TOFAUTI YA "JK" NA "JPM" KWENYE MIKOPO ELIMU YA JUU.
By Malisa GJ,
JK aliweka madaraja kwenye ada tu (tuition fee) lakini kwenye mambo mengine akaweka usawa. Kwa hiyo mtu mwenye mkopo 100% na mwenye mkopo 10% wote walikua wakipewa privilege sawa kwenye mambo mengine.
Kwa mfano fedha za kujikimu (M&A) wote walipewa 8,500/= kwa siku. JK aliamini kwamba mwenye asilimia kubwa za kupata mkopo na mwenye asilimia ndogo, wote wanastahili kula, wote wanastahili malazi bora, wote wanastahili pesa za vitabu na machapisho etc.
Na watoto wengi wa maskini walikua wakitumia fedha zao za kujikimu kulipia ada. Unakuta ada ni 2M halafu bodi ya mikopo imekupa 50% means inakulipia just 1M, the rest 1M unapaswa ulipe mwenyewe. Ukiangalia hali ya familia yenu ni duni. Pengine ni yatima na una wadogo zako wanakutegemea. So inabidi ujibane kwenye hela yako ya kujikimu (8,500/= per day) ili uweze kulipa sehemu ya ada iliyobaki. Watoto wengi wa maskini wamesoma kwa mtindo huo hadi wakamaliza.
JPM yeye ameweka madaraja kwenye kila kitu, kuanzia tuition fee hadi fedha za kujikimu na mambo mengine. Yani ukipata mkopo 10% means unapewa 10% kwenye kila kitu. Kuanzia ada, pesa za kujikimu, stationeries, mafunzo kwa vitendo etc.Angalia tofauti kati ya jedwali la kwanza (wakati wa JK) na jedwali la pili (wakati wa JPM).
Wakati wa JK utaona mwanafunzi amepewa 50% ya ada ambayo ni sawa na 721,000/=, na wakati wa JPM utaona kuna mwanafunzi kapewa ada 25,412/= hata haijulikani ni asilimia ngapi. Mwanafunzi wa chuo kikuu anapewa tuition fee elfu 20?? Maajabu.
Wakati wa JK utaona fedha za kujikimu mwanafunzi kapewa 1,852,000/= kwa mwaka ambayo ni sawa na Tzs 8,500/= kwa siku, lakini wakati wa JPM kuna mwanafunzi kapewa 45,150/= ambayo ni sawa na TZS 376/= kwa siku (Shilingi mia tatu sabini na sita). Duuh.!
Wakati wa JK gharama za stationeries wanafunzi wote walipewa 200,000/= bila kujalisha viwango vyao vya mikopo, but wakati wa JPM kuna wanafunzi wamepewa stationeries 4,024/= kwa mwaka. Hivi elfu 4 unanunua kitabu gani? Hiyohiyo utolee photocopy na kufanya printing. Maajabu.!
Wakati wa JK pesa ya mafunzo kwa vitendo ilitolewa TZS 620,000/= kwa mwaka, lakini wakati wa JPM kuna wanafunzi wamepewa 6,307/= kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Hivi ni mafunzo gani kwa vitendo yanafanywa kwa buku 6?? Labda mafunzo ya kupika vitumbua.
Najaribu kutafakari wale wanafunzi waliokua wakitumia sehemu ya pesa zao za kujikimu kujilipia ada, sasa hivi watafanyaje? Una mkopo 10%, ada ya chuo chako ni 1.5M, bodi inakulipia 150,000/= wewe unatakiwa uchangie 1350,000/=. Ukiangalia familia yako ni duni. Baba yako hajawahi kumiliki laki 5 tangu umfahamu. Kwahiyo suala la yeye kukulipia 1.35M kukamilisha ada ni ndoto kwake.
Unajipa moyo ngoja tu ukaripoti chuoni maana utajibana kwenye fedha za kujikimu ujilipie sehemu ya ada iliyobaki. Kufika chuoni unakuta umepewa mgao wa TZS 45,150/= kwa mwaka sawa na TZS 376/= kwa siku. Unajiuliza kalamu ya Obama inauzwa 400/= inakuaje upewe 376/= kujikimu?? Unaanza kuhisi labda ni dola 376 (USD), lakini unaambiwa ni shilingi.
Hapo lazima ubebe mabegi urudi nyumbani. Ndio maana sikuwashangaa wale wanafunzi wa Mkwawa walioripoti chuoni juzi then kesho yake wakafungasha virago na kuondoka. Ni kwa sababu kama hizi.
Nashauri JPM atafakari upya suala la mikopo ya elimu ya juu kwa watoto maskini wa Tanzania. Hivi anawezaje kumpa mtu 376/= kwa siku eti fedha ya kujikimu?? This is joke. Naamni hata yeye hakupewa 376/= kwa siku enzi zake akisoma.
Kama kila mwezi TRA wanajisifu kuvuka malengo ya makusanyo, sioni sababu ya wanafunzi wa elimu ya juu kunyanyasika. Wote wenye sifa wapewe mikopo, tena kwa viwango vya kutosheleza majitaji yao. Hivi ndivyo ulivyoahidi wakati wa kampeni zako. Kazi yetu (opposition) ni kukukumbusha utimize ahadi yako, na ni muhimu utimize bila watendaji wako kuleta ujanja ujanja wa aina yoyote.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.!
Malisa GJ
No comments:
Post a Comment