Muda mfupi baada ta Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kuagiza Jeshi la Polisi kumwachia msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego na kuelezea kuwa nyimbo yake ya Wapo hata Rais Magufuli anaipenda ila anataka pia azungumzie mambo mengine ikiwepo kuhusu wanaokwepa kodi.
Baada ya hatua hiyo, aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amepongeza uamuzi huo wa Rais Magufuli ambao umetolewa kwa umma na Dk. Mwakyembe.
Nape ametoa pongezi zake kupitia akaunti yake ya Twitter kwa kuandika,
” Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!”
No comments:
Post a Comment