Hili ni tatizo la kiafya ambalo huathiri ukuta wa tumbo na kitovu. Tatizo hili husababishwa na mambo makubwa matatu; kwanza ni kasoro ya kuzaliwa. Hapa ni kwamba kitovu kinakuwa na kasoro tangu pale mtoto anapokuwa tumboni kabla hajazaliwa.
Tatizo hili kwa watu wazima lipo mara tatu zaidi kwa wanawake ukilinganisha na wanaume ambapo lipo kwa kiasi kidogo sana. Kwa watoto kiwango cha tatizo hili vinalingana kwa wote wa kike na wa kiume na tafiti zinaonesha kwamba, tatizo ni kubwa kwa watoto wa Kiafrika ukilinganisha na mataifa mengine.

Aina ya pili ya tatizo hili ni ngiri ya kitovu. Hii inatokea tu pasipo na kasoro za kuzaliwa nazo. Hili linatokea kutokana na shinikizo la mgandamizo wa hewa na nguvu ndani ya tumbo kunakosababishwa na unene kupita kiasi, kunyanyua mizigo mizito au vitu vizito mara kwa mara, kikohozi cha muda mrefu na ujauzito wa mimba ya mapacha kwa mwanamke.
Aina ya tatu ya ngiri ya kitovu inaitwa ‘Paraumbilical hernia’. Aina hii ya ngiri hutokea zaidi kwa watu wazima na husababishwa na kasoro upande wa juu wa kitovu kuelekea kwa juu kufuata mstari wa kati wa tumbo.

DALILI ZA UGONJWA
Ngiri hutokea katika eneo la kitovu ambacho kwa lugha nyingine huitwa ‘Umbilicus’, ‘navel’ au ‘Belly button’. Kwa watoto wachanga wanapozaliwa kitovu huwa kirefu sana na huungana na kondo la nyuma la mama ili kupeleka lishe na hewa ya oksijeni kwa mtoto anapokuwa tumboni.
Baada tu ya kuzaliwa, mtoto hujitegemea hivyo kitovu hukatwa katika eneo maalum ili kipungue urefu. Baada tu ya kitovu cha mtoto kupona, mtoto anaweza kupatwa na tatizo hili la ngiri ya kitovu tangu anapokuwa mtoto mchanga ambapo akilia kitovu kinatokeza juu na anaponyamaza kinarudi ndani.

Hali hii wakati mwingine humsababisha mtoto apatwe na maumivu makali huku akilia kila wakati.
Aina hii ya ngiri huwa haipasuliwi kwani huisha yenyewe baada ya miaka miwili hadi mitatu, lakini baada ya umri huo kama haikuisha basi mtoto atafanyiwa upasuaji kurekebisha.
Endapo mtoto ngiri hiyo itakuwa inamsumbua kabla ya umri wa miaka mitatu, basi hatapasuliwa bali itafanyiwa utaratibu wa kuirudisha kitaalam ili isiendelee kutokeza na kuleta maumivu.
Ngiri inapokuwa kubwa, tundu lake huwa haliongezeki hivyo husababisha matumbo na kila kitu kitachomoza na kubana nje kushindwa kurudi ndani na kusababisha hali iitwayo ‘Strangulation’.
Kama hali hii haitatibiwa mapema basi italazimika upasuaji wa dharura na ikichelewa huweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa. Tatizo hili hutokea hata kwa ngiri nyingine ambazo tutakuja kuziona katika matoleo mengine.

UCHUNGUZI
Ngiri ya kitovu huonekana kwa macho pale inapochomoza ambapo dhahiri itaonesha imechomoza, wakati mwingine mgonjwa atalalamika maumivu na kama ni mtoto atakuwa analia mara kwa mara.
Vipimo vingine vitategemea na daktari kadiri atakavyoona inafaa.

MATIBABU
Matibabu ya ngiri ni kupasuliwa, haishauriwi kufungia sarafu kwani inaweza kukosewa na kusababisha sehemu ya utumbo kubanwa au kuleta maambukizi ya ngozi kwenye kitovu. Kwa mtoto huisha yenyewe taratibu na ikibidi hupasuliwa baada ya umri wa miaka mitatu.
Wakubwa ni lazima ipasuliwe kama inaleta shida. Wahi hospitali ya mkoa kwa uchunguzi na tiba.

No comments:
Post a Comment