Sunday, 10 September 2017

Kwanini Ni Muhimu Kufahamu Saikolojia Za Watu

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Archandramu .com.Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama tena siku hii ya leo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani leo ni siku bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kufanya yale tuliyotazamia kuyafanya na kutegemea kupata  ushindi. Rafiki, kama umestahilishwa kuiona tena siku hii ya leo basi utumie muda wako vizuri vilivyo.
Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Basi ndugu msomaji, karibu sana tuweze kusafiri tena kimawazo siku hii ya leo hadi pale tamati ya somo letu la leo.
Kila mmoja wetu ni wazi kuwa amekulia malezi tofauti, tumetokea tamaduni tofauti, kwahiyo kila mtu ana tamaduni zake na hata falsafa au misingi yake aliyojijengea au kujengewa na wazazi. Kila mtu ana mitazamo yake katika maisha mwingine ana mitazamo chanya na mwingine ana mitazamo hasi. Kwahiyo, katika jamii yetu tunaishi na watu wa kila aina na kila mtu ana changamoto zake za kimaisha.
Rafiki, tunaalikwa kuelewa saikolojia ya watu kwanza ili uweze kuendana nao, mara nyingi watu ni wagumu kubadilika na pale unapomlazimisha kitu ndiyo anaweza asifanye kabisa akaishia kukusikiliza tu lakini kutenda ni hakuna. Hakuna kazi ngumu kama kuishi na watu hata ufanye kitu gani lakini kumbuka kuwa huwezi kumfurahisha kila mtu lakini unaweza kujifurahisha wewe mwenyewe tu. Kila mtu  atapenda ufanye vile anavyotaka yeye na mwingine vivyo hivyo mwisho wa siku inakuwa ngumu kumridhisha kila mtu.
Kwahiyo, sisi kama binadamu tunapaswa kusomana na kuelewa saikolojia za mwenzako ndiyo mtaweza kwenda pamoja. Wewe usipate shinda ya kumbadilisha kila mtu bali pata shida ya kujibadilisha wewe mwenyewe kwanza na watu wengine ishi nao kama vile saikolojia yao inavyotaka na mambo yako yaendelee mbele, maisha yako ya songe. Kuna watu ambao maisha yao wamezoea kuumizwa, kufanyiwa ubaya, kutukanwa kwahiyo wengine hawajui hata ladha ya upendo katika maisha yao hivyo wanaona ni sawa nao kuwatendea wenzao kama vile walivyozoea kutendewa wao.
Wengine hawapendi kumuona mtu akifurahi, mambo yake yakienda vizuri, kuna wengine wana maisha ya wivu, akiona wenzake kapata nafsi yake inauma kweli, kuna mambo mengi sana unapaswa kuwaelewa watu na ishi nao kwa akili sana. Waelewe watu hawatakusumbua kabisa katika maisha yako kwani kuna aina za watu mbalimbali na kama ukishazielewa saikolojia zao ziko upande gani basi umeshamweza.
Hatua ya kuchukua leo, kila mtu ana mitazamo yake ya maisha, kila mtu ana changamoto zake za maisha hivyo ni vema kuwaelewa watu, soma saikolojia zao ili uweze kuendana nao. Kuwa makini na watu siyo kila mtu ni wa kumwambia hadithi zako,siyo kila mtu ni wa kumuuliza swali na kutegemea kupatiwa jibu sahihi. Uliza swali sehemu sahihi na utapata jibu sahihi.
Mwisho, wazungu wanasema perspective is your choice wakiwa na maana ya kwamba mtazamo wako  ndiyo changuo lako. Wanafalsafa wanaamini kuwa hakuna kitu kizuri au kibaya bali kila kitu kinatokana na mtazamo wako wewe yaani jinsi unavyolihukumu jambo husika. Kwahiyo, waelewe watu  na tambua kila mtu ana matatizo yake na ukishawajua watu hawawezi kukupa shida.

No comments:

Post a Comment