Matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook yanazidi kuongezeka ikiwa na watumiaji zaidi ya Bilioni 1.65 duniani kote, jambo linalofanya kuwepo na hatari ya usalama kwa waharifu wa mtandaoni “hackers” kuingilia akaunti za watu na kuangalia watu hao wanawasiliana nini na watu wao wa karibu ambao wanawasiliana kwa njia ya meseji.
Ili kulidhibiti hilo uongozi wa Facebook ulitoa taarifa kuwa umeanza kufanya majaribio ya mfumo wa secret message, mfumo ambao utawazuia watu wengine kuangalia mmiliki wa akaunti anachati kitu gani na watumaiji wenzake wa Facebook.
Mfumo huu utamwezesha mmiliki wa akaunti kuchagua kama anataka kuchati kwa siri “secret message” na baada ya hapo kifaa ambacho atakuwa ametumia kufanya marekebisho hayo ndiyo pekee kitaweza kusoma hizo meseji na kama atatumia kifaa kingine hataona hizo meseji.
“Mawasiliano ya siri yanaweza kusomwa na kifaa kimoja pekee na hakutakuwa na haki ya kifaa kingine kuona ujumbe huo,” ilisema taarifa ya Facebook.
No comments:
Post a Comment