Friday, 3 March 2017

MAKONDA NI SHUJUA ANAPASWA KUPEWA CHEO KIKUBWA ZAIDI YA ALICHO NACHO

Katika wanasiasa vijana mashujaa kabisa tangu Tanzania ipate uhuru mkuu wa mkoa wa Dsm Mh Makonda ameingia katika kundi hilo

Hakuna vita kubwa na mbaya kabisa duniani kama vita ya kupambana na wauzaji wa madawa ya kulevya. Hata marekani na nchi nyingi za dunia hii yeyote anayekuwa mstari wa mbele katika hii vita hawezi kutoka salama
Ni lazima apate hizi figisu figisu hata waziri wa sheria mh Mwakyembe  alisema kuwa huwezi kutoka salama katika hii vita yeye mwenyewe anasema aliona ugumu wake

Viongozi wote waliopita hapa Tanzania hakuna aliyejitokeza hadharani kupambana na madwa ya kulevya wote walikuwa wanapiga mikwara mikwara tu. Hata Marehemu Amina Chifupa alipiga mkwara sikumbuki kama ameshawahi kutaja hata mtu mmoja
Makonda ameweza amewataja hadharani na wote waliotajwa sio wageni katika masikio ya watanzania. Makonda ni shupavu sana tena sana ni shujaa kuliko hata kinjekitile, Makonda anastahili Tuzo ya heshima katika hii nchi

KUHUSU VYETI
Mimi nadhani haya yote yamekuja baada ya hii vita yake na wauzaji wa madawa ya kulevya
Kama kweli walikuwa wanajua anatumia vyeti ambavyo sio vyake kwanin wasingeyaleta haya tangu akiwa Dc kinondoni?kwa hiyo wamejua makonda anatumia majina yasio yake baada ya kutaja wauzaji madawa ya kulevya.?
Mimi naomba wasitutoe kweli reli hii ya kupambana na madawa ya kulevya tunajua ni biashara yenye utajiri mkubwa sana lakini ni lazima hii biashara ipigwe vita

Wapinzani walikuja na kauli eti wanachafuliwa majina. Hivi hawa watu mbona wanasahau mapema sana? Walivyowataja mafisadi katika ile list yao walioiita LIST OF SHAME hawakujua kuwa wanachafua majina?waliwataja viongoz wakubwa wa serikali kuwa ni mafisadi akiwemo Lowasa ambaye leo hii yupo kwao uko
Na kama lowasa anajua kuwa katika watu waliosababisha akose sifa za kupewa nafasi ndani ya ccm ni hao alionao sasa hivi

Gwajima anasema ana vyeti vya makonda vyote viwili amevipata wapi?.Je huyu mtu amepata wapi vyeti original vya mtu mwingine? Tunavyojua sisi Necta hawatoi vyeti mara mbili hata kama umepoteza. Hizi siasa sasa zimeingia adi makanisani ni hatari sana kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu..Siku hizi wachungaji wanafanya siasa makanisani nadhani wabadilishe usajiri wa makanisa yao wapewe usajiri wa chama cha siasa tu

ELIMU YA MAKONDA HATUNA SHIDA NAYO SISI
Hatuna shida na elimu ya makonda kabisa,Sisi shida yetu ni utendaji wake wa kazi tu.
Katika viongozi vijana wa awamu hii Rc Makonda amejitahidi sana tena sana amejituma sana kuhakikisha wananchi wa mkoa wake wanakuwa na utawala bora
Makonda alifanya ziara mkoa mzima kuangalia na kutatua kero za wanannchi wake, Kuna wabunge toka walipochaguliwa adi leo hii hawajarudi majimboni wapo wanakula starehe tu Dsm.Kijana huyu ni zaidi ya wabunge wengi sana hapa Tanzania lazima watu wamchukie kwa wivu wao hasa wanasiasa
Makonda anachukiwa kwa sababu ya kujituma kwake na sio kitu kingine
Makonda huyu huyu amesaidia kujengwa kwa wodi ya wazazi ya kisasa kabisa hapo Dar es salaam na wodi hiyo itawahudumia mama zetu na dada zetu sisi masikini hawa wanasiasa wana hospitali zao
Hawa mishahara yao ni mikubwa sana inafika adi milioni 18 kwa mwezi hawawez kuleta wake zao katika hizi hospitali za serikali
Hawa wanasiasa wanaojiita wasomi ndio wamearibu hii nchi adi kufika hapa
Kwani kwenye ufisadi wa escrow, richmond na huu wa nssf si hawa hawa wasomi wenye vyeti karibia kumi ndio wameshiriki?
Kwanini mnamchukia mtu kwa sababu ya kazi yake? Kwa sababu kwa kujituma kwake?
Makonda anachukiwa na wanasiasa wengi sana kutoka ndani ya chama chake adi nje ya chama chake na yote haya ni kwa sababu ya wivu tu hakuna kingine

Watanzania tunaitaji mtu atakayejitolea kwa dhati kusaidia wananchi bila kujali vyeti vyake au dini yake.Hata kama makonda anatumia vyeti ambavyo sio vyake hiyo haina maana hawezi kazi  tumeshampima tumeona kazi yake ni zaidi ya maprofesa
Wabunge wangapi wana P.hd na wengine wana masters na maprofesa lakini wameshindwa kutatua kero za watanzania.?
Hawa hawa wasomi wetu waliopo bungeni ndio wamepitisha sheria ya makato ya mikopo kwa wanufaikaji wa elimu ya juu adi kufikia 15%
Hakuna hata mmoja aliyejua kuwa hii ni kinyume na mkataba wa bodi na wanachuo

Tumeona adi bunge likaamua kuacha kujadili maswala mbali mbali ya kitaifa kuanza kumjadili makonda yaani tulishangaa kuwa hawa wabunge wamepatwa nani?
Baada ya muda siri zinafichuka kuwa mtu mmoja mdogo sana alitoka dar kwenda dodoma kubadilisha upepo wa bunge na akafanikiwa
Wabunge walimsema wengine adi kumtukana kuwa hana marinda kisa tu hii vita ya madawa ya kulevya

MY TAKE

Mh Rais nakuomba

Kwa dhati kabisa kuwa usitengua wadhifa wa mkuu wa mkoa wa Dsm Mh Makonda maana ndio vijana wanaothubutu na kujitolea kwa sababu ya taifa lake
Wakina Makonda mtaani wapo wachache sana wengi waliobaki ni wabeba mikoba na magazeti ya wanasiasa
Makonda anastahili nafasi kubwa zaidi ya ukuu wa mkoa kama inawezekana mpe hiyo nafasi haraka sana  maana anafaa sasa kuwa mtumishi wa watanzania wote na sio dsm tu
Hizo kelele zote ni kwasababu ya vita ya madawa ya kulevya pamoja na wivu wa wanasiasa juu ya makonda

NDIMI
RAPHAEL LUKINDO

No comments:

Post a Comment