MWENYEKITI wa Bodi ya Parole, inayoshughulikia msamaha wa wafungwa magerezani, Agustino Mrema, amesema vita dhidi ya dawa za kulevya ameanza kupambana nayo baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli, kushika nafasi hiyo.
Mrema alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema muda mfupi baada ya kuanza kazi katika nafasi hiyo alianza kupambana na vita hiyo kwa kuzungumza na vijana wanaotumia dawa za kulevya ikiwamo kuwashawishi wawataje wafanyabiashara wa biashara hiyo haramu.
Aliongeza kuwa vijana hao walikuwa wanagoma kuwataja wahusika wakihofia usalama wao, lakini aliamua kuwapeleka katika vituo kwa ajili ya kuwasaidia kupata matibabu.
Mrema alisema kupambana na vita hivyo ilikuwa ni miongoni mwa mikakati yake aliyokuwa ameiweka baada ya kuteuliwa kuhakikisha anawaelimisha wananchi hususani vijana kuepukana na masuala ya uhalifu ambayo yangewasababisha kukutwa na hatia.
Pia alisema lengo lake ilikuwa ni kuhakikisha uhalifu unapungua na hivyo kuepuka kujaza magereza kutokana na masuala ya uhalifu.
"Kwa hiyo nina mshukuru sana Rais John Magufuli kwa kutia mkono wake katika suala hili la vita dhidi ya dawa za kulevya, mimi nilianza mapema kwa hiyo nashukuru imeendelezwa, naahidi tuko pamoja katika vita hii, hata ushauri nilishaanza kuutoa kwa vijana walioathirika," alisema Mrema.
"Nimekuwa nikitoa ushauri nasaha na elimu kuhusu umuhimu wa kutii sheria bila shuruti kwa makundi mbalimbali ya vijana kutokana na tabia na mienendo waliyonayo kuliko makundi mengine, lengo ni kuhakikisha hawaingii hatiani na hivyo kusababisha msongamano wa wafungwa kwenye magereza, mahabusu nchini yaani kupunguza idadi ya wafungwa watarajiwa."
Alisema vita nyingine alianza kupambana nayo kwa ajili ya kupunguza idadi ya wahalifu baada ya kuanza kazi hiyo ni waendesha bodaboda, vibaka, wasichana wanaouza miili yao, au dada pamoja na kaka poa

No comments:
Post a Comment