Thursday, 16 February 2017
UFAFANUZI - Kuhusu Kufutwa Vituo vya Huduma za VVU na UKIMW
1. Ifahamike kuwa tuna Vituo vya Kutoa huduma za VVU na UKIMWI takribani 4,737 katika ngazi na Halmashauri mbalimbali nchini. Hivi vinaendelea kutoa huduma ikiwa ni pamoja na huduma za kitabibu (Bio-Medical interventions); Huduma za mabadiliko ya Kitabia (Behavioural Interventions) na Huduma za kuwajengea utengamano na za kiuchumi kwa wenye maambukizi ya VVU.
2. Tumefuta Utaratibu wa kutoa huduma za VVU na UKIMWI kwa Makundi Maalum kupitia Vituo Maalum (Drop In Centres). Na Vituo hivi havizidi 40 nchi nzima. Huduma zitatolewa katika Vituo vya kutolea Huduma za afya. Na pale itakapolazimu huduma za mkoba (Outreach services) kwa kutumia watoa huduma za afya itatolewa.
Serikali imeweza kupata ushahidi wa kina kuwa Vituo hivi vingi (Drop In Centres) vimekuwa vikitumika kuraghibisha (promote) vitendo vya mapenzi ya Jinsia moja, jambo ambalo ni kinyume na Sheria za Nchi.
4. Nimeagiza Mamlaka zote za Utoaji huduma za Afya kuhakikisha Huduma za VVU na UKIMWI zinapatikana kwa mtu yoyote nchini bila Ubaguzi wa aina yoyote kwa kuwa ubaguzi katika utoaji wa huduma za afya ni kinyume cha Sheria na Sera za nchi. Aidha tutahakikisha Watumishi wanapatiwa mafunzo ya ziada katika utoaji huduma rafiki kwa makundi maalum.
5. Bado tuna nafasi ya kupanua huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya kutolea huduma za Afya takribani 3000 nchini ambavyo mpaka sasa havina huduma za VVU na UKIMWI. Tunawaomba Wadau wetu tushirikiane ktk kuhakikisha Vituo hivi vinafanya kazi badala ya kujikita kwenye hizi Drop In Centres chache. Muhimu tujenge uweze wa Taasisi rasmi na sio hizi za muda.
Ummy Mwalimu
WAMJW
16 Feb. 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment