Saturday, 6 May 2017

AJALI: WANAFUNZI 29 NA WALIMU 3 WAPOTEZA MAISHA MKOANI ARUSHA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, RPC Charloes Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema kuwa, School Bus la shule hilo lilikuwa na jumla ya Wanafunzi 35, huku katika ajali hiyo Waliokufa ni 32 na wanafunzi watatu wakijeruhiwa vibaya.
RPC Mkumbo amesema kuwa, wananchi bado wanaendelea kusaidia katika uokoaji ambapo miongoni mwa waliokufa kati ya hao 32, ni walimu watatu nao wamepoteza maisha.
“Ni kweli, ajali imetokea na hapa tupo njiani na vijana wangu wapo eneo la tukio. Waliokufa ni 32. Wakiwemo wasichana na wavulana. Majeruhiwa wamekimbizwa Hospitali kwa matibabu” ameeleza RPC Mkumbo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mtandao huu.
Awali taarifa ilieleza kuwa, zaidi ya wanafunzi 20 wamepoteza maisha wakati wa Bus hilo la shule wakati wakielekea Karatu katika kufanya mitihani.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo ThobiasOmega blog imezipata  muda huu inaeleza kuwa,  ajali hiyo mbaya kabisa katika mkoa huo wa Arusha  imetokea eneo  la Kata ya Rhotia Wilaya ya  Karatu. Basi la wanafunzi wa St Lucky ya Arusha walikuwa wanaenda karatu kufanya mtihani na wanafunzi wenzao wa Tumaini English Medium School ya Karatu ndipo walipopata ajali hiyo.
THOBIAS OMEGA BLOG inaendelea kuwasiliana na vyanzo mbalimbali vya habari, na tutakuhabarisha hapahapa kujua idadi kamili pamoja na majina yao. Endelea kuperuzi mtandao wako ulio bora zaidi.

Miili ya baadhi ya wanafunzi ikiwa imewekwa pamoja mara baada ya ajali
Wasamaria wema wakiendelea kufanya uokozi
Gari la Shule la St.Lucky Vincent Nursery &Primary School kabla ya kuanza safari

No comments:

Post a Comment