Raia 58 wa Tanzania ambao walikuwa wanaishi nchini Msumbiji wamefukuzwa nchini humo na kurudishwa Tanzania huku wakidai kunyang’anywa mali zao, vitambulisho pamoja na hati za kusafiria na askari wa Msumbuji.
Watanzania hao kabla ya kufikishwa kwenye mpaka wa Tanzania na Msumbiji mpaka wa Kilambo waliwekwa ndani ya mahabusu kwa siku tatu.
Raia hao watanzania ambao wamefukuzwa nchini Msubiji wamesena Wameacha mali zao, fedha walizokuwa nazo mifukoni wameporwa na askari wa Msumbiji wakati wanakamatwa, sehemu zao za biashara ambazo walikuwa wamefungua wameziacha wazi, bila kufuata taratibu raia hao waliwekwa mahabusu na baada ya siku tatu wakafikishwa mpaka wa Kilambo mkoani Mtwara ambao ni mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
Wakiwa mkoani Mtwara raia hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali hapa nchini wameiomba serikali kuwasaidia kwani hata mawasiliano na ndugu zao yamekuwa magumu kutokana kuporwa simu na askari wa Msumbiji.
Naibu kamishina wa uhamiaji ambae ni afisa uhamiaaji wa mkoa wa Mtwara Rose Mhagama anasema kitendo hicho kinatoa taswira mbaya kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Msumbiji licha ya kuwa na uhusiano mzuri na ujirani mwema.