KUJITAMBUA ni uwezo au uelewa wa mtu binafsi kung'amua yeye ni nani anapaswa kufanya nini kwa sababu ipi? lini? Ili iweje na kwa mkadha upi.
Hiyo ndio maana ya kujitambua lakini bwana Greenberg na wenzake anaelezea aina kuu tano za kujitambua ambazo ni kama zifuatazo :
1:Kujitambua kwa mtu binafsi, Huku ni kujitambua kunakozungumzia taarifa za mtu binafsi na jinsi anavyotunza kuhusiana na yeye mwenyewe, mchango wake au kazi yake ktk jamii au katika kikundi. 2:Kujitambua rasmi au kujitambua kwa asili. Huku ni kujitambua kwa mtu kwa hisia za ujumla juu ya akina nani wanakuzunguka na wanaitwaje na wapo kwa ajili ya nini ukiijua vyema aina hii hupelekea interaction katika jamii uliyopo . 3: Kujitambua kwa ngazi ya kijamii , Kujitambua kwa namna hii huhusisha taarifa ambazo mtu anazitunza juu ya watu wengine katika jamii na mazungumzo yao ktkt jamii kwa njia ya kuangalia kusikiliza na kuona juu ya kinachoendelea ktk jamii. 4: Kujitambua kwa kikundi au kwa muundo wa kundi, Huku kujitambua kunahusisha maarifa juu ya watu na vitu wanavyo vifanya, wajibu wao ktk jamii na nafasi zao ktk uongozi na wanachokifanya ktk jamii na mipango yao ambayo ni endelevu ktk hiyo jamii. 5: Kujitambua kwa mtu kazini alipo / Ofisini au kujitambua kwa mtu ktk kazi yake anayoifanya, Kujitambua huku ni kule kujitambua kunakohusisha uwepo wa Mfanyakazi ktk kituo cha kazi na nini Mfanyakazi anafanya kwa wakat huo na jinsi alivyo na mahusiano na waganyakazi wengne na mawasiliano yake na wengne awapo kazini pia huhusisha ujuzi wa wengine wawapo kazini na nini wanafanya na nini watafanya kwa baadae na wapi watayafanyia hayo ambayo wameyatambua yakuwa watayafanya kwa baadae.
🌷VIASHIRIA VITAKAVYOKUPELEKEA KUJUA YAKUWA UMEJITAMBUA AU KUKUFANYA UJUE YAKUWA HUYU MTU AMEJITAMBUA
Viashiria hvyo vimegawanyika ktk sehemu kuu tatu ambazo n MAZINGIRA ADUI ZAKO NA YA MWISHO NI WEWE fuatana nami kuvielewa viashiria hvi ambavyo ukivitumia na kuvitambua ktk maisha yako vitakusaidia kufika ktk mafanikio yako kwa kiwango cha huu na kiashiria cha kwanza ni
👉WEWE yaani wewe mwenyewe unatakiwa kujijua wewe mwenyewe uwezo wako au nguvu zako mapungufu yako au madhaifu yako utu wako your motivations kujitambua huku kunaendeleza ujuzi wako ulionao yapi n madhaifu na upi n uwezo wako juu ya kitu ukifanyacho
👉��MAZINGIRA ULIYOPO AU YANAYOKUZUNGUKA
Kiadhiria hiki hujionesha kupitia makundi ya watu mnaifanya nao kazi pamoja kwa pamoja kwa ajili ya kushindania au kutimiza jambo flani huvyo jizoeshe kujenga akilini mwako maswali yafuatayo na ujiulize mwenyewe akilini mwako Mara kwa Mara na maswali hayo ni haya: a) Ili niyatimize haya nini nizingatie ? b)Je kunauhusiano wowote ambao unatakiwa kuendelezwa ? Au kuondolewa? c) Nifanye nn au nifanyaje ili nifike ktk mafanikio Yangu au nifike ktk mafanikio Yangu je kuna njia nyingine yeyote yakipekee ambayoitanifanya nifanikiwe ? 👉ADUI ZAKO katika kiashiria hiki cha kujitambua Hapa adui yako si elimu waliyonayo au uliyonayo au usomi lahasha ila unatakiwa kujua uwezo au uimara na udhaifu wa wengine juu ya nafasi ukiyonayo au uliyopo na ujue watu gani unashindana nao na pia Utajilinganishaje na unaoshindana nao nn kinakufanya wewe na wenzio muwe tofauti na wengine ? Ambacho kinakufanya uweze kufika ktk mafanikio .Hivyo ndivyo viashiria vya kukufanya ujue yakuwa umejitambua na kwa juyafanya na kuyafuata hayo itakusaidia kufikia ktk malengo na mafanikio yako.
UMUHIMU WA KUJITAMBUA
🌷Husaidia kujenga imani katika mambo mbalimbali uyafanyayo ktk maisha ya kila siku.
🌷Husaidia lakini pia ni kiashiria cha mafanikio katika ufaulu mkubwa wa mambo mbalimbali uyafanyayo
🌷Husaidia kujenga ujuzi na unapojenga ujuzi unajua nini cha kufanya siku zote za maisha yako na uanzie wapi umalizie wapi. 🌷Inakusaidia kukupa taarifa juu ya kitu unachokifikiri kwa ajili ya baadae kwa muktadha wako mwenyewe .
🌷Husaidia kumfanya MTU awe makini ktk mambo take yote ayafanyayo au juu ya mambo yote ayafanyayo ktk maisha yake ya kila siku .Asante By Yustin William Sanga

No comments:
Post a Comment