Friday, 20 January 2017
Mahubiri ya Mch. Chris Oyakhilome DSc, D.D
❤Rhapsodi Ya Uhakika❤
“Atakulinda”
Alhamisi, Januari 19.
*-… Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha (Danieli 3:16-18)._*
Kama Mkristo, kamwe usiwe na udhuru, kutishika, au kusita kuelezea imani yako kuhusu Kristo na ujumbe wa Injili. Hakuna jambo na wala usimruhusu mtu akuzuie au kukufanya ukae kimya kuhusu Yesu pamoja na ujumbe wa Injili. Yeye ni mkuu kuliko serekali yoyote ile, taasisi, au sekta iwayo yote. Anaongoza na kutawala juu ya ulimwengu wote, kila kitu mbinguni na hata katika serekali. Hakuna jina na wala hakuna uweza ulio juu ya mamlaka Yake (```Waefeso 1:21```).
Kwa hiyo, kataa kutishwa na sheria yeyote ile ambayo inakataza au kuzuia ukiri wa imani yako ndani ya Kristo, na kuhubiri kwa Injili. Jifunze kutoka kwa Shedraki, Meshaki na Abednego, ambao walitishwa na serikali ya wakati ule kwa waisujudie sanamu ya dhahabu ya mfalme au vinginevyo watupwe katika tanuru la moto. Walikataa kusujudu, wakichagua kuwa ni heri wafe, kuliko kuisujudia sanamu.
Hebu soma tena mstari wetu wa ufunguzi kuhusu kauli yao yenye kuvutia na kujitoa kwao kikamilifu kwa Bwana katika kujibu tamko la mfalme. Ilimkasirisha na kumpandisha gadhabu mfalme, ambaye aliamuru kwamba watupwe katika ziwa la moto. Ile tanuru ya moto ilikuwa ni kali sana kiasi kwamba uliwaunguza na kuwauwa wale watumwa wa mfalme waliowatupa kwenye tanuru Shedraki, Meshaki na Abednego. Ijapokuwa, Shedraki, Meshaki na Abednego hawakudhurika hata kidogo. Bwana aliwalinda. Pindi Nebukadreza alipotambua kuwa hawakudhurika kwa ile tanuru ya moto, alitubu; soma utii wake katika ```Danieli 3:28-29```.
Hicho ndicho kinachotokea pindi unaosimama kwa ujasiri katika imani, licha ya upinzani mkubwa na mgumu. Baada ya kitambo kidogo, wapinzani wako watavutiwa na imani yako thabiti, ambayo inaweza kuwaongoza katika wokovu wa roho zao. Hivyo, mtumikie Mungu kwa maisha yako. Kazi yako yaweza ondolewa kwako kwa kuhubiri Injili, lakini hawawezi kuondoa amani ya Bwana katika roho yako. Wanaweza wakakutelekeza kutoka katika kampuni yako, lakini hawawezi kuitelekeza roho yako.
Mungu ni muweza! Mwamini Yeye. Alimuokoa Shedraki, Meshaki na Abednego dhidi ya tanuru la moto; Alimtoa Danieli kutoka katika shimo la Simba; Alimuokoa Modekai dhidi ya ouvu wa Namani. Yeye ndiye anayesimama kwa ajili yako; Yeye ndiye apiganaye kwa ajili yako. Yeye ndiye akulindaye.
*Sala*
*Baba Mpendwa wa mbinguni, ninakushukuru kwa faraja ya Maandiko; nimetiwa nguvu na kuhuishwa kwa Roho Wako katika mtu wangu wa ndani [rohoni] kiasi kwamba pasipo kujali changamoto, ninashinda kwa kitukufu. Roho Mtakatifu anaishi ndani yangu, na Amenifanya mimi kuwa zaidi ya mshindi, katika Jina Lake Yesu. Amina.*
*Somo Zaidi:*
*```Danieli 6:27```*
Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.
*```Warumi 8:26-28```*
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
*```Danieli 3:28-29```*
Nebukadreza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe.
29 Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila ya watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lo lote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.
*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:*
Mathayo 13:24-43,
Mwanzo 44-45
*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:*
Mathayo 7:21-29,
Mwanzo 19:1-38
www.rhapsodyofrealities.org
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment