Monday, 1 May 2017

*YALIYOJIRI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI), 2017 KATIKA VIWANJA VYA CHUO CHA USHIRIKA MOSHI,MKOANI KILIMANJARO*


#Tunakushukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo suala la elimu bure nchini - Said Meck Sadik.

#Kati ya walimu wa Sayansi 100 waliopangikiwa mkoa wa Kilimanjaro, 94 wamesharipoti - Said Meck Sadik.

#Serikali ya Mkoa imekuwa ikisisitiza uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi mahala pa kazi - Said Meck Sadik.

# Changamoto ya ukosefu wa ajira ni la tatizo la Dunia na Tanzania ni moja ya nchi inayokabiliwa na tatizo hilo - Mkurugenzi ILO.

#Kwa jitihada zinazofanywa na serikali, tunaona uchumi wa kati uko karibu - Mkurugenzi  ILO.

# Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi kwa ukaribu na TUCTA na ATE - Jenista Mhagama.

#Tucta inaishauri Serikali kufuata sheria za kazi katika kuwachukulia hatua wafanyakazi - Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunaishauri Serikali kuharakisha uboreshaji wa mifuko ya jamii ili wafanyakazi waanze kunufaika - Dkt. Yahaya Msigwa.

#Wapo waajiri ambao wanakiuka sheria za kazi, mfano kunyanyasa watumishi na kutoa kazi kwa ndugu zao - Dkt.  Yahaya Msigwa.

#Tunaiomba Serikali kupandisha kima cha chini cha mshahara unaokatwa kodi kufikia 750,000/-. - Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tucta inawakumbusha wafanyakazi kutimiza wajibu wao sehemu za kazi - Dkt. Yahaya Msigwa.

#Si wajibu wa Tucta kutetea uovu kama vile ulevi, ubadhilifu na utoro sehemu za kazi - Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunaipongeza Serikali kwa kusisitiza uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi - Dkt. Yahaya Msigwa.

#Tunakushukuru Mhe. Rais kwa kubali kuwa mgeni wetu rasmi wa siku hii ya leo - Tumaini  Nyamhokwa - Rais TUCTA.

#Siku ya Wafanyakazi Duniani ni siku muhimu kwa wafanyakazi kutafakari masuala yanayowahusu - Rais  Magufuli.

#Wafanyakazi ndio injini ya maendeleo katika taifa lolote duniani - Rais Magufuli.

#Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wafanyakazi - Rais Magufuli.

#Nawahakikishia wafanyakazi kuwa tunaanza ukurasa mpya kwani serikali tumeamua kwenda mbele - Rais Magufuli.

#Nawaarifu kuwa serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha fao la Bima ya Ajira na wadau wameshatoa maoni - Rais Magufuli.

#Serikali inalishughulikia suala la ucheleweshaji wa mafao ili wafanyakazi wanapostaafu waache kuhangaika - Rais  Magufuli.

#Vyama vya Wafanyakazi ni mahala pa kazi na sio hiari na visigeuzwe sehemu ya migogoro - Rais  Magufuli.

#Waajiri wote wanatakiwa watoe mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kinyume na hapo ni kuvunja sheria - Rais Magufuli.

#Serikali itaendelea kusaini na kuridhia mikataba ya kimataifa wafanyakazi yenye maslahi kwa wafanyakazi - Rais Magufuli.

#TUCTA endeleeni kuwaelimisha wafanyakazi ili fedha za bodi ya mikopo ya elimu ya juu ikusanywe kikamilifu - Rais Magufuli

#Tumebaini watumishi hewa 19706 waliokuwa wanaisababishia serikali hasara ya Tsh Bil. 230 kwa mwaka katika misharaha peke yake - Rais Magufuli.

#Serikali itashughulikia suala la mfumuko wa bei ili kuondokana na ugumu wa maisha - Rais Magufuli.

#Wapo walio na umri wa kustaafu lakini hawataki kuondoka hawa nao tutaanza kuwafuatilia, hawana tofauti na watumishi hewa - Rais Magufuli

#Nilitaka nisafishe kwanza kabla ya kupandisha mishahara kwa wafanyakazi ili tusiwafaidishe wasiostahili - Rais Magufuli.

#Nawaahidi tutatoa ajira  52000 katika sekta mbalimbali baada ya kutoa watumishi hewa na walio na vyeti feki - Rais Magufuli.

#Yeyote atakayehamishwa hakuna kuhama mpaka ulipwe hela ya kuhamishwa - Rais Magufuli.

#Serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wafanyakazi na haitadharau wala kupuuza maombi yenu - Rais Magufuli

#Niwaahidi wafanyakazi kuanzia bajeti ijayo tutaongeza mishahara kutoka kiwango kilichokaa kwa muda mrefu - Rais Magufuli.

#Mwaka huu tutapandisha madaraja ya kazi pamoja na  kuweka nyongeza ya mishahara kuwa sawa na madaraja yake - Rais Magufuli.

#Serikali hii itakuwa mtetezi namba moja kwa wafanyakazi - Rais Magufuli.


#Nikitoka hapa nitakaa na Baraza la Mawaziri ili kuweka mikakati ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi - Rais  Magufuli.

#Kwa sheria zote zitakazoletwa kama miswada tutafanyia kazi kwa wakati ili mambo yenu yaende vizuri - Spika Job Ndugai

#Nasisitiza msiwahamishe wafanyakazi kabla hamjawalipa stahili zao - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

*_IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO_*

No comments:

Post a Comment