Friday, 8 May 2020

BREAKING NEWS UTUMISHI WAMWAGA NAFASI KIBAO ZA AJIRA KWA WATANZANIA*


🇹🇿 *Wanahitajika wafuatao*

▪️Ma Afisa Kilimo
▪️Ma Afisa UTUMISHI
▪️ICT Officers
▪️Wahudumu wa Afya
▪️Wahudumu wa Mochwari
▪️Washauri na Saha
▪️Watunza kumbukumbu
▪️Tutors
▪️Madaktari wa Meno
▪️Telephone operators
▪️Mafundi Bomba
▪️Wahasibu
▪️Ma Afisa Misitu
▪️Ma Afisa wanyamapori
▪️Ma Afisa uvuvi
▪️Ma Afisa Nyuki
▪️Ma Afisa Utalii
▪️Wataalamu wa maabara
▪️Ma Afisa Takwimu
▪️Mafundi Magari
▪️Ma Afisa habari
▪️Ma Engineer
▪️Insurance officers
▪️Watendaji wa Vijiji
▪️Na Nyinginezo

🇹🇿 *Maombi yote yanatumwa online kwa mfumo wa Ajiraportal*

👁️ *Deadline 21 May 2020 Bofya link hii hapa Kuanza kutuma Maombi kwa Ajiraportal*👉👉👉👉👉👉https://t.co/qIFrbBULYk?amp=1



*Usiwe Mchoyo Share Nafasi Hizi za Kazi Kwa watanzania wanaotafuta kazi*

*Sharing is caring*

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

Monday, 5 February 2018

WATUMISHI WASIYOIUNGA MKONO CCM KUFUKUZWA KAZI


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amefunguka na kuwataka watumishi mbalimbali mkoani kwake ambao hawaiungi mkono Serikali ya awamu ya tano iliyopo chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuondoka mapema katika nafasi zao hizo.
Mnyeti amesema kuwa siku zote Chama Cha Mapinduzi ndiyo kimekuwa kikihangaika kuomba kura majukwaani huku viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwa si wanufaika wakubwa kulinganisha na watumishi, hivyo watumishi wanapaswa kutambua na kuiunga mkono Serikali ya CCM na kama hataki waondoke kwenye nafasi hizo. 

"Wanaoumia kuomba kura majukwaani ni CCM anayekuja kula ugali na familia yake ni wewe mtumishi, unanufaika wewe na familia yako. Sasa tumejipanga vizuri wale wote ambao siyo wenzetu watupishe mapema kabla ya uchaguzi, mimi ndiyo Mkuu wa Mkoa huu wa Manyara nasema hivi kama wewe huungi mkono Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ondoka mapema" alisisitiza Mnyeti

Sunday, 4 February 2018

Agizo elimu bure wananchi waelimishwe zaidi

Dar/Mikoani. Wakati suala la chakula likionekana kuwa tatizo kubwa katika utekelezaji wa agizo la kufuta michango, wazazi 123 mjini Tabora wamegawana fedha walizokuwa wamechangia kwa ajili ya huduma za shule na wanafunzi.
Utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, ni moja kati ya mambo yaliyo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na Rais John Magufuli ameanza kuitekeleza kwa kupiga marufuku michango ya aina yoyote shuleni.
Kama haitoshi, Rais alirudia agizo lake Januari 17 alipotoa onyo kuwa endapo atasikia tena wazazi wakilalamikia michango, mkurugenzi wa wilaya husika ajifute kazi.
Serikali inatoa Sh23.8bilioni kila mwezi kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa elimu bila malipo, lakini utekelezaji wa agizo hilo unakosolewa kutokana na umuhimu wa chakula kwa shule za kutwa, hasa kutokana na ukweli kuwa baadhi ya wanafunzi wanaishi mbali na shule
Uzoefu unaonyesha katika shule za nje ya miji, wanafunzi hutakiwa kufika saa 1:30 asubuhi ili kuanza masomo saa 2:00 asubuhi na hupumzika mchana kwa ajili ya chakula, lakini sasa inabidi vipindi viishe saa 8:30 mchana.
“Dhamira ya Rais ni njema, lakini fedha inayopelekwa haiwezi kutosheleza mahitaji yote,” alisema aliyekuwa ofisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.
“Kwa mfano nakumbuka kuna shule moja pale Buguruni ilikuwa na wanafunzi 124 na ilipokea Sh67,000 tu ambazo hazikutosheleza. Suala la ulinzi, umeme na chakula ni changamoto katika shule nyingi.
“Serikali ikiunganisha huduma hizo kwa kuongeza bajeti, michango haitakuwa na ulazima.”
Changamoto ni chakula
Alisema athari zinazoweza kujitokeza endapo michango yote itafutwa ni pamoja na wanafunzi wengi kutofanya vizuri katika masomo yao kutokana na ukosefu wa chakula.
Maoni kama hayo yalitolewa na Profesa Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye alielezea umuhimu wa walimu kushiriki kikamilifu katika elimu ya watoto wao, kama kutoa michango ya msingi ya chakula, maji, ulinzi hata ujenzi wa miundombinu.
Profesa Bana alisema wazazi wakisitisha kuchanga kwa sababu ya agizo la elimu bila malipo, kunaweza kukawa na madhara kwa sababu ni ukweli usiopingika kwamba afya ya mwili huenda sambamba na afya nzuri ya mwili.
“Kwa uzoefu wangu wa kufundisha shule za msingi, lazima elimu iwe shirikishi kwa maana ya wazazi kuchangia ni vigumu kumuelewesha mtoto aliye na njaa,” alisema Profesa Bana.
“Wanaomshauri Rais Magufuli waangalie masuala ya msingi yanayoweza kuchangiwa na wazazi, hasa chakula shuleni.”
Alisema msingi wa elimu ya kujitegemea lazima uende sambamba na jamii husika kuchangia elimu bila wasiwasi.
“Kama walimu wanahofiwa kupokea michango, kamati za shule ziunde kamati ndogo za kupokea michango ili huduma muhimu kwa watoto ziendelee. Huwezi kuacha watoto na njaa wakati wazazi walikuwa wanachangia na wana uwezo huo,” alisisitiza.
Mtaalamu mwingine aliyezungumzia suala hilo ni mratibu wa Mradi wa Mtoto Mwerevu kutoka Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Ruth Maziku aliyesema ipo hatari ya kushuka kwa kiwango cha elimu iwapo wanafunzi hawatapata chakula.
Alisema katika umri wa miaka mitano hadi 14 ambao mwanafunzi anatarajia awe kati ya darasa la kwanza na la saba, chakula ndio msingi mkubwa wa kukuza ufaulu.
“Kwa umri huo anapaswa kula milo mitano, mitatu ikiwa mikubwa na miwili midogo. Chakula kinasaidia ubongo kufanya kazi yake ipasavyo na kuongeza uelewa kwenye masomo,” alisema.
Mtaalamu huyo alisema ukosefu wa chakula unaweza kuongeza utoro kwa wanafunzi wanaoishi mbali na shule.
“Kwa hiyo wataalamu wa lishe tunasisitiza watoto kupata chakula cha mchana shuleni,” alisema.
Viongozi wa mikoa, wilaya wanena
Mkoani Iringa, mkuu wa mkoa, Amina Masenza alisema Serikali haijapiga marufuku michango ya wazazi kwa ajili ya maendeleo ya shule, bali inayokusanywa na walimu.
Masenza alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata za Nyanzwa na Ibumu Wilaya ya Kilolo.
“Ni marufuku michango yote inayotolewa na wanafunzi kwa walimu. Mwalimu atakayebainika kuhusika na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Wanafunzi wanatakiwa kupokewa shuleni na kuendelea na masomo bila ya kusumbuliwa,” alisema Masenza.
“Kama wananchi mtakaa wenyewe na kukubaliana kuwa mnachanga kwa ajili ya maendeleo ya shule zenu bila ya kuhusisha mwalimu katika michango hiyo, hapo mnaruhusiwa. Hata waraka wa elimu bila malipo unasema hivyo.”
Masenza alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa maswali na baadhi ya wakazi wa Kata ya Ibumu waliotaka kujua aina ya michango iliyopigwa marufuku na ile inayoruhusiwa.
Katika majibu yake, alisema michango inayoibuliwa na jamii haina budi kusimamiwa na jamii husika bila kuwahusisha walimu, kuanzia ukusanyaji wa michango hadi matumizi yake.
Kuhusu malipo ya walinzi, mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli alisema suala la ulinzi wa shule, halmashauri yake inalipa mishahara yao katika shule zote za wilaya hiyo.
“Kuhusu usafi huo ni wajibu wa wanafunzi, na chakula tunatoa kwa wanafunzi wa bweni tu, chakula cha nini kwa mwanafunzi wa kutwa,” alihoji.
Naye katibu tawala wa Wilaya ya Kilombero, Robert Selasela alisema utaratibu wa michango ya ulinzi na chakula vinatekelezwa katika serikali ya kijiji.
Kuhusu mwongozo wa elimu bila malipo, Selasela alisema licha ya maelekezo ya fedha kujikita katika vifaa vya ufundishaji, ukarabati wa shule, huduma za kiutawala na mengineyo, bado wanavijiji wameamua kuchangia mahitaji ya chakula bila kushirikisha uongozi wa shule.
“Shule ni mali ya serikali ya kijiji. Rais anatukumbusha tu, ruzuku tuliyopata hadi Novemba mwaka jana ilikuwa ni Sh285.9 milioni, sawa na asilimia 73 ya Sh440 milioni. Bajeti ni Sh20,000 kwa kila mwanafunzi,” alisema.
“Kuhusu michango ya chakula ni wanakijiji wanakusanya chakula, si pesa na wanatumia kamati zao na kupika wenyewe.”
Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Zuwena Omary alisema licha ya michango kupigwa marufuku, jamii inapaswa kutambua majukumu ya wazazi na Serikali katika suala la elimu bure.
Alisema suala la wazazi na walezi kuchangia shule za msingi na sekondari za kata ambazo wanafunzi wanaishi kwenye hosteli halikwepeki.
Wazazi walivyogawana michango
Mkoani Tabora wazazi 123 wa watoto wanaosoma Shule ya Msingi Ipuli , wamegawana fedha taslimu na vyakula walivyonunua kwa ajili ya mlo wa mchana, ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais la kuzuia michango shuleni.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya wazazi wa shule hiyo, Samson Gabriel alisema uamuzi wa kuwarejeshea wazazi hao michango hiyo ya chakula na fedha ni utekelezaji wa agizo la Rais na maelekezo ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Mariam Hamis wazazi hao walichanga Sh676,000 mpaka kufikia Januari 17 na Sh272,000 zilikuwa zimetumika kununua mahindi na mchele.
“Baada ya agizo la Serikali, wazazi wameamua kugawana Sh404,000 zilizosalia pamoja na chakula kilichokuwa kimenunuliwa ambacho ni mahindi na mchele,” alisema Mariam.
Mmoja wa wazazi walioshiriki kugawana fedha na vyakula hivyo, Perpetua Kamiliwe , ambaye alikuwa ameshika kiroba cha mchele, alisema mambo yalikuwa mazuri.
“Nimechukua mchele wenye thamani ya pesa niliyochangia. Sioni kama kuna jambo limeharibika,” alisema.
Mzazi mwingine, Ibrahim Zuberi aliliambia Mwananchi kuwa licha ya kugawana chakula hicho, wanaishukuru Serikali kwa kupiga marufuku michango katika shule za umma, kwa maelezo kuwa umewapunguzia wazazi gharama na ugumu wa maisha.
“Michango hii imekuwa kero na mzigo kwa wazazi tunamshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa busara. Hakika huyu ndiye kiongozi anayewajali wanyonge,” alisema.
“Michango ilikuwa ya viwango tofauti kati ya Sh6,000 hadi Sh10,000 kwa kila mwanafunzi.”
Hata hivyo, mmoja wanafunzi wa shule hiyo, Salome Yohana alisema uamuzi wa wazazi kutochangishana fedha kwa ajili ya chakula, utawaathiri katika masomo.
Imeandikwa na Robert Kakwesi (Tabora), Geofrey Nyang’oro (Iringa), Kelvin Matandiko na Tumaini Msowoya (Dar)     

Tuesday, 30 January 2018

Breaking news:MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017/2018 YAMETOKA


BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), latangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017, ambapo ufaulu umepanda kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu.
Orodha ya Shule 10 Bora.
1. St. Francis Girls – Mbeya
2. Feza Boys – Dar es Salaam
3. Kemoboya – Kagera
4. Bethel Sabs Girls – Iringa
5. Anwarite Girls – Kilimanjaro
6. Marian Girls – Pwani
7. Canossa – Dar
8. Feza Girls – Dar
9. Marian Boys – Pwani
10. Shamsiye Boys – Dar
Shule Kumi (10) Za Mwisho Kitaifa
1. Kusini – Kusini Unguja
2. Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja
3. Mwenge SMZ – Mjini Magharibi
4. Langoni – Mjini Magharibi
5. Furaha – Dar
6. Mbesa – Ruvuma
7. Kabugaro – Kagera
8. Chokocho- Kusini Pemba
9. Nyeburu – Dar
10. Mtule – Kusini Unguja
KUANGALIA MATOKEO YOTE BONYEZA LINK HAPA CHINI

Link 1: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017

Link 1: MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2017

Link 2: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2017

Link 2: MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2017

           AU 
INGIA www.necta.go.tz/results/form four2017

Tuesday, 23 January 2018

SERIKALU YA TANZANIA YAAHIDI KUANZA KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI BAADA YA KUMALIZA UHAKIKI 2018


Serikali ya Tanzania imeahidi kuanza kuboresha maslahi ya watumishi ya walimu ikiwemo mishahara yao kipindi hiki kutokana na kumaliza zoezi la muda mfupi la uhakiki wa wafanyakazi hewa katika sehemu mbalimbali za ajira.
Hayo yamewekwa wazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe George Joseph kakunda leo (Jumatano) katika mkutano wa 10 kikao cha saba cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa alipotaka kujua ni lini serikali itawapandishia mishahara walimu.
"Utaratibu huu ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kifupi cha miaka kama miwili hivi kupisha uhakiki wa watumishi ambapo ni zoezi lililofanywa kwa umahiri na ueledi mkubwa, baada ya kuwa tumelikamilisha sasa tutaingia kwenye awamu ambayo ni ya kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara yao", amesema Mhe Kakunda.
Kwa upande mwingine, Mhe kakunda amewatoa hofu walimu wote ambao hawakupandishwa madaraja yao kutokea mwaka 2016 hadi 2017 na kudai katika mwaka huu wa fedha wameshafanya matayarisho wa kupandisha madaraja hayo. Serikali yatangaza kuboresha viwango vya mishahara kwa watumishi.
  

Sunday, 14 January 2018

UVIMBE KATIKA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAUME (SCROTAL MASSES)


Na Archandramu Mbungu.

Uvimbe katika sehemu za siri za mwanaume unaweza kusababishwa na matatizo mengi, mfano maambukizi katika kiwanda cha kuzalishia mbegu za kiume, Ngiri au Hernia, kuvimba kwa mishipa ya damu, kujaa maji au busha, kuvimba kwa mirija ya mbegu za kiume, saratani ya korodani, maambukizi sugu ya korodani, kujinyonga kwa korodani na matatizo mengine.
JINSI MATATIZO HAYA YANAVYOTOKEA
Maambukizi katika vifuko vya kutunzia mbegu au kiwanda cha mbegu na maambukizi sugu ya njia ya mkojo au maambukizi ya tezi dume hasa endapo mwanaume atakuwa ameshawahi kuumwa ugonjwa wa kisonono au gono ambao dalili zake ni kutokwa na usaha katika njia ya mkojo.
Wengine hupatwa na tatizo hili baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume au endapo mgonjwa atakuwa aliwekewa mrija wa mkojo kwa muda mrefu. Ugonjwa wa kifua kikuu pia huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Tatizo huanza ghafla, huambatana na homa na kutetemeka na maumivu makali ya korodani, ukipapasa kwa ndani ya korodani utagusa vivimbe kama goroli kwa ndani zaidi juu ya korodani. Ugonjwa unaweza tu kutulia baada ya kuanza matibabu lakini madhara yake ni kuziba kwa njia ya kupitishia mbegu hivyo kukufanya uwe mgumba.
Maambukizi ya korodani yote huwa makali na huanza ghafla au kwa kipindi kifupi, hutokea zaidi katika kipindi cha ujana na husababishwa na maambukizi mengine yoyote ya korodani. Mgonjwa hulalamika homa kwa vipindi, maumivu ya korodani na kuvimba upande ambao una maumivu.
Hali hii ikiendelea bila jitihada za haraka kuchukuliwa, korodani hiyo husinyaa na kupotea kabisa na kukufanya uwe na korodani moja, endapo tatizo litakuwa kwenye pande zote mbili, basi korodani zote mbili zinaweza kusinyaa na kupotea na kujikuta huna korodani.
Endapo korodani itajinyonga basi itakufa kwa kutokuwepo na mzunguko wa damu wa kutosha na tiba yake ni upasuaji na kuiondoa.
Mwanaume ambaye ana korodani moja, ni vema akapime mbegu za uzazi kuona kama zipo za kutosha na yule ambaye hana kabisa korodani, uwezekano wa kuzaa haupo. Saratani ya korodani huzalisha uvimbe ambao ni mgumu kwenye korodani na hauna maumivu. Kwa hiyo, endapo una uvimbe mgumu kwenye korodani na hauna maumivu, ni vema uondolewe kwa upasuaji.
Ugonjwa wa ngiri au hernia hutokana na uwepo wa uwazi toka juu tumboni hadi ndani ya mfuko wa korodani. Njia hii huwa inakuwepo unapozaliwa na kuziba taratibu kutokana na kuendelea kwa misuli.
Kama njia ya ngiri itaendelea, husababisha matumbo kuingia humo na kujaa kwenye mfuko wa korodani. Ugonjwa huu wa ngiri ni tofauti na busha. Busha ni hali ya kujaa maji katika mfuko wa korodani na husababishwa na maambukizo ya vimelea viitwavyo filaria na huenezwa na mbu.
Ugonjwa wa ngiri pia huwatokea watoto, vijana na watu wazima. Ugonjwa wa busha na ngiri hutibika kwa upasuaji. Kinga ya mabusha ni matumizi ya dawa za kinga ya mabusha na matende ambayo kila mwaka hutolewa bure na serikali kwa wananchi wote, huwa kunakuwa na kampeni maalumu.
Ugonjwa wa ngiri hutokana na kasoro katika njia zake, ili kuepuka ni kutofanya kazi ngumu kama utagundulika una tatizo hilo.
USHAURI
Matatizo haya ya korodani husababisha matatizo makubwa ya uzazi kwa mwanaume kwa hiyo ni vizuri kuwahi hospitali kama una matatizo sehemu hiyo, usipuuze hata maumivu kidogo kwani athari zake ni kubwa.
Matatizo au maambukizi katika njia ya mkojo pia ni shida kubwa kwa mwanaume. Epuka kuumia korodani, joto kali kwenye korodani, uvutaji wa sigara, bangi na matumizi mengine ya madawa ya kulevya.
Epuka ngono zembe, vyote hivi huhatarisha afya yako ya uzazi.

Kwa mawasiliano zaidi.
Piga namba 0766245554 au 0658245554
Email:mbunguarchandramu@gmail.com

Saturday, 13 January 2018

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA MJADALA JUU YA KUONGEZWA KWA MUDA WA URAIS

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokutana na Katibu mwenezi wa CCM ndugu Polepole. Zaidi soma taarifa hii kutoka ikulu

Friday, 5 January 2018

WAZIR MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA UPANDAJI MIKOROSHO BORA NA MIPYA MILIONI 10 MKOANI LINDI




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mh Godfrey Zambi alipokuwa akimueleza jambo wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji mikorosho Bora na mipya Million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza Maelezo toka kwa Afisa Ubanguaji Toka Bodi ya Korosho Tanzania CBT Domina Mkangara wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Upandaji mikorosho Bora na mipya Million10 iliyofanyika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

SERIKALI YAMJIBU TUNDU LISSU


NA ARCHANDRAMU MBUNGU.
Serikali imesema haioni sababu ya kuendelea kulumbana na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye, anapata matibabu jijini Nairobi baada ya kushambuliwa kwa risasi Mjini Dodoma takribani miezi minne iliyopita.
Msemaji Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan, Abbas, ametoa kauli hiyo kufuatia Mh. Lissu kuituhumu serikali juu ya kushambuliwa kwake na kumsababishia majeraha makubwa mwilinini mwake. 
Dk. Abbas kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema, Mbunge huyo bado ni mgonjwa na kwamba Serikali inaendelea kumuombea Tundu Lissu ili apone haraka.
"Mhe Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa. Tunaendelea kumuombea apone haraka" ilisema taarifa ya Dkt. Abbas 
Tundu Lissu leo Januari 5, 2018 ametoa malalamiko yako na kusema kuwa kitendo cha yeye kupigwa risasi kuwa ni mipango iliyokuwa inalenga kumzimisha kabisaa ili asiendelee kuwasumbua 

Friday, 22 December 2017

Breaking News: LEO SERIKALI IMETANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU ZAIDI YA 3000


Leo December 22, 2017 Waziri wa Nchi ofisi ya Rais – TAMISEMI Seleman Jafo ametangaza ajira mpya kwa walimu ili kuziba nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi na walimu katika shule za Msingi na Sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi.
Akiongea na waandishi wa habari Jafo amesema baada ya uhakiki wa maombi yalitumwa, jumla 3,033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi, kati yao walimu 266 ni wa sekondari na 2,767 ni wa shule za Msingi.
Walimu watatakiwa kuripoti katika ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa na kisha kwenda kuripoti katika shule walizopangiwa, walimu wanatakiwa kuripoti December 27, 2017 hadi January 17, 2018 wakiwa na vyeti vyao,” – Jafo

Thursday, 14 December 2017

*YALIYOJIRI WAKATI RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ANAFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) MKOANI DODOMA.*


*Dkt. John Pombe Magufuli-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.*

#Mimi ni mwalimu, sijabadilika, shida na raha za ualimu nazifahamu.

#Sisi vongozi ndani ya serikali hatuwezi tukawaangusha, walimu ni jeshi kubwa.

#Nashukuru Viongozi wa Chama cha Walimu kwa uamuzi wa kuufanyia Mkutano huu Mkoani Dodoma.

#Nitaendelea kuwa mtumishi wa watanzania wote,sitawabagua kwa Dini wala Vyama

#Sekta ya Elimu ni Nyeti na muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote.

#Natoa pongezi kwa viongozi watangulizi wataifa hili kwa jitihada walizofanya katika kuiendeleza sekta ya elimu.

#Natoa pongezi kwa walimu kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuwaelimisha watanzania.

# Tumeongeza Fedha za elimu bure kutoka Tzs 18.77 Bil. Hadi kufikia Tzs Bil. 23.868 kwa mwezi na mpaka sasa tumetumia Tzs Bil. 535.

# Serikali ya Awamu Tano imejenga na kurabati shule za Msingi na Sekondari 365 mpaka sasa.

#Mwaka huu tumegawa vifaa vya maabara katika Shule za Msingi za sekondari 1696.

#Walimu wanapomaliza masomo wafanye kazi kwenye vituo wanavyopangiwa.

#Walimu wanaopewa Posho za Madaraka wazitumie vizuri, na wanaotoa madaraka watoe bila upendeleo kwa walimu wanaojituma kwa ajili ya watanzania.

#Serikali imelipa Tzs Bil. 56.92 kwa ajili ya kulipa madeni ya walimu.

#Haya Madeni ya walimu tutayalipa yote, mara baada ya kazi ya uhakiki wale wote walioomba madai halali watalipwa.

#Viongozi niliowateua akiwemo Makamu wa Rais ni watetezi wakubwa wa walimu.

#Tumeongeza bajeti katika sekta ya afya kutoka Tsz bil. 31 hadi Tzs Bil. 239.

#Mnapokaa katika vikao vyenu kumbukeni kuuliza madai ya fedha zenu ikiwemo kutoka Benki ya Walimu.

#Serikali inapaswa kuhakikisha kile kinachopatikana kinapelekwa katika sekta zote, kile kinacholetwa kwenu na serikali naomba mkipokee.

#Udahili wa wanafunzi umeongenzeka kutoka Mil. 1 hadi Mil. Moja na Laki 9 kutokana na elimu bure na kwa sekondari udahili umeongezeka kwa asilimia 31.

#Serikali imetoa ajira 3462 kwa walimu wa sayansi na niwaahidi walimu, wanafunzi ajira zipo.

#Mamlaka husika angalieni kwa makini suala la mgawanyo wa walimu Mijini na Vijijini, lakini isiwe mwanya wa kuhamisha bila kufuata utaratibu.

#Usihame kama hujalipwa pesa yako, hakuna atakayekufukuza kazi kama hajakulipa pesa ya uhamisho.

#Tumekuwa na hifadhi za Jamii nyingi zisizofuata taratibu za hifadhi za jamii, ndio maana tunataka tuwe nazo mbili, moja ya Serikali nyingine ya sekta binafsi.

#Tunataka tuwe na hifadhi za jamii zinazojali watu wake na zitakazojenga viwanda.

#Tunaziunganisha Hifadhi za sekta za jamii kwa lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

#Natambua umuhimu wa posho ya kufundishia kwa walimu ili kuwapa motisha walimu

#Uchumi wa nchi yetu upo vizuri na ndio maana ipo miradi tunayoitekeleza kwa fedha zetu.

#Serikali inafahamu umuhimu wa kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwaongezea uwezo.

#Katika uchaguzi wenu, msichague watu kwa maslahi yao wala kwa rushwa, viongozi watakaowapeleka mbele na kwa ajili ya maslahi ya walimu.

#Vyombo vya dola vinavyohusika na rushwa vinafanya kazi.

#Viongozi mliopo chambueni madai ya walimu katika mikoa yote na mkiridhika nayo yapelekeni kwa waziri mkuu, haiwezi kumaliza mwezi mmoja nitayalipa yote.

*Mwl. Simoni Keha-Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)*

#Chama cha walimu kimefanya vikao kadhaa na serikali, ambazo hoja zetu zimepokelewa tunaamini zitafanyiwa kazi kwa maslahi wa walimu.

#Tunapongeza Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa uamuzi wa kuwajengea walimu nyumba.

#Tunaishukuru Serikali kwa Umamuzi wa kupeleka Bungeni sheria ya mabadiliko ya Hifadhi ya Jamii

*Mwl. Leah Ulaya Kaimu Rais-Chama cha Walimu-(CWT)*

#Juhudi zako na Serikali zinaonekana wazi, Watanzania na walimu tumeanza kuiona Tanzania Mpya.

#Walimu tunaimani sana na serikali yako, walimu wako ni wazalendo.

#Watumishi wote nchini tuungane kwa pamoja kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli ili aendelee kututumikia.

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*

Wednesday, 13 December 2017

IJUE HISTORIA YA ISRAEL

 

Israeli ni nchi yenye eneo la kilomita za mraba 20,770 na idadi ya watu 8,600,000 kwa mjibu wa sensa ya mwaka 2016.
Kihistoria waisraeli waliishi katika nchi iliyoitwaKanaani, halafu Israeli kuanzia mnamo 1200 KK hadi mnamo mwaka70 BK Waroma wa Kale walipovamia na kuharibu Yerusalemu, ambao tena mwaka135 waliwafukuza wote kutoka nchi yao.

Historia ya Israeli ya Kale inaanza tangu kupatikana kwa taifa hilo katika nchi yake inayoitwa Israeli. Kufuatana na masimulizi ya Agano la Kale taifa la Israeli lilianzishwa na wanawaisraeliwaliotoka Misri chini ya uongozi wa Musa na kuvamia Kanaani mnamo mwaka1200 KK chini ya Yoshua.

Wataalamu wengine wa kisasa wanaona ya kwamba taifa lilitokea hasa ndani ya nchi kwa kuungana kwa vikundi mbalimbali.

Muungano huo wa vikundi na makabila ukawa taifa na kuunda ufalme wa kwanza wa Israeli wakati wa mfalme Sauli aliyefuatwa na Daudina mwanae Suleimani.

Baada ya kifo cha Suleimani likatokeafarakano na jina la "Israeli" likatumiwa na ufalme wa kaskazini, wakati mji mkuu wa kaleYerusalemu ukaendelea kama mji mkuu waufalme wa Yuda.

Falme zote mbili zilishindwa katika vita na kuanzia mwaka 587 KK hapakuwa tena na dola la kujitegemea, bali eneo lilikuwa chini ya falme mbalimbali kama vile Babiloni, Uajemina Ugiriki wa Kale.

Lakini harakati za Wamakabayo za kurudishauhuru uliweza kuwafukuza Wagiriki na kuanzisha ufalme wa Kiyahudi kati ya 140 KKhadi 4 KK.

Hata hivyo kuanzia mwaka 63 KK ufalme huo uliwekwa chini ya ulinzi wa Dola la Roma na polepole kugawiwa na hatimaye kuwa jimbo la Kiroma (tangu 70 BK).

Maangamizi ya Yerusalemu mwaka 70 BK huhesabiwa kama mwisho wa Israeli ya Kale. Wataalamu wengine wanaona tayari uvamizi wa mji wa 587 KK na Wababeli kama mwisho wa kipindi hiki na kuangalia kipindi kati ya 587 KK hadi 70 BK kama kipindi kipya.       
 FAHAMU MJI WA YERUSALEMU NA MZOZO ULIOPO
Kumekuwa na mzozo wa muda mrefu kuhusu udhibiti wa mji wa Jerusalem kati ya Waisraeli na Wapalestina.Mji huo kwa sasa huwa umegawanywa mara mbili, Jerusalem Mashariki na Jerusalem Magharibi.Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu nayo Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa), ingawa eneo hilo bado kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya 1967.Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa. Eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000.Israel ilitangaza 1980 Jerusalem yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi duniani hazikubali azimio hilo.Hivyo basi, balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Jerusalem, katika mji wa Tel Aviv.Mzozo huo umefufuliwa tena kutokana na hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kutarajiwa kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.     DINI ZILIZOPO KTKA MJI WA YERUSALEMU                          Mji huu huwa na umuhimu mkubwa kwa dini tatu kuu - Ukristo, Uislamu na Uyahudi. Dini zote tatu humuangazia Abraham anayetajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani.      Ni mji ambao umedhibitiwa na dini hizo kwa vipindi mbalimbali katika historia.          Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu. Mji huo ni miongoni mwa miji ya kale zaidi ambayo ipo hadi sasa duniani. Ni mji ambao umetekwa, ukabomolewa na kuharibiwa na kisha kujengwa tena.Kila sehemu ya ardhi yake ukichimba kwenda chini hufichua enzi fulani katika historia yake.Ingawa umekuwa chanzo cha ubishi na mzozano kati ya dini mbalimbali, dini zote huungana kwa pamoja kuungama kwamba ni eneo takatifu.Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale. Kuna maeneo manne makuu na kila eneo, majengo huwa tofauti. Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia. Eneo hilo huzungukwa na ukuta mkubwa wa mawe. Hapo, kunapatikana baadhi ya maeneo yanayoaminika kuwa matakatifu zaidi duniani.Kila eneo kati ya maeneo hayo manne (unaweza kuyaita mitaa) huishi watu wa aina moja. MTAA WA WAKRISTO Wakristo wana maeneo mawili, kwa sababu Waarmenia pia ni Wakristo. Eneo lililotengewa Waarmenia, ambalo ndilo ndogo zaidi kati ya hao manne, lina vituo vya kale zaidi vya Waarmenia duniani.Jamii ya Waarmenia imehifadhi utamaduni wake wa kipekee ndani ya Kanisa la St James na nyumba kubwa ya utawala. Maeneo hayo mawili yamechukua sehemu kubwa ya mtaa huo wa Waarmenia.Ndani ya mtaa wa Wakristo, kuna Kanisa Kuu la Kaburi na Ufufuo wa Yesu Kristo, ambalo ni muhimu sana kwa Wakristo kote duniani.Hupatikana katika eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika kisa cha kusulubiwa, kufariki na kufufuka kwa Yesu.Kwa mujibu wa utamaduni wa Kikristo, Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary. Kaburi lake linapatikana ndani ya kanisa hilo la kaburi na inaaminika kwamba hapo ndipo alipofufuka.Kanisa hilo husimamiwa kwa pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kikristo.Sana huwa ni wahudumu wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia.Kuna pia wahuudmu kutoka kanisa la Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.MTAA WA WAISLAMU Mtaa wa Waislamu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf.Waislamu huamini kwamba Mtume Muhammad alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote. Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe la msingi. Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.MTAA WA WAYAHUDI Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka lililokuwa Hekalu Takatifu.Ndani ya hetalu hilo kulikuwa na Patakatifu pa Patakatifu, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa.Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac. Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa Patakatifu.Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia hutembelea eneo hilo kuomba na kukumbuka utamaduni wao, hasa nyakati za siku kuu za kidini.           
   By E.KAULULE
    source:  wikipedia

MATATIZO YA HEDHI NA TIBA YAKE KWA WANAWAKE


Na Archandramu Mbungu.
KILA mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika.

DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.

TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

PAPAI NALO NI DAWA
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

Monday, 11 December 2017

AZIKA MWANAE AKIWA HAI KISA AMEAHIDIWA KUOLEWA NA TAJIRI


Mama mmoja amezika mwanae wa miezi mitatu akiwa hai baada ya kuahidiwa kuolewa na kijana tajiri. Mama huyo hakutaka kumwambia mwanaume huyo kuwa tayari alikuwa amezaa mtoto na mwanaume mwingine.

Kwa ajili ya kutaka kudumisha uhusiano mpya na tajiri huyo ndipo alipoamua kufanya tukio hilo la kutisha. Alimvizia mtoto huyo amelala na kwenda kumzika akiwa hai.

Tukio hili limebainika baada ya ndugu na majirani kumuona pekee pasipo mtoto ndipo walimbana hadi akasema ukweli kuwa amemzika mtoto huyo siku mbili zilizopita.

A single mother buried her 3 months old baby after she met a rich man who promised to marry her.

She did not tell the rich man that she already had a child from a married man. In order to save her new relationship with the rich young man.. she decided to play single by getting rid of the child.

Sadly she buried her the child alive while the child was asleep. This is sad brothers and sisters.


Share ili kupinga na kukomesha vitendo viovu

*HEBU ANGALIA UMUHIMU WA KUHESHIMU WATU WENGINE *

1. Kuzaliwa kwako kumefanywa na *watu wengine.*

2. Jina lako umepewa na *watu wengine.*

3. Umepata elimu kutoka kwa *watu wengine.*

4. Kipato chako kwa namna fulani kinatoka kwa *watu wengine.*

5. Hata Heshima uliyonayo unapewa na *watu wengine.*

6. Wa kwanza kukuogesha ni *watu wengine.*

7. Wa mwisho kukuogesha pia watakuwa  *watu wengine.*

8. Mazishi yako yatasimamiwa na *watu wengine.*

9. Utapelekwa kuzikwa na *watu wengine.*

10. Kila unachokimiliki kitarithiwa na *watu wengine.*

 Sasa kwa nini unakuwa na kiburi,dharau na nyodo dhidi ya *watu wengine* ?

 Kumbuka hakuna sehemu yoyote katika maisha yetu isiyohitajia *watu wengine.*

Ni matumaini yangu ujumbe huu utawarushia na *watu wengine.*

Sunday, 10 December 2017

UTU NI ZAIDI YA FEDHA NA HESHIMA YA DUNIA...


MWAKA 1993 MWEZI MARCH MPIGA PICHA MAARUFU WA AFRICA KUSINI (PHOTOJOURNALIST) KEVIN CARTER ALITEMBELEA NCHI YA SUDAN KWA AJILI YA KUPIGA PICHA ZA HABARI KUHUSIANA NA BALAA LA NJAA LILILOIKABILI NCHI HIYO.
NI KIPINDI AMBACHO NCHI YA SUDAN ILIKUMBWA NA BALAA KUBWA SANA LA NJAA HALI ILIYOPELEKEA WATU WENGI KUFA NJAA NA WENGINE WAKIHANGAIKA KUOKOA UHAI WAO KWA KULA MAGOME YA MITI, NYASI NA MIZIZI.
NI KIPINDI KIBAYA SANA KATIKA HISTORIA YA SUDAN KWA SABABU JUMUIYA YA KIMATAIFA ILISITA KUPELEKA MSAADA WA CHAKULA KUTOKANA NA HALI MBAYA YA KISIASA ILIYOKUWEPO SUDAN (VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE).
JAPO BAADAE UMOJA WA MATAIFA (UN) ULIKUBALI KUPELEKA MSAADA WA CHAKULA LAKINI WATU WENGI WALIKUA WAMESHAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BALAA LA NJAA.
NI KIPINDI HIKI NDIPO KEVIN CARTER ALIENDA NCHINI SUDAN AKIFUATANA NA MWANDISHI MWENZIE WA KIRENO JOÃO SILVA KURIPOTI JUU YA BAA LA NJAA LILILOIKUMBA NCHI HIYO.
KATIKA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE WA KIKAZI KEVIN ALIFANIKIWA KUPIGA PICHA YA MTOTO MMOJA MDOGO ALIYESHINDWA KUENDELEA NA SAFARI YA KUWAFUATA WALEZI WAKE WALIOKUWA WAMEENDA KUPOKEA CHAKULA CHA MSAADA TOKA UN. MTOTO HUYO ALIPEWA JINA LA KEN.
NDEGE ZA UN ZILIKUA ZIKIDONDOSHA MSAADA WA CHAKULA KWA WANAKIJIJI WA ENEO HILO. WAZAZI WA KEN WALIFARIKI KWA NJAA NA YEYE KULELEWA NA JAMAA WA KARIBU.
SIKU HIYO WALEZI WA KEN WALIENDA KUOKOTA CHAKULA CHA MSAADA KILICHOKUWA KIKIDONDOSHWA NA NDEGE ZA UN. KEN ALIJARIBU KUWAFUATA WALEZI WAKE LAKINI ALIISHINDWA KUENDELEA NA SAFARI KATIKALI YA PORI KUTOKANA NA UCHOVU, NJAA KALI, KIU, NA MWILI KUKOSA NGUVU. AKIWA PEKE YAKE PORINI ALIANGUKA.
AKAJARIBU KUFICHA KICHWA CHAKE ARDHINI KUTOKANA NA JUA KALI LILILOKUA LIKIWAKA (ZAIDI YA NYUZIJOTO 40°C). HAPAKUWA NA MTI WA KUJIKINGA MAANA MITI ILIKAUKA KWA UKAME, MINGINE WATU WALIKULA MAGOME WAKIWA KATIKA JITIHADA ZA KUJIOKOA NA NJAA.
KEN HAKUJUA KUWA NYUMA YAKE KULIKUA NA NDEGE AINA YA "TAI" AMBAYE HULA MIZOGA NA ALIKUA AKIMNYEMELEA. AKIWA PALE CHINI ALIVAMIWA NA NDEGE HUYO AMBSYE ALIMDONOA SEHEMU YA UTOSI NA KUMUUA KABLA YA KUANZA KULA NYAMA YAKE KWA KUDONOA KAMA ADONOAVYO MIZOGA.
WAKATI NDEGE HUYO AKIMKARIBIA KEN, MWANDISHI WA HABARI KEVIN CARTER ALIKUA NA CAMERA YAKE AKIPIGA PICHA. BAADAE AKACHUKULIWA NA NDEGE ZA UN NA KUMUACHA MTOTO HUYO AKILIWA NA "TAI" BILA MSAADA WOWOTE.
PICHA HIYO ILICHAPISHWA KWENYE GAZETI LA NEW YORK TIMES TAR.26 MARCH 1993 NA KUIBUA MJADALA MKUBWA JUU YA MAADILI YA TAALUMA YA UPIGAJI PICHA ZA HABARI (ETHICS OF PHOTOJOURNALISM).
WENGI WALILAUMU KITENDO CHA KEVIN CARTER KUPIGA PICHA NA KUACHA KUOKOA MAISHA YA MTOTO YULE. KATIKA UTETEZI WAKE CARTER ALISEMA HAKUJUA KAMA TAI YULE ANGEMSHAMBULIA KEN.
ALIONGEZA KUWA ALISUBIRI KWA MUDA WA DAKIKA 20 KUONA KAMA TAI YULE ANGERUSHA MBAWA ZAKE KUMSOGELEA KEN. ALIPOONA TAI HUYO HAMSOGELEI MTOTO HUYO ALIAMUA KUONDOKA KWA NDEGE MAALUM ZA UN ZILIZOKUA ZIKITOA MSAADA ENEO HILO NA KUMUACHA MTOTO KEN PEKE YAKE. LAKINI BAADAE AKAAMBIWA KUWA MTOTO HUYO ALIDONOLEWA NA TAI HADI KUFA.
TAARIFA NYINGINE ZINADAI KUWA CARTER ALIKUA AKITEKELEZA KAZI ALIYOPEWA NA MUAJIRI WAKE, KWAMBA AKIFIKA SUDAN AFANYE KAZI MOJA TU YA KUPIGA PICHA NA ALIZUIWA KUFANYA KAZI YA UOKOAJI KWA SABABU HAKWENDA SUDAN KWA KAZI HIYO.
PAMOJA NA HAYO YOTE CARTER ALITUNUKIWA TUZO KWA PICHA HII, MNAMO MWEZI APRIL MWAKA 1994 KWENYE TUZO MAARUFU ZA PULITZER. PICHA HII ILIPEWA TUZO YA KUWA PICHA BORA YA MAKALA (FEATURE PHOYOGRAPH).
LAKINI CARTER HAKUIFURAHIA TUZO HIYO KUTOKANA NA KUKOSA UTU AMBAO ULIPELEKEA KIFO CHA MTOTO KEN. ALIISHI MAISHA YA MASONONEKO NA KUJILAUMU KILA MARA KWA KUSHINDWA KUOKOA MAISHA YA MTOTO YULE.
ALIOMBA RADHI KWA KUSEMA ''KWAKWELI NAOMBA MSAMAHA KWA KUTOMUONDOA MTOTO HUYO KATIKA MAZINGIRA YA HATARI (“I’M REALLY, REALLY SORRY I DIDN’T PICK THE CHILD UP,”).
TAR.27 MWEZI JULY MWAKA 1994 (MIEZI MINNE TU BAADA YA KUPOKEA TUZO) KEVIN CARTER ALIAMUA KUJIUA KWA SUMU YA CARBON MONOXIDE (CARBON MONOXIDE POISONING) KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO ULIOSABABISHWA NA HISTORIA YA SUDAN YA KIFO CHA MTOTO KEN.
KEVIN CARTER ALILIPWA FEDHA NYINGI SANA NA GAZETI LA NEW YORK TIMES KWA PICHA ILE. HALI KADHALIKA ALIPEWA TUZO YA HESHIMA KWA UPIGAJI PICHA BORA, LAKINI BAADAE AKAONA VYOTE HAVINA THAMANI KWA KITENDO ALICHOKIFANYA KWA KUKOSA UTU.
KABLA YA KUJIUA CARTER ALIANDIKA UJUMBE KWENYE KIPANDE CHA KARATASI AKISEMA "MAUMIVU YA MOYO YANAZIDI FURAHA YA FEDHA" (THE PAIN OF HEART OVERWEIGH THE JOY OF GETTING MONEY)...
.... NAJISIKIA VIBAYA SANA, KUMBUKUMBU ZA MAUAJI, NJAA NA MATESO YA MTOTO KEN ZINANIJIA KILA MARA. NAENDA KUMFUATA NA KUMUOMBA MSAMAHA KAMA NITAPATA BAHATI YA KUFANYA HIVYO... ( I AM SO DEPRESSED ... I AM HAUNTED BY THE VIVID MEMORIES OF KILLING, ANGER AND PAIN OF STARVING CHILD KEN... I HAVE GONE TO JOIN HIM AND ASK FOR FORGIVENESS IF THAT OPPORTUNITY ARRISE."
MY TAKE!
MALI, FEDHA, NA HESHIMA YA DUNIA HAVIWEZI KUZIDI UTU WA BINADAMU MWENZIO (HUMAN DIGNITY). KEVIN
CARTER ALIKUBALI KUUZA UTU WA MTOTO KEN KWA FEDHA NA HESHIMA YA KUPATA TUZO, LAKINI BAADAE DHAMIRI IKAMHUKUMU NA AKAAMUA KUJIUA.
JIULIZE UNAISHIJE.? UNATHAMINI UTU WA WENZIO AU UNAJALI ZAIDI FEDHA, MALI NA HESHIMA YA DUNIA KULIKO UTU?
UNA UHAKIKA WA MILO MITATU NA WAKATI MWINGINE UNATUPA CHAKULA LAKINI JE UNAJUA KUNA WATU WASIO HATA NA UHAKIKA WA MLO MMOJA, NA WENGINE WANAKUFA KWA KUKOSA CHAKULA? JE UNAWASAIDIAJE?
UNASAFIRI NJIANI NA GARI BINAFSI, UKO PEKE YAKO LAKINI UNAOMBWA LIFT NA BIBI KIZEE MGONJWA UNAKATAA ETI ATAKUCHAFULIA GARI. UNATHAMINI MALI KULIKO UTU??
KUMBUKA MALI ZA DUNIA, FEDHA NA HESHIMA YA DUNIA NI VYA KITAMBO TU, LAKINI UTU WA MTU NI HAZINA YA MILELE.  KEN.!