Monday, 20 November 2017
RAIS MUGABE KWA HILI ANASTAHILI PONGEZA
Sasa siyo siri tena kwamba Afrika nzima Simba wa Nyika amebaki mmoja tu nae ni Rais wa sasa wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe na huenda siku ambayo Mwenyezi Mungu ataamua kumchukua huyu Mzee basi bara zima la Afrika litakuwa limepoteza ' Lulu / Thamani ' ya kweli ya Kiongozi madhubuti.
๐๐ผSiku ya Jumanne wiki hii Dunia nzima ilipatwa na mshtuko mkubwa hasa baada ya kutokea sintofahamu huko nchini Zimbabwe baada ya pale Rais wa nchi hiyo Mzee Mugabe alipozingirwa katika makazi yake ya Kifahari ( Palace ) jijini Harare huku Jeshi likichukua hatua za kuimarisha Ulinzi mkali nchini humo kwa msaada ya Magari ya Kijeshi.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
Ufuatao ni mtiririko kama siyo mserereko mzima wa Ripoti Maalum ya juu ya chote kilichotokea huko nchini Zimbabwe ambapo nitaelezea ilivyokuwa, ilivyo na mwisho wake wote utakuwaje ambapo mwishoni wote tutakubaliana kwamba Rais Mzee Mugabe kweli ni Mzee ila bado akili na mbinu zake ni za hali ya juu.
๐๐ผMiezi ya hivi karibuni inaelezwa kwamba Rais Robert Mugabe kwa Siri kabisa aliwaita Watu wake wa karibu aliyekuwa Makamu wake wa Rais Bwana Emerson Mnangagwa na Mkuu wa Majeshi wa Zimbabwe Jenerali Chiwenga na kuwaeleza mambo yake kadhaa ya Kifamilia ambayo yalikuwa yakimtatiza kwa muda mrefu,
Katika Kikao chake hicho na hawa Watu wake wa karibu Rais Mugabe alifunguka zaidi Kwao kwa kuwaambia kwamba mara kwa mara amekuwa katika mvutano na Mkewe Grace na kwamba tokea mwaka 2008 alipanga Kuachana na Urais wa Zimbabwe lakini Mkewe alikuwa hataki na akimshinikiza kuwa asitoke na mpaka hata kuutishia Uhai wake kitu ambacho kwakweli kilimkera sana Yeye ( Rais Mugabe )
๐๐ผHivyo mara baada ya Rais Mugabe kufunguka hivyo kwa hawa Watu wake wa karibu huku akiwataka wamsaidie sana kwakuwa amevumilia karaha za Mkewe Grace kiasi kwamba hadi amejuta kuwa nae kwakuwa amemsababishia Uadui mkubwa dhidi yake kutoka kwa Wazimbabwe hasa kutokana na maisha ya Kifahari aliyokuwa akiishi Grace.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
MUITIKIO WA MAKAMU WA RAIS NA MKUU WA MAJESHI CHIWENGA KWA RAIS MUGABE.
๐๐ผMara baada ya Rais Mugabe kuwaambia yote hayo hawa Watu wake wa karibu Makamu wa Rais Emerson Mnangagwa na Mkuu wa Majeshi Chiwenga na wao pia wakamuambia kwamba kwakuwa amewaambia ukweli wote juu ya kinachomsibu basi awape muda ili wawili hao wakae chini na waandae mkakati maalum ambao ungewahusisha Watu wa Idara za Kijasusi za Zimbabwe na Jeshi la nchini Zimbabwe.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
HALI IKAWAJE...!?
๐๐ผBaada ya wawili hawa Makamu wa Rais na Mkuu wa Majeshi kumaliza kupanga mikakati yao walirudi kwa Rais Mugabe na kumpa mrejesho wao na mkakati kabambe waliouopanga ambao wao waliamini kwamba ungefanya Kazi kwani umeshirikisha Watu wengi na hadi baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Chama chake cha ZANU-PF.
๐๐ผWalipomaliza kumpa mkakati wote Rais Mugabe ( ambao mkewe Grace katika mambo yote haya hakushirikishwa ) ndipo Rais Mugabe akaanza kuutekeleza ambapo aliunda Timu maalum ya kutengeneza fitna ndani ya Serikali yake na Chama chake cha ZANU-PF ili mradi tu akija kufanya maamuzi fulani basi yaendane sambamba na yale maelekezo yote aliyopewa na Makamu wake wa Urais na Mkuu wake wa Majeshi.
๐๐ผPasipo Wazimbabwe wote kujua kwamba Rais Mugabe ni zaidi ya wamjuavyo na kwamba siku zote hata kama Ng'ombe akiwa Mzee ila hazeeki maini Mzee huyu alipohakikishiwa na Timu yake ya Fitna kuwa kila kitu sasa kipo tayari huku Makamu wa Urais na Mkuu wa Majeshi wakijua kila kitu Rais Mugabe alijifanya kumtafutia zengwe Makamu wake Urais kisha akamfuta Kazi na mara baada ya kumfuta Kazi hapo hapo tena akaitisha Mkutano maalum na Wanachama wa ZANU-PF na kumteua Mkewe kuwa Makamu wa Urais kuchukuwa nafasi ya Emerson Mnangagwa.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
KILICHOFUATIA
๐๐ผMara baada ya Rais Mugabe kuyafanya yote hayo kama ambavyo alielekezwa na akina Emerson na Chiwenga Rais Mugabe kwa Siri tena aliwatonya hawa hawa Watu wake kwamba Mkewe Grace ni mwoga sana na kwamba hapendi Umasikini na ni mfujaji mkubwa wa Mali za Wazimbawe na kwamba Yeye binafsi ameshamchoka na alichokuwa akikitaka ni Yeye na Grace kutenganishwa kwani kuna Msiri wake ndani ya Familia yake alishawahi kumwambia kwamba aliwahi kuambiwa na Grace mwenyewe kwamba hampendi Rais Mugabe ila yuko nae Kwanza ili kuhakikisha anapata Utajiri na muda ukifika ataachana nae na Yeye kuishi maisha yake na Wanae.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
MPANGO MKUBWA ULIOPANGWA NA UKAFANIKIWA NI UPI..
๐๐ผKila kitu kilipohakikishwa kwamba kipo tayari akina Makamu wa Rais Emerson na Mkuu wa Majeshi Jenerali Chiwenga walimwambia Rais Mugabe kwamba sasa atulie tuli kwani wanaenda kumaliza mzizi wa fitna ili lengo lake la kutaka Kupumzika Siasa na kuachana na Mkewe Grace.
๐๐ผMara baada ya kuhakikishiwa kwamba yote haya yakifanyika hali ya Usalama wa Wanazimbabwe na nchi ya Zimbabwe utakuwa salama tu na hakuna jambo baya litakolotokea Rais Mugabe aliwaruhus wawili hawa kutekeleza sasa rasmi mkakati wao huku Yeye akijifanya kama hajui kinachoendelea.
๐๐ผNdipo asubuhi ya Jumanne wiki hii ya tarehe 14 November, 2017 Wazimbabwe wengi wakiwa hawajui kinachoendelea Jeshi la Zimbabwe likaamua kujitokeza hadharani huku likiwa na Vifaa vyote vya Kivita na haraka haraka kushika / kudhibiti maeneo maalum na kwenda pia kumzingira Rais Mugabe katika ' Palace ' yake huku Mkewe Grace nae akiwemo.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
MTEGO ALIOTEGWA GRACE MUGABE BILA YEYE KUUJUA NA AKAUKANYAGA NI HUU
๐๐ผMara baada ya Jeshi la Zimbabwe kumzuia Rais Mugabe nyumbani Kwake katika Kasri lake ( Palace ) alipandikizwa Mwanamke mmoja ambaye inasemekana alikuwa ni mwana Usalama wa Taifa wa Zimbabwe ambapo alihakikisha anamtisha na kumshawishi Mkewe Rais Mugabe Grace kwamba atoroke kwani Mumewe anaenda Kuuwawa na Yeye atakamatwa, Kushtakiwa na Kufilisiwa Mali zake zote.
๐๐ผGrace Mugabe ( Mkewe Rais Mugabe ) baada ya Yeye kuambiwa haya yote pasipo kujua kwamba yote hayo anayoambiwa yalishapangwa mapema na hata Mumewe Rais Mugabe pamoja na Viongozi wengine Waandamizi hasa wa Usalama wanajua akakubaliana na ule ushauri wa yule Dada Jasusi na usiku akatoroka Jijini Harare kwa msaada wa yule Dada na kuelekea nchi jirani ya Namibia kusikilizia japo taarifa za ndani zaidi zinasema kwamba huenda Grace Mugabe akawa amekimbilia Botswana au Dubai au Malaysia ambako ndiko kuna Mali nyingi za Familia ya Mugabe na ambazo nyingi zina umiliki wake Yeye ( Grace )
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
MAFANIKIO YA MKAKATI WA SIRI
๐๐ผMara baada ya kuhakikisha kwamba Grace Mugabe ameshatoroka Jijini Harare yule Dada Jasusi alirudisha mrejesho kwa Mabosi zake Makamu wa Rais Emerson, Mkuu wa Majeshi Jenerali Chiwenga na Wakuu wa Usalama ndipo lengo lao likatimia 100% ambapo ili kuwazuga Watu wengi na kuwahadaa Wazungu ambao muda wote wa hili tukio la Jumanne walikuwa wakifurahia Jeshi likajifanya kuchukua hatamu lakini kumbe chini kwa chini mikakati mingine ikipangwa huku Rais Mugabe nae akishirikishwa moja kwa moja.
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
MAKUBALIANO YA AWALI
๐๐ผKutokana na hali yote ilivyokuwa na mkakati kufanikiwa kwa 100% Rais Mugabe aliwaambia akina Emerson na Chiwenga kwamba kiukweli Yeye sasa amechoka Kuongoza hivyo alichokuwa akitaka ni kwamba kwa siku hizi mbili tatu Jeshi la Zimbabwe chini ya Jenerali Chiwenga lishike hatamu lakini pia watafutwe Viongozi Waandamizi wa Kamati Kuu ya Chama cha ZANU-PF ili wataarifiwe kwamba Mzee Mugabe anataka Kupumzika hivyo ameamua kumuachia Uongozi Makamu wake yule yule ambaye mwanzo alimfukuza ( kimkakati zaidi )
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
Yafuatayo ni MAKUBALIANO MAALUMU
๐๐ผYaliyofanyika katika Vikao vya Jeshi tokea jana, juzi na jana na Rais Mugabe:
1. Rais Mugabe akijiuzuru hatoshtakiwa
2. Rais Mugabe akijiuzuru ataendelea Kulipwa Pensheni yake
3. Rais Mugabe akijiuzuru Mali zake hazitoguswa wala kutaifishwa
4. Rais Mugabe akijiuzuru atatangazwa kuwa Baba wa Taifa na kupewa Heshima hadi Mauti
5. Rais Mugabe atakubali rasmi aliyekuwa Makamu wake Emerson Mnangagwa amrithi.
6. Rais Mugabe atawashawishi Wajumbe wote wa ZANU-PF wakubali kujiuzuru Kwake
7. Rais Mugabe atahakikishiwa Ulinzi wake na Mali zake zote mpaka atakapokufa..
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
KITENDO CHA KUONEKANA KATIKA MAHAFALI KINAASHIRIA NINI..!?
๐๐ผKitendo cha Rais Mugabe kuonekana leo katika Mahafali katika Chuo Kikuu jijini Harare kilikuwa ni cha Kimkakati zaidi na hasa katika Kuimarisha Umoja, Amani na Utulivu kwa wana Zimbabwe na kuonesha kwamba Zimbabwe iko salama kitu ambacho hakijafurahiwa kabisa na Nchi za Ulaya hasa Marekani na Uingereza ambao walishaanza kushangilia Kitendo kilichotokea na haraka sana wakamuibua ' Kibaraka ' wao wa muda mrefu aliyekuwa Kiongozi wa Upinzani Bwana Morgan Tshivangirai aanze ' chokochoko ' zake lakini akagundua kwamba Nchi bado iko salama na asingefanikiwa..!!
๐๐ผ๐๐ผ๐๐ผ
HITIMISHO
๐๐ผKinachofanyika sasa ni mazungumzo ya ndani kwa ndani katika Serikali ya Zimbabwe na Chama cha ZANU-PF na kama mambo yataenda kama yalivyopangwa basi kuna uwezekano mkubwa siku chache zijazo au wiki ijayo Rais Robert Mugabe akatangaza rasmi kuachia ngazi Urais wake na kumkabidhi rasmi Bwana Emerson Mnangagwa hivyo kupelekea kutimia kwa mikakati ya Kisiri iliyopangwa na ambayo kiukweli imepangika na inaelekea kufanikiwa na kuwa ni alama ya ushindi kwa Rais Mugabe....!!
๐๐ผ..MWISHO..๐๐ผ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment