Saturday, 22 October 2016

Serikali yatangaza kuwa ajira hadi mwezi wa Pili 2017

Waziri wa utumishi wa umma na utawala bora angella kairuki amesema serikali itaanza kutoa ajira mwakani mwezi wa pili 2017 na kupandisha madaraja vyeo na kulipa stahiki mbalimbali za watumishi wa umma. Kairuki ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi jijini dar es salaam amesema kuwa mda huu serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na kubadilisha miundo ya utumishi wa umma pamoja na kupitia upya mishahara ya watumishi sekta binafsi kwa miezi iliyobaki mwaka huu.

Kairuki ameongea hayo akiwa anaulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu Serikali itaajiri lini amewataka watanzania kuwa wavumilivu pindi zoezi la uhakiki linafanyiwa tathimini kwa mapana.

No comments:

Post a Comment