Friday, 10 March 2017

MNAPENDA MAMBO YA UDAKU NA MAPENZI HAYA SOMENI HIII


Wanandoa wapya waliooana muda si
mrefu,
waliishi maisha ya kimasikini sana.Siku
moja mume akamuita mke wake akamwambia''mke
wangu naondoka naenda safari ya
mbali,kwenda
kutafuta mali ili tuje tuishi maisha ya
furaha na raha ila sijui nikiondoka
nitakaa huko miaka mingapi.Nakuomba mke wangu uwe
mwaminifu
usinisaliti na mimi pia huko niendako
nitakuwa mwaminifu sitakusaliti''.Mke
alikubali na mume
akaondoka akaanza kutembea.Alitembea kwa siku
nyingi sana hatimaye akafika kwa
mkulima mmoja aliyekuwa anatafuta mtu
wa kumsaidia
kufanya kazi katika shamba lake.Yule
kijana akaomba kazi akapata ila akamwambia
yule mkulima''nitafanya kazi ila mshahara
wangu utakuwa unanitunzia mpaka siku
nikitaka
kuondoka nitakuambia unipe hizo pesa
zangu zote nilizofanya kazi kwako.Yule mkulima
akakubali ombi la yule kijana.Kijana
akafanya ile kazi kwa miaka ishirini,na
siku moja
akamwambia
boss wake kwamba ataondoka hivyo ampe pesa zake zote.Yule mkulima
akasema sawa
ila nitakupa mambo mawili uchague
moja.Mkulima
akasema 1.nikupe pesa zako zote
uondoke au 2.nikupe ushauri wa aina tatu afu
nisikupe pesa zako zote ulizofanya kazi
kwangu kwa
kipindi
chote cha miaka ishirini.Lakini sitaki
unipe jibu sasa hivi katafakari afu kesho utanipa
jibu umechagua kipi.Yule Jamaa akakaa
akatafakari,kesho yake akaja na
jibu.Boss
akauliza unataka kipi?Yule jamaa
akasema nipe huo ushauri wa aina tatu.Boss akarudia
tena
''nikikupa huo ushauri ujue sitakupa pesa
zako
ulizofanya kazi kwangu.Yule jamaa
akasema sawa ww nipe huo ushauri.Yule Boss
mkulima
akasema
i.usifanye mambo kimkato na usipende
njia za mkato.
ii.usipende kudadisidadisi na kushangashangaa mambo yasiyokuhusu
mana kuna mambo
mengine ni mabaya ukiyadadisi na
kuyashangaa sana yatakupelekea kifo.
iii.usifanye maamuzi wakati unahasira au
unauchungu. Baada ya hayo yule Boss akamwambia
haya
kijana wangu unaweza kuondoka,shika
hii mikate
mitatu hii miwili utakula wewe
mwenyewe ukiwa njiani kurudi nyumbani na huu mmoja
utakula na
mke wako siku ukifika nyumbani.Jamaa
akachukua ile mikate akaanza
safari.Mara
akakutana na mzee mmoja akamwambia''kijana umepitia hii njia?hii
njia ni ndefu sana
unaweza kumaliza mwezi hujafika hivyo
pitia hii
njia ya
mkato utafika haraka.Jamaa akakubali akaanza kutembea kupitia ile njia ya
mkato,mara
akakumbuka ushauri wa kwanza
aliopewa.Akaamua kurudi tena kwenye
njia ya
awali ile ndefu Baadae akaja kugundua ile njia ya mkato ilikuwa na waasi
waliokuwa
wanaua yeyote na kumteka akipitia hiyo
njia.Akatembea
kwa
muda mrefu akachoka akaona nyumba ya wageni akalipia pesa
akaoga
afu akalala.Usiku akasikia makelele sana
akaamka ili akaangalie kuna nini,wakati
anataka
kufungua mlango akakumbuka ushauri wa pili,jamaa akarudi akalala
zake.Asubuhi
mwenye gest akamuuliza vipi hukusikia
makelele
usiku?
Jamaa akasema alisikia ila sikutaka kufatilia sana yasiyonihusu.Mwenye
nyumba akasema
wewe ni mtu wa pekee kutoka salama
mana hapa
huwa
kuna mtu anatoka usiku anapiga kelele na yeyote anayetoka nje kushangaa na
kutaka
kujua nini kinaendelea huwa anauawa
na yule mtu
na
kuzikwa kwenye uwanja ule.Jamaa akaendelea na safari na baada ya safari
ya siku nyingi
usiku na mchana akafika nyumbani
kwake kwake
usiku na
mke wake alikuwa amelala.Alipoch ungulia kwenye ufa akaona kuna mtu
mwingine wa kiume
amelala pembeni.Jamaa alipatwa na
hasira na
ghadhabu
akataka aingie awaue mke wake pamoja na yule mwanaume mwingine
aliyekuwepo ndani
afu yeye arudi akafanye kazi kwa boss
wake.Lakini
kabla
hajafanya hivyo akakumbuka ushauri wa tatu akaamua kwanza.Akagonga mlango
mke
wake akafungua,mke alifurahi sana
akamkumbatia
mume wake.Lakini mke alimsukuma yule
mwanamke na kumwambia''kwanini umenisaliti?''mke akasema sijakusaliti
mume wangu toka uondoke.Jamaa
akasema
vipi na yule
mwanaume ndani ni nani?.Mke akasema
huyo ni mtoto wako ulipoondoka nilikuja kugundua kuwa nina ujauzito ndio
nikamzaa huyu
mtoto.Wote
walifurahi sana na baadae mke
akaandaa chai ndipo mume akauchukua
ule mkate wa tatu aliopewa na boss.Baada ya sara
aliumega mara
akakuta kitita cha pesa nyingi
sana,zilizidi hata
zile alizostahili kulipwa baada ya kufanya
kazi miaka ishirini.MUNGU WETU YUKO KAMA HUYU
BOSS,WAKATI MWINGINE ANAPOTAKA
KUJITOA
SADAKA,ANATAKA ATUPE VITU ZAIDI
YA VILE TUNAVYOJITOA,ANATAKA
TUWE NA HEKIMA ZA KIMUNGU PAMOJA NA BARAKA ZA
MWILINI.MUNGU ANATUWAZIA MEMA
SIKU
ZOTE.
LIKE PAGE NA PIA  SHARE NAWENGINE WAJIFUNZE.

No comments:

Post a Comment