Friday, 10 February 2017

MBOWE:MAKONDA AMECHAFUA JINA LANGU,NITAMSHITAKI

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe 

Dodoma. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatafika polisi kwa kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mbowe amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kama utaratibu wa kisheria utafuatwa.                     

“Makonda hana mamlaka ya kumpa wito mtu kwenda polisi kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa,”amesema Mbowe.

“Makonda amemchafulia jina langu, chama, familia na upinzani.”                     

Mbowe ni mmoja kati ya watu 65 waliotakiwa na Makonda kufika kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.


Lakini pia kwenye ukarasa wake wa Instagram Mh.Mbowe ameyaandika haya
       RC hana mamlaka ya kisheria ya kumuita mtu Polisi, nitamfungulia mashtaka ya kunichafulia jina langu kwa kunihusisha na biashara ya dawa za kulevya, nipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote endapo njia sahihi zitatumika. Sisi kama Chama tunaunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Serikali imechelewa kuendesha vita, CHADEMA na Kambi ya Upinzani kwa ujumla haiungi mkono mapambano hayo yanayoendeshwa kwa hila. RC anachofanya ni kuwaepusha watuhumiwa wa dawa za kulevya na mkono wa sheria.

No comments:

Post a Comment