Wakazi sita wa Manispaa ya Kigoma Ujiji waliokuwa wakisafirisha bidhaa zao kutoka eneo la Kibirizi kwenye Manispaa ya Kigoma kuelekea Kalemii nchi jirani ya DRC Congo wamepotelea ziwa Tanganyika tangu Januari 23 mwaka huu hadi sasa.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Feldinand Mtui amesema boti ya mizigo iliyojulikana kwa jina la MV Ngendo ya Buchwa ambayo iliondoka katika eneo la Kibirizi januari 23 mwaka huu ikieleke DRC Congo ikiwa na watu sita na bidhaa ambayo haija fika ilipokukuwa ikielekea jambo lililosababisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ushiriki na wamiliki wa maboti mkoa kuanza kufanya msako maeneo mbalimbali ya ziwa Tanganyika.
Aidha kwa upande wa mwenyekiti wa usafirishaji mkoa Edimund Kisinja anaeleza uzoefu wa usafirishaji wa mizigo kuelekea nchini jirani ya DRC Congo ambapo pia na ndugu na jamaa wanaeleza maoni yao.
No comments:
Post a Comment