KIMENUKA HUKO INSTAGRAM ,BABU TALE AMPAMAKAVU LIVE ERIC SHIGONGO
Hili ni bifu jipya kati ya meneja wa Diamond ,Babu Tale na Mkurugenzi waGlobal Publishers inayomiliki magazeti ya udaku yaani Kiu,Ijumaa wikiend ,Risasi na Champion.
Takribani siku tatu hivi Erick shigongo amekuwa akipost ujumbe kenye ukurasa wake wa Instagram akizungumzia kumpa ushauri msanii Diamond kuwa makini katika tasnia yake ya mziki vinginevyo atazama kwenye shimo.
Ujumbe huo ulilenga hasa kumshauri msanii Diamondna menejiment yake kwa ujumla kutotoza gharama kubwa sana kwa show zandani ya nchi ili wale mashabiki wake wa kipato cha chini waweze kupata fursa ya kuhudhuria,
Jambo hilo halijampendeza Meneja wamsanii huyo Babu tale kwani ameona kama wameingilia biahara yao,na huu ndio ujumbe aliouandika Babu tale kumjibu EricShigongo
"Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya...baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako... siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata...ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali.... tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu... Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond... ila sie tume kaa kimya... na kujifanya unazunga eti unatushauri... kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?..... Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? ...na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya@Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost... ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa....tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa...hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe....mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa....yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum'bomoa msanii kupitia magazeti yako.....tafadhali heshimu heshima yetu kwako👍...... "Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao.....😓" "
No comments:
Post a Comment