Tuesday, 28 February 2017

KINJEKITILE NGOMBARE MWIRU: HAIINGII AKILINI KILA MWENYE TUHUMA NA KASHFA AKIMBILIE UPINZANI

 
Mwanaharakati Kinje Ngombare Mwiru, amezungumza mtazamo wake kuhusiana na sakata zima la msanii Wema Sepetu kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo 
Amesema kitendo cha CHADEMA kumpokea Wema kinaonyesha dhahiri kwamba Vyama vya Upinzani vimeanza kupoteza mwelekeo kisiasa na vinashindwa kupambana na Chama cha Mapinduzi(CCM) ambacho kinashughulika na mambo mbalimbali yanayowakabili wananchi 

"Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani. Huo ni udhaifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa vyama hivyo, wameshindwa hoja za msingi kupambana na CCM sasa wanajisifu na kujigamba kwa kuwakaribisha watu watuhumiwa", alisema Kinje 

Aliongeza kwa kusema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona hata alipoingia Edward Lowassa CHADEMA , Chama hicho kilikosa hoja na ndipo kilipoanza kupoteza mwelekeo na matokeo yake yanaonekana katika uchaguzi ambapo CCM ilipata ushindi mkubwa 

Kitendo cha CHADEMA , kupokea wanachama wenye tuhuma mbaya ni dhahiri inaonesha chama hicho kimepoteza uelekeo na kukwamisha vyama vya upinzani 

Alimaliza kwa kusema wananchi wanapatwa na wasiwasi juu wanasiasa ambao ni watuhumiwa wa dawa za kulevya kuwepo kwao kwenye siasa ni kama maficho ya uharifu.

No comments:

Post a Comment