Tuesday, 28 February 2017

WASANII BONGO MOVIE WAMPINGA VIKALI WEMA SEPETU, WAKANUSHA KUIDAI CCM


MOVIE BADO INAENDELEA: Hivyo ndivyo tunaweza kusema baada ya wasanii wa Bongo Movie Wasanii wa Bongo Movies waliokuwa wakishiriki kwenye kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya Mama Ongea na Mwanao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kukanusha taarifa iliyotolewa na Wema Sepetu kuwa CCM haijawalipwa pesa za kampeni walizofanya kwenye uchaguzi huo.

Mara baada ya Thea na Yobnesh kuzungumza maneno machache, mkutano huo na waandishi wa habari ulimalizika, ukiwa umechukua dakika chache tu na kuacha kila mtu akaizungumza lake.

“Ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama Mwenyekiti Msaidizi wa Muda, nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli… wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo.

“Zipo simu za kushwishiwa kuhama lakini hatutohama chama na Kundi la Mama Ongea na Mwanao litaendelea kuwepo chini ya Usimamizi wa Bi. Samia Suluhu.” Alisema Batuli.


Hivi karibuni msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu aliibuka mbele ya wanahabari wakati akihamia Chadema kwa madai ya kufanyiwa hila kwenye CCM huku akidai kuwa Kundi la Mama Ongea na Mwanao linakidai CCM pesa yao ya kampeni waliyofanya mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment