Thursday, 30 November 2017

Neno *"Eden"* ni neno la Kiebrania *"Makazi ya Mungu"*. Hivyo kitu cha kwanza Mungu kumpa mwanaume ni *"Uwepo wake(his presence)"*.

(1) Hivyo kitu cha kwanza kwa mwanaume sio *mwanamke,* bali *uwepo wa Mungu*, na anapaswa kukutana na mwanamke katika uwepo wa Mungu. Eve na Adam walikutana katika bustani ya Eden.

(2) Kitu cha pili Mungu kumpa mwanaume baada ya kumuweka katika bustani ni KAZI. (Mwanzo. 2:15).
Mungu alimpa mwanaume kazi kabla ya mwanamke. Inamaanisha mwanume anahitaji kazi kwanza kabla ya mwanmke,vipaumbele vya Mungu viko wazi kabisa.

(3) Kitu cha tatu Mungu alimwambia mwanaume *"palilia"*......
Kupalilia hapa kunamaanisha, leta matokea chanya katika kila kitu kinachokuzunguka, zidisha ufanisi na ubora katika kila kitu na kila MTU, kufanya kila kitu kitoe matunda . Aliongea hivyo kwa mwanaume tu!

Ndio maana Mungu hatampa mwanaume *Mwanamke mtimilifu*.

Mwanaume aliumbwa na Mungu ili kuumba chochoe akitakacho. Mwanmke umtafutaye hayupo na hajawahi tokea; Yupo kichwani mwako. Kazi yako ni kuchukua malighafi zilizopo kumpalilia mwanamke aliye kichwani mwako. Hivyo umeoa ni miaka ishirini (20) sasa na bado hupendi aina ya mwanamke uliyenaye, *Hilo ni kosa lako.*

(3a) Ikiwa mkeo anaongezeka uzito na hupendi hilo, *usimlaumu;* ni kazi yako kumuamsha SAA kumi na mbili asubuhi, *"Mpenzi amka twende Jogging".*

(3b) Hupendi mavazi? Mpeleke kwenye Duka la nguo mnunulie uyapendayo.

(3c) Hawezi kuongea kiingereza vizuri? Mpeleke shule mlipie ada ya masomo ya ziada *mpalilie!!!!*

(4) Kitu cha NNE Mungu alimwambia mwanaume, *"Linda bustani"*.Mwanaume alitakiwa kuwa mlinzi au mwangalizi wa kila kitu chini yake.Ndio maana Mungu alikupa jina imara. Mkusanyiko wa misuli mikubwa na imara, sio kwa ajili ya kumuonea na kumnyanyasa mwanamke, ila * Kumlinda mwanamke*.

(5) Kitu cha mwisho Mungu alimpa mwanaume  *Neno*... Mungu alimwambia mwanaume asiguse mti wa wa kati; Mungu hakumwambia mwanamke kuhusu mti *KATU!!!*..... Manaake ni kuwa mwanaume ndie aliyepokea neno na ni jukumu lake kumfundisha mwanamke neno la Mungu.

Zingatia: Hapana kitu humvunja moyo mwanamke kama kumuuliza mwanaume *"unafikiri nini"* na jibu likawa dhaifu *Vyovyote vile ni sawa"*....au kukaa kimya.......mmmm!!!

Usifanye hivyo kaka, Usifanye hivyo.anahitaji *Maarifa(knowledge) na uelekeo(direction)*. Hiyo ilikuwa amri ya mwisho Mungu alimpa mwanaume, mstari wa 17.

★Tizama hii: Katika mstari wa 18 , Mungu anasema*"Si vyema MTU huyu kuwa peke yake"*. Usisome mstari huo kwa haraka,sasa rudia pole pole, "Sio vyema kwa MTU huyu kuwa peke yake".
MTU GANI???

Jibu: Ni mwanaume :
*aliye katika uwepo wa Mungu
*aliye na kazi
*anaeweza kukupalilia
*anaeweza kukulinda
*anaeweza kukufundisha

Hivyo,haya ndio matatizo:

★ Ikiwa utakutana na mwanaume asiyependa uwepo wa Mungu,
Hafanyi kazi,
Hawezi kukupalilia,
Hawezi kukulinda na kukufundisha,hivyo....

NI VYEMA KWA MWANUME HUYO KUWA PEKE YAKE!
Full Stop!!

No comments:

Post a Comment