Friday, 21 October 2016

Waziri Wa elimu aiagiza bodi ya mikopo kurejesha mfumo Wa zamani wa utoaji fedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu

Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kurejesha mfumo wa zamani wa kutoa fedha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Waziri wa Elimu ameyasema hayo leo usiku wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa TBC ambapo amekiri kuwepo kwa mapungufu katika namna ya fedha hizo zinavyotolewa hali inayopelekea wanafunzi kupata fedha kidogo ambazo hazikidhi mahitaji.



Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na sitofahamu kubwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu nchini baada ya wengi wao kukosa mikopo huku wengine wakipewa fedha kiasi kidogo ambazo hazitoshi kujikimu.

No comments:

Post a Comment