiwa na kifusi.

Waokoaji wamefanikiwa muda huu kuwaokoa wachimbaji waliofukiwa, sasa hivi wamemtoa mtu wa 15 ambaye ni Mchina








Saturday, 28 January 2017

BREAKING NEWS: RADI YAUA MMOJA NA KUJERUHI KADHAA- TUKUYU

Mti ukiwa umechanwa chanwa na Radi
Wakati mwingine watu hujiuliza mengi pasipo kupata majibu.
Ikiwa hali ya unyeshaji wa Mvua nchini Tanzania kwa Mikoa mbalimbali haijawa Imara hali inayowawazisha Watanzania wengi.
Kwa mshituko Mkubwa ulioikumba Jamii ya Wananchi wa Mjini Tukuyu hivi punde ni  Tukio la majonzi ambapo Radi iliyoambatana na Ngurumo kubwa imesababisha Kifo cha mtu mmoja maeneo ya  stendi -Tukuyu na wanawake wawili wamekimbizwa hospital Makandana Tukuyu
Wananchi wa Tukuyu wakiwa Eneo la Stendi ya Tukuyu kutazama jinsi Radi ilivyoshambulia mti na kusababisha mauti na majeruhi
Wananchi wakitazama maajabu ya Radi na kuchukua picha za kumbukumbu

Friday, 27 January 2017

AMUUA MKWE KISA TSH 200

MKAZI wa kijiji cha Mwamgongo mkoani hapa Zubeda Said (33) anadaiwa kupigwa na mumewe hadi kuuawa baada ya kupoteza Sh 200.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, dada wa marehemu, Siwema Masoud alidai kuwa awali ndugu yake huyo alimpigia simu kuwa Januari 19 usiku alipigwa na mumewe kwa kupotea Sh 200.

Alisema siku moja kabla alimpa mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka mitano Sh 200 akanunue maandazi, lakini mtoto huyo aliporwa fedha hiyo na wenzake, akashindwa kurudi nyumbani kwa siku mbili, akarudi siku ya ugomvi wa wawili hao na mumewe kukasirika.

Alidai kuwa mume huyo, Kunduwenda Kiza (37) akimfokea mtoto huvyo mama mtu kuamua kumwomba radhi mumewe huyo lakini bila mafanikio kwani katika hali ya kushangaza mumewe alimpiga mpaka kupoteza fahamu.

Siwema asilimulia kuwa kesho yake saa 9.45 alfajiri hali ya Zubeda ilibadilika na  kutokwa damu sehemu mbalimbali zilizo wazi mwilini mwake, mumewe akamkimbiza kwenye zahanati ya kijiji hicho na Januari 20, alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa ya Maweni.

Alisema  Januari 21, saa 12.45 Zubeda alipoteza maisha hali iliyowapa mashaka na kufikisha taarifa Polisi  kwa uchunguzi maiti lakini walipokwenda na askari hospitalini wakaambiwa jalada halionekani.

Hata hivyo, mganga aliyetambuliwa kwa jina la Dk Muganyizi alijitolea na kuufanyia uchunguzi mwili huo na baada ya uchunguzi maiti alibaki mochari.

Lakini wakati ndugu wakijiandaa kwenda kuchukua mwili walishangaa kukuta umeondolewa, na kwa msaada wa polisi waliukamata ukisubiri kusafirishwa kinyemela.


Mwandishi alifika Maweni na kugundua kuwa kabla ya kifo alilazwa wodi 2(b) ya wanawake huku jalada lenye taarifa zake likiwa limetoweka huku uchunguzi wa Mganga ukibaini kuwa na majeraha ndani ya mwili yaliyosababisha kuvuja damu kulikochangia kifo hicho.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ferdinand Mtui  alikiri kupokea taarifa za kifo cha kutatanisha cha Zubeda.

Kamanda Mtui alisisitiza kuwa mshukiwa Kiza anashikiliwa na Polisi   kwa upepelezi na ikibainika ametenda kosa hilo, atafikishwa mahakamani.

Saturday, 10 December 2016

DARASA APOLA NYOTA YA DAIMOND AFRIKA MASHARIKI KWA GHAFLA.

Ni baada ya kutoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la MAISHA NA MUZIKI