Sunday, 5 March 2017
UMASIKINI NA UTAJIRI SIO BAHATI BALI NI UCHAGUZI NA MAAMUZI
Nikiwa najifunza katika maandiko nikakutana na andiko hili,
Kutoka 30 : 15 - Matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
Mungu anamuagiza Musa kuwaambia wana wa Israeli juu ya sadaka maalumu ya sensa. Kilichonishtua ni hiyo kauli ya Mungu kuwa MATAJIRI HAWATALETA ZAIDI WALA MASIKINI HAWATALETA KILICHOPUNGUA, nikajiuliza kwa nini?
Ndipo Roho wa Mungu akaanza kunifundisha, siwezi kueleza yote hapa lakini nakupa dondoo itakayokubadilisha maisha ukiamua kuamini na kutumia.
Mungu akaniambia TAJIRI na MASIKINI wote wanafursa sawa katika maisha.
=> Wote wanazaliwa na wanawake.
=> Wote wanazaliwa wakiwa uchi na hawajui chochote.
=> Wote wanakua na kuongezeka.
=> Wote wanamasaa 24 katika siku, saa 12 mchana na saa 12 Usiku.
=> Wote wanapumua chini ya jua moja.
=> Wote wanaumwa na kufa na kuzikwa na kuoza, kifupi wote ni wanadamu na wote ni sawa.
Nini kinachofanya mmoja kuwa MASIKINI na mwingine kuwa TAJIRI.
1. UTII
(Kufuatilia kitu kwa usahihi)
2. NIDHAMU (Matumizi ya muda)
3. KUKOMALIA KITU MPAKA KITOKEE (Maskini wengi wanakomalia mambo yasiyo na manufaa kwao, mfano watakomaa mpaka Mwenyekiti wa Chama cha Soka atolewe, watakomalia vyeti vya mtu, utadhani vitawapa hela. Kifupi wanatumia nguvu yao kwenye mambo yasiyo na manufaa.)
4. KUGHAIRI/KUPUUZIA MAMBO YA MSINGI.
Masikini wote huwa wanamuda wa kutosha na kesho. Atafanya kitu kwa uvivu akijua hata kesho atamalizia. Wakati Tajiri anakomaa ikiwezekana kila kitu kiishe leo ili kesho Ifanye mambo mengine.
5. KUDHARAU MAMBO MADOGO AU MWANZO MDOGO.
Kwa masikini biashara inayoingiza elfu mbili kwa kila bidhaa anaona ni ya kijinga na faida ni ndogo, hivyo anaifanya ili mradi siku ziende. Wakati tajiri anakomaa na faida ndogo akijua akikusanya kwa wingi itampeleka mahali.
Dereva wa Bodaboda anaingiza pesa nyingi kwa mwezi kuliko mfanyakazi wa kawaida wa Benki. Lakini madereva wa bodaboda wengi huishia kunywa Viroba na kuhonga wanawake, na kulalamika maisha magumu.
6. MASIKINI ANATAKA KUPUMZIKA MAPEMA ILI AKASTAREHE, TAJIRI YUKO RADHI KUTUMIA MUDA WA ZIADA KUMALIZIA KAZI ZAKE.
Maskini akiingia ofisini ataanza kunung'unika kwanza, kulaumu foleni, hali ya hewa, kazi nyingi, mshahara unachelewa, katika hayo anatumia muda mwingi kuharibu Morali ya kazi kwa siku nzima. Baada ya hapo atataka akale kwanza, ndio arudi kuanza kazi. Muda mwingi anatumia kwenye mambo yasiyo na msingi. Tajiri akifika atajipa kuchangamka, atakunywa kahawa huku anaendelea na kusoma emails, Barua zilizoko mezani, kuangalia diary kama kuna appointment leo. Anajipa positive energy.
7. TAJIRI ANAWEKEZA AKIBA (SAVINGS), MASIKINI ANAKULA AKIBA.
Kile ambacho masikini anafanya kwa msimu, Tajiri anafanya kila siku. Masikini huweka akiba akipata hela nyingi wakati kwa Tajiri kuweka akiba ni tabia. Hata kwenye kidogo
Akiba itatolewa.
Kwa kuangalia tu haya kwa uchache utaona tofauti sio connection sijui ukoo ila shida ni kwenye mfumo wa fikra zetu. Tajiri akipata wazo atakomaa nalo mpaka aone likitokea kuwa kitu halisi. Masikini hata kuandika mawazo yake anaona ni ukichaa au kurukwa na akili.
Masikini anafanya jambo huku ameshajiaminisha kuwa halitakaa lifanikiwe, wakati tajiri anafanya akiamini matokeo chanya. Moja kwa moja hawa watu wanapishana hata kwenye Lugha zao. Masikini ukimuuliza vipi maisha atakwambia "Tupo tunahangaika tu, hali ngumu" Tajiri atakwambia "Mungu anasaidia" hata kama hali ni ngumu bado anajipa matumaini.
HAKUNA ALIYEZALIWA TAJIRI, AMUA KUHAMA HICHO KITUO LEO. BADILI FIKRA NA BADILI MTAZAMO. HATA WEWE UNAWEZA KUTAJIRIKA NA KUISHI MAISHA YA UHURU WA KIFEDHA. NAISHIA HAPA KWA LEO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment