Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Wednesday, 1 February 2017

TUKIO JINGINE:WATU SITA WAPOTEA ZIWA TANGANYIKA, HADI SASA HAWAJULIKANI WALIPO

Wakazi sita wa Manispaa ya Kigoma Ujiji waliokuwa wakisafirisha bidhaa zao kutoka eneo la Kibirizi kwenye Manispaa  ya Kigoma kuelekea Kalemii nchi jirani ya DRC Congo  wamepotelea ziwa Tanganyika tangu Januari 23 mwaka huu hadi sasa.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Feldinand Mtui amesema boti ya mizigo iliyojulikana kwa jina la MV Ngendo ya Buchwa ambayo iliondoka katika eneo la Kibirizi januari 23 mwaka huu ikieleke DRC Congo ikiwa na watu sita na bidhaa ambayo haija fika ilipokukuwa ikielekea jambo lililosababisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ushiriki na wamiliki wa maboti mkoa kuanza kufanya msako maeneo mbalimbali ya ziwa Tanganyika.

Aidha kwa upande wa mwenyekiti wa usafirishaji mkoa Edimund Kisinja anaeleza uzoefu wa usafirishaji wa mizigo kuelekea nchini jirani ya DRC Congo ambapo pia na ndugu na jamaa  wanaeleza maoni yao.

Sunday, 18 December 2016

UGONJWA WA INI NI HATARI KULIKO UKIMWI



 
Mojawapo ya njia zinazoambukiza ugonjwa wa Homa ya Ini.

Ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.
Virusi hivyo vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus).
Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho.
Watu takribani 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa homa ya Ini (Hepatitis B).

HEPATITIS B INAVYOSAMBAZWA
Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.
Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na muingiliano wowote ule wa damu katika maana pana. Vilevile kuchangia taulo na mwenye Virusi vya homa ya ini, kubadilishana naye nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho ni hatari sana.
Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa Virusi vya Hepatitis B ni hatari kuliko hata vya Ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba. Virusi vya Ukimwi (HIV) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.
Kwa wastani kirusi cha Hepatitis B kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. Ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika kama atapimwa.
Mtu mwenye homa ya ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye Ukimwi. Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye HIV.

DALILI
Watu wengi huwa hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.
Hata hivyo, watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa. Dalili hizo ni ngozi na macho kugeuka njano. Hii kwa kawaida huitwa Jaundice, yaani homa ya nyongo au manjano.
Dalili nyingine ni mgonjwa kujisaidia mkojo mchafu (mweusi), uchovu wa mara kwa mara, kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo.
Kwa wagonjwa wengine, Virusi vya Hepatitis B hukua mpaka kusababisha ini kuharibika kabisa (cirrhosis of the liver) au saratani ya ini (liver cancer).

HAUNA TIBA
Mpaka sasa Hepatitis B hauna tiba, vilevile hakuna dawa maalum za kurefusha maisha. Ugonjwa huo ukishafikia kiwango cha ini kuharibika au kupata saratani ya ini, maana yake ni kiwango cha mwisho kabla ya kifo.

KUNDI LIPI NI HATARI ZAIDI?
Asilimia 80-90 ya watoto wachanga ambao huambukizwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzaliwa, homa ya ini (Hepatitis B) hukua mpaka kufikia kuwa sugu na hatimaye kifo.
Asilimia 30-50 ambao huambukizwa kabla ya kufikisha umri wa miaka sita, Hepatitis B hukua mpaka kuwa sugu na baadaye ni kifo.
Asilimia 90 ya watu wazima wanaopata HBV, virusi hivyo hutoweka ndani ya miezi sita. Yaani uimara wa ini husababisha virusi hivyo kupotea.
Asilimia tano kushuka chini ya watu wazima wanaopata maambukizi ya HBV, virusi hivyo vya Hepatitis B kugeuka sugu na hatimaye kifo.
Asilimia 15-25 ya watu wazima huwa wamepata maambukizi utotoni na hatimaye Hepatitis B kuwa sugu, hufariki dunia kutokana na matokeo ya ini kuharibika kabisa (cirrhosis of the liver) au kuwa saratani ya ini (liver cancer).

TANZANIA IPO KUNDI LA KIFO
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Kusini ya Jangwa la Sahara ndiyo eneo hatari zaidi. Tanzania ni moja ya nchi zilizopo katika eneo hilo. Kiwango cha hatari Kusini ya Jangwa la Sahara kinalingana na kile cha Mashariki ya Bara la Asia.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa watu wengi walipata maambukizi nyakati za utotoni na kwamba kati ya asilimia tano mpaka 10 ni waathirika sugu.

TUUTOKOMEZE UGONJWA HUU
Kwa kutambua yote hayo, Global Publishers Ltd, imeanza rasmi kampeni za kuitokomeza hepatitis B ambazo zitaambatana na uzinduzi wake kitaifa uliofanyika Machi 7, mwaka huu, Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Ilala, Amana, Dar es Salaam, mgeni rasmi akiwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (pichani).
Mkurugenzi wa Global Publishers, Ericc Shigongo alisema alipozungumza na www.uchaguzinawagombea.blogspot.com, dhamira kuu ya kuanza mbio hizo za kuutokomeza ugonjwa huo ni kwa sababu unaua watu wengi na ni hatari sana kwa kizazi cha sasa na kijacho.
“Ni lazima tuungane kama taifa, huu ugonjwa ni hatari sana, sisi Global Publishers tumeanza, kinachofaa ni wewe na yule kujitokeza ili tuishinde hii vita tukiwa pamoja,” alisema Shigongo kisha akaongeza:
“Ndugu zetu wengi sana wanapoteza maisha kila siku kutokana na hepatitis B (homa ya ini), tiba yake hakuna lakini chanjo ipo, kwa hiyo sisi Global Publishers tumeona kuchukua jukumu la kuhakikisha hepatitis B inatokomezwa.”