.
*LIFE BEGINS AT 40.... HOW OLD ARE YOU?*
Life Begins at 40..
Huo ni msemo wanao waingereza wakimaanisha maisha yako ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa au toka umefika duniani na toka umeanza kukua nk nk lakini bana maisha #halisi yataanza rasmi siku ukitimiza *miaka 40.*
Hapo kama bado nauli ya *daladala ni ishu, ada, chakula, kodi ya nyumba, nk* basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unatumia Facebook kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote.
Nadhani unanielewa sasa hasa wewe ambaye unahisi umri wako bado ni mdogo kwa hiyo bado bado kidogo muda wa kuwa serious na maisha haujafika.
Sikia kijana mwenzangu *TODAY* is your future kwa taarifa yako..
Ulipokuwa mdogo ulisema, nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. *Je unayo?* Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.
Kama haijatokea je bado *hujawa mkubwa?* Basi kama ni mkubwa ujue kuna *kitu hujafanya.*
*Utasema tena nikifika miaka 40* nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international school nk. Subiri uone miaka inavyoenda.
Usishangae kufika *40* bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini.
*Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!*
Hapo ndo unawaza kufuga *ng'ombe* wa maziwa Kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu *12 kwa 15!*
Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha *bizness in Australia.*
Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa *300M!* Wamejenga mjengo wa ukweli.
Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz *(Google that).*
Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full *kutukanwa na makondakta.*
Wenzako in their *40s* wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini mzazi anahitaji support kidogo *una-mute!*
Wenzako in their *40s* wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia *5M* kimyakimya.. Wewe ukitoa *laki moja* basi mpaka mtaa wa saba watajua! Halafu unashangaa wenzako wanazidi kuinuliwa. Unaanza kuwaita *Freemason.* Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... *(Malizia)*.
Wakati wenzako walikuwa wanajenga maisha wewe ulikuwa unashinda Facebook kuongelea UKUTA uwepo au usiwepo.. Sijui kuvunja viti uwanja wa taifa. Harmonize anajua kuimba au hajui. Wema Sepetu atafute mtoto au aache tu. *Can you imagine?*
Wenzako mkifika miaka 40 watu wa rika lako wana exposure ya uhakika. Wewe at 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe chakula hata virutubisho hakina. Wenzako at 40 washaacha ajira siku nyingi washatembea dunia na kujifunza maisha kutoka kila mahali. Walishafika kuanzia *Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!!*
Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku *Tegeta Posta* ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! *Unaishi* au *unaisha?*
Acha mawazo mgando. *Eti mi nina mshahara mzuri.* Mshahara mzuri? Kweli?
*Sikia, hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu.*
Jiandae kusimama mwenyewe.
*Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini?* Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. *Don't be afraid*. Don't dwell in that comfort zone!! *Unasubiri kiinua mgongo?*
*Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi.*
*Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa.*
Kwa nini hukufungua ukiwa *30yrs* ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect. Kisa ulikuwa unafatilia ratiba zote za mechi za mpira na matamasha na mikutano yote ya kisiasa ukasahau muda unaenda. Hao unaowafatilia wako ndani ya kazi zao kwa hiyo muda wao unatumikia shughuli zao wakati wewe utatumia muda wako na pesa yako kwenda kuangalia nk.
*Jenga nidhamu mpya ya kulinda muda wako sasa.*
*Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET.*
Halafu ukianza kuregret ndo *pressure zinakuja, stress,* nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime. Kisa? Ulikuwa unatumia muda wote kuangalia vitu vya kuchekesha chekesha na kuongelea mambo ya siasa sijui wasanii sijui msanii gani ana hela nyingi sijui nani kafulia sijui nani ana mimba.. Seriously? Sijui nani hajapendeza kunyoa bora asuke😡😠😠. Hivi vitu vinaiba muda wako sana ndugu zangu. Mimi mwenyewe nilikuwa hivyo lakini nikastuka mapema sana! Utashangaa umri unaenda bila kupiga hatua. Umri wako ni kila sekunde na kila dakika na kila saa. Ndo umri huo. Umri siyo mwaka kwa mwaka. Ni sekunde na dakika. Ndo maana matajiri wanalinda muda wao kwa wivu mkali. Coz TIME IS MONEY. Utashangaa unapoteza muda afu unafika 40 years ndo unawaza uanzie wapi. Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Hajakupa uuchezee chezee tu. Be careful. Time flies.
*Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?* So kama wewe unasema "Mimi bado mdogo.." endelea tu kupoteza muda wako utakumbuka tu siku moja but it might be too late. Endelea tu kupoteza muda na skendo za wasanii. Au unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake. Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira. Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established. Bila hivyo utashangaa kweli. Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa *sh Bilioni mbili kwa ajili ya kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja? Wakati huo wewe unamiliki kigari cha mkopo unakipaki uwanja wa CCM unalipia sh 1000/- tu, *mnaita buku*. Fikiria vitu kama hivi. Utajua vizuri umuhimu wa kutumia muda wako vizuri. Ilikuwa *January* sasa *October* hii. Mwaka unayoyoma. Wewe mwaka huu nini kipya hasa umefanya kimaendeleo. Kupost kuhusu *Lipumba*? Au *Scorpion?*
*Life begins at 40 my friend.... How Old are you now?*
You can change your life even now!
*TUBADILIKE*
Copy n paste
Share................
No comments:
Post a Comment