Mtunzi Jimmy Luoga
EPISODE:7
Ilipoishia tuliona Erick na Liz wanakubaliana kukutana fukwe ya Koko, siku inawadia Erick anakuwa wa kwanza kuwasili eneo hilo ambapo anaamua kukaa eneo la ufukweni akipunga hewa, baada ya dakika kadhaa mhudumu anakuja mahali alipo na kuambiwa ana mgeni wake upande wa bar, anapoungia pale bar anakutana na Liz akiwa amependeza maradufu na siku ile ya kwanza.Je nini kitaendelea?, ungana nami katika sehemu hii ya saba.
SASA ENDELEA.....................
Nilijongea mpaka kwenye ile meza ambayo Liz alikuwa ameketi peke yake, nilipokelewa kwa tabasamu zuri lililosheheni vema katika kinywa cha Liz, "karibu Erick!" yalikuwa maneno ya Liz nami nilishukuru kisha nilivuta kiti na kuketi jirani naye, Mhudumu alikuja kutusikiliza siku hiyo sikupenda kunywa Whysk kilevi ambacho nilikitumia mara kwa mara hivyo niliagiza chupa kubwa ya Amarula, nilipomueleza Mhudumu amsikilize Liz alikatiza na kusema yeye pia angetumia kinywaji hicho pia.Baada ya dakika kama tatu hivi Mhudumu alikuwa akilifungua lile chupa kubwa la Amarula kisha akatumiminia katika bilauli na kuondoka eneo hilo, taratibu tuliinua bilauli na kuanza kujigigidia ule mvinyo wenye asili ya utamu kama chocolate, mazungumzo ya hapa na pale yalichukua nafasi na kunifanya kwa mara ya kwanza kusikia kicheko cha Liz msichana ambaye kila nilipomtaza niliwaza namna ambavyo ningefanikiwa kumsaula nguo zake siku hiyo ili nifaidi ule ulimbwende wake.Baada ya mazungumzo ya hapa na pale huku tukiwa tunakunywa ile Amarula Liz aliomba nimuelekeze kiliko choo, nilimuita Mhudumu naye akaja na kuondoka nae, hapo ndipo nilipoweza kuufidi uzuri wa msichana huyo ambaye alivalia gauni fupi lililoonyesha vema miguu yake ya bia na lile umbo lake la kibantu ambalo lilinifanya nizidi kutamani usiku huo niwe nae, nyuma alifungasha hasa kiasi cha kuwafanya hata wale vijana waliokuwa wanacheza pool table wageuze shingo zao kumtazama Liz wangu, kiuno ndiyo kilizidi kuniacha hoi kwa wembamba wake na kujikuta nikimkufuru Muumba kwa kuwapendelea baadhi, nilijikuta nikiwa nimeduwaa mpaka sauti ya Liz iliponishtua kwani tayari kumbe alishaenda na kurudi, "vipi Erick unaonekana upo mbali sana" nilishtuka kisha nikajifanya kama vile nilikuwa nae, "nilikuwa nawaangalia hao vijana wanaocheza pool Liz" hakuwa na swali tena zaidi tuliendelea kujinywea lile chupa kubwa la Amarula, baada ya dakika kadhaa kupita nilimuita kijana wa chakula ambaye tulimuagiza kuku mzima wa kienyeji aliyechomwa na chipsi naye akafanya hivyo, tuliendelea kunywa huku huku tukizungumza hili na lile.Baada kama ya masaa mawili niliweza kuona mabadiliko kutoka kwa mgeni wangu Liz, muziki uliomvutia ulipopigwa aliimba naye kisha kidogo alisimama na kujitikisa kidogo kisha akaketi kitini, niliweza kufanya tathmini haraka kuwa Liz huyo hakuwa yule aliyekuja mwanzo bali huyo alikuwa Liz ubini wake ungekuwa Amarula nikiwa na maana kuwa tayari alishalewa, Liz alichangamka na kunizoea zaidi tofauti na hapo awali alipokuwa hajalewa "Erick leo naenda kulala kwako!" nilishtuka kwani nilijua ningetumia maneno mengi kumlaghai Liz kwenda kwangu, furaha na hamu ya kumrarua msichana huyo iliyateka mawazo yangu kwani tangu nizaliwe nilikuwa sijawahi kufanya tendo la ndoa tofauti na Allen ambaye tangia akiwa Sekondari alikuwa akibadili wasichana kama nguo, kuna wakati mpaka Baba yetu mlezi marehemu Andrew alikuwa akichukizwa na tabia ya Allen na kumuonya, kuna wakati nilihisi huenda marehemu hakuona sababu ya kumpatia zile mali Allen kutokana na vijitabia vyake.Majira ya saa nne kasoro usiku tayari mimi na Liz macho yalikuwa mazito na kujikuta tukianza kuchezeana hadharani jambo ambalo lilinifanya niogope mapaparazi wasije wakachukua picha zetu na kwenda kuwauzia wamiliki wa magazeti, nilimnyanyua Liz ambaye kichwa chake alikiegemeza katika bega langu la kulia kisha nikamuingiza ndani ya gari akiwa amelewa chakari, Niliendesha gari kwa kasi kupitia barabara ya Oestabay, baada ya lisaa limoja mlinzi alikuwa akitufungulia geti pale nyumbani, "hapa ni wapi Erick?" Liz aliongea kama mtu aliyeshtuka toka usingizini, nilipomueleza pale ni nyumbani kwangu alikataa kushuka garini na kudai nimrudishe hostel, nilihisi kuchanganyikiwa kwani tayari ilishatimu saa sita kasoro robo, kwa hekima na busara zangu niliingia tena garini nikiwa nimekunja uso kwa hasira kisha nikawasha gari, "Erick mpenzi umekasirika?" yalikuwa maneno ya Liz ambaye aliongea kilevilevi, nilimjibu kuwa sikukasirika hata kidogo japo mpenzi msomaji ungeniona ungeliafiki hilo, "Leo nimeamini kuwa kweli unanipenda zima gari" kwa mara nyingine Liz alikuwa akinitega, nilifanya kama alivyoniagiza.Nilimuona msichana huyo akijivuta kwenye zile siti mpaka akakaribia siti yangu, alinishika shavu langu na kugeuzia uso wangu kwake, nikiwa natazamana naye uso kwa uso nilimuona Liz akifumba macho kimahaba haswa huku akinisogezea kinywa chake, kwakuwa nilishatazama picha mbalimbali za kikubwa nilidaka kinywa chake ambacho kilikuwa na joto la aina yake na kuanza kudendeka, Liz alihema kimahaba huku mikono yake akiwa kaizungusha katika shingo yangu, nilipata raha ya ajabu kwani tangu nizaliwe nilikuwa mimi na kitabu, kitabu na mimi.Tayari jogoo wangu alishawika na kwa tukio hilo Liz kama vile alishtukia alihamisha mkono wake mmoja kisha akauteremsha mpaka pale alipokutana na kukigusa kitu kigumu kilichokuwa ndani ya suruali, alikipapasa kiutaalamu kisha taratibu alifungua lisani ya suruali yangu, wakati huo ndimi zetu zilikuwa zimegandana na kutufanya tujione kama tulikuwa dunia nyingine, kwa mbali nilihisi mropelo wangu ukiwa umekamatwa na mkono laini wenye joto la aina yake huku ukipikicha na kunifanya nijisikie raha ya ajabu, Ghafla Liz alijitoa kwenye kinywa changu nakuinamia ule mropelo wangu kisha taratibu aliutumbukiza kinywani, nilijikuta nikipata raha ya ajabu huku mikono yangu nikizichezea nywele laini za Liz, nilianza kugumia kwa raha hali iliyopelekea mimi kumuomba Liz tuingie ndani tukamalizie mchezo huo ndani.Nilipiga hatua haraka huku nikiwa nimekumbatiana na Liz, ishara ya pale ndani ilionyesha kuwa Allen hakulala humo kutokana na funguo kuzikuta mahali ambapo niliziacha mchana.Niliufunga mlango kwa ndani kisha moja kwa moja nilimkumbatia Liz kwa nguvu, hapo nilibadilika kabisa nilimsaula nguo zote na kumuacha kama alivyozaliwa kisha namimi nikavua nguo zote na kubaki mtupu, nilimbeba Liz juu juu mpaka kwenye sofa kisha nikamkalisha na kumchanua miguu, nilimuangalia dodo zake mbivu kisha nikaanza nazo, Liz alitoa miguno ambayo iliashiria alipata raha ya ajabu kupita kiasi, niliteremka mpaka kunako chumvi ambapo miguno ilibadilika na kuwa kilio sio cha maumivu la hasha ni cha raha ambazo alizipata nilipokuwa nanyonya kwa ustadi pale pahala ambapo panasababisha migogoro kadha wa kadha ulimwenguni.Mwisho nilimsikia Liz akiniomba nitumbukize mropelo wangu kwani alishazidiwa, niliinuka akiwa amechanua miguu vilevile nilisimama katikati yake kisha taratibu nikauweka mropelo wangu kunako joto, ilizama taratibu mpaka yote ikapotelea ndani, nilianza kuuzungusha mropelo wangu uliosimama na kukaza sawia, Liz alianza kulia taratibu lakini kadiri nilivyozungusha mropelo wangu alizidi kulia kwa sauti huku mimi nikizidi kutoa kichapo kikali, kama vile haitoshi Liz alinisukuma kisha akanigeuza mimi nikawa nimeketi kwenye kochi na yeye akawa kaukalia mti pori wangu, Liz alijua kutumia haswa kiuno chake huku mikono yake akiwa kazungusha shingoni kwangu, nilipata raha ya ajabu na kujikuta nikigumia kama beberu, Liz alijua kulilia kama vile alifundwa, nilikuwa tayari kwa lolote hata kama angesema nimpatie mali zangu zote.Baada ya dakika kadhaa Liz aliongeza kasi huku meno yake yakiwa kifuani kwangu,Mwanzo yale meno nilijua ananipapasa lakini alivyozidisha kasi nilijikuta niking'atwa bila kujitambua nilihisi raha badala ya maumivu, mwisho aliniomba nimpe nami nikafanya hivyo.Raha ilizidi nilipomfikisha kileleni na kujikuta wote tukiwa hoi bin taabani.Tulihamia chumbani huko nako mambo yaliendelea kwenye sita kwa sita, mimi juu Liz chini, ilikuwa mechi ya kufa mtu mpaka usingizi uliponichukua sikujitambua, nikiwa usingizini niliweza kumuote ndoto ambayo nilimuona mama yangu mzazi akiwa analia, kila nilipojaribu kumsogelea alirudi nyuma na kunikana mimi sio mwanae.Nilishtuliwa toka usingizini na mlio wa simu, mara baada ya kuamka niliweza kugundua simu hiyo alipiga Allen lakini baada yakuweka sikioni niliambiwa kuwa nilihitajika kituo cha Polis haraka, niligeuka kumtazama Liz msichana ambaye nilitokea kumpenda sana.Nilijiuliza mara mbilimbili kwanini niliitwa kituo cha Polis na aliyetumia simu ya Allen ni nan?
Mambo yanazidi kuwa matamu, Je nn hatma ya simulizi hii? Ungana nami toleo lijalo.
No comments:
Post a Comment