Tuesday, 28 February 2017
JIFUNZE NAMNA YA KUULINDA MOYO WAKO NA KUUTOA KWENYE MAANGAMIZO
✍ *MWL MWAKATWILA*
Bwana Yesu asifiwe sana.. Karibu tena katika kipindi cha leo darasani
Tusogee mbele tuliangalie jambo lingine katika mambo mengi unayotakiwa uyajue ambayo adui anaweza kuyatumia katika kuushambulia moyo wako nalo ni hili.
*ANAWEZA KUUSHAMBULIA MOYO WAKO KWA KUTUMIA MACHO*
Sikiliza. Moja ya siraha ambayo shetani anaitumika kuushambulia moyo ni macho ya mwanadamu. Shetani hutumia sana ujinga wetu wa kutokujua namna ya nguvu iliyopo kwenye macho yetu haya ili kuharibu moyo wa mtu. Angalia mistari hii utanielewa haraka ninasema kitu gani. "Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?.......Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;"(Ayubu 31:1 Na 7)
Ukiipitia hiyo mistari utaona kitu cha ajabu sana. Ayubu anafunga agano na macho yake, sikia, hafungi agano na Mungu au kitu kingine anafunga agano na macho yake. Neno agano maana yake ni patano maalumu lililowekwa kwa kufuata utaratibu maalumu. Au unaweza kusema ni mkataba maalumu ulio na utaratibu maalumu unaokubarika kwa kila aliyeko ndani ya huo mkataba.
Ayubu hapo anatuambia aliweka mkataba au patano maalumu na macho yake. Yaani kulikua na patano kati ya Ayubu na macho yake katika suala zima la kutazama au kuona kwa Ayubu. Kuna mamboy ambayo macho hayakutakiwa kufanya na kuna mambo ambayo Ayubu hakutakiwa kufanya. Angalia anasema WALIPATANA KUTOKUANGALIA MSICHANA!!!
Umesikia hiyo? Ayubu alifunga hilo agano kabisaaa na macho yake. Na inaonekana macho yalijua Mtu yaani Ayubu na macho wana patano hakuna ruhusa ya kumuangalia msichana!!! Unaweza kusema inawezekanaje hapo?
Angalia huo mstari wa saba. Utagundua agano lao lilijengwa kwa namna hii. Ebu tazama kwanza huu mstari wa saba unasema hivi. "Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu" Ukiangalia hapo unaona moyo unaweza kabisa *KUYAANDAMA MACHO AU KUYAFUATA MACHO YANATAKA NINI*.
Ayubu alifunga agano na macho yake kuwa si kila kitu macho yataona basi moyo wa Ayubu uyaandame hayo macho yameona. Unajua shetani leo hii anajua kuwa macho ya mwanadamu yanaweza kabisa *YAKAUVUTA MOYO WA HUYO MTU KUFANYA KILE MACHO YANATAKA*. Mungu anapotuambia linda sana moyo wako anajua kabisa kuwa moyo wako unaweza kabisa ukayafuata macho yanataka ninini.
Ndiyo maana nakwambia watu wengi kwa kutokujua kuwa kuna nguvu ya ajabu kwenye macho ambayo inaweza kuufanya moyo wa mtu UTII KABISAA KILE MACHO YAMEONA.Ngoja nikuambie kitu hiki, Sehemu zingine Mungu anatuonya anasema hivi. "Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia."(1Yohana 2:16). Ebu ludia ludia kuisoma hiyo mistari, utagundua kuwa macho kama macho YANAWEZA TENGENEZA TAMAA YAKE. Haiitwi tamaa ya mwili inaitwa tamaa ya macho.HAPO UNAONA MACHO YANAWEZA KUTENGENEZA TAMAA YAKE KABISAAA WALA SI MWILI.
Ukiipitia hiyo mistari ndiyo utajua kwanini Ayubu aliweka Agano na macho yake hakuweka hapo agano na mwili. Alijua kuwa macho yanauwezo wa kuitengeneza tabia mbaya kabisa hata mwili usiwe na habari macho yanafanya nini!!!
Ngoja nikupe mfano huu. Sikiliza, MACHO YAKITAZAMA MSICHANA NA MTU MWENYE HAYO MACHO AKIKUBALIANA NA HICHO MACHO IMEKIONA CHA KUMTAZAMA MSICHANA. NA MOYO WA MTU HUYO UKAVUTWA UYATENDE HAYO MACHO YAMETAZAMA NA MACHO YAKAACHIA MFUMO WA TAMAAYAKE NDIYO HAPOO UNAONA MTU YAANI ROHO ANAZINI MOYONI WAKATI MWILI HAUNA HABARI. Sijui unanielewa?
Mwili unaweza ukawa umekufa ganzi lakini macho yakiwa yanaona na yakatamani nakuambia ukweli akili zako huko moyoni zinaweza kufanya kitu na macho kabisaa.
Watu wanaozini moyoni MWILI HUU HUWAHAUPO KWENYE TUKIO ILA MACHO YALIYOONA NA MOYO WENYE MAWAZO FIKRA KUTAFAKARI NK NDIYO VINATUMIKA AU UIFANYA HIYO HUDUMA!!!. Unaposoma maandiko unaona macho yakitu cha ziada ingawa yapo kwenye mwili, katika ulimwengu wa roho macho yanaweza fanya mambo kwa kujitegemea kabisaaa. Ni sehemu ya mwili ila kuna makubwa yapo kwenye macho.
Adui akijua wewe hujui kwenye macho kuna nguvu gani. Anaweza kuyatumia macho yako hayo ili kuushambulia moyo wako na akauharibu kabisaa. Ngoja nikuonyeshe mfano mwingi uone hiki ninacho kuambi Angalia mistari hii." Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake...... Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;......Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani."(Mithali 6:12-13 na 16-18 na 25-26).
Ukiipitia hiyo mistari utagundua macho kama macho yanaweza kabisaa kutengeneza uharibifu mkubwa kwa mtu. Angalia macho yanaweza kubeba kiburi, hasemi kiburi moyoni anasema macho yenye kiburi. Angalia hapo macho yaweza kutumika kuinasa nafsi ya mtu mwingine. Macho hapo ndiyo yaliyotumika kumvutia huyo mwanaume(KUMNASA) na akajikuta kanasika. Sikiliza Kilichokua kikitafutwa ni nafsi ya huyo mtu, macho ndiyo yaliyotumika kumkamatia. HASEMI MWILI ANASEMA MACHO
Maandiko yanasema macho yalitumika kukonyeza!!!! Konyeza hiyo inaonekana ilikua ni konyeza mbaya mpaka Mungu aliikasirikia. Ninachotaka nikuonyeshe ni hiki. Macho yako yanaweza kutumika kuiangamiza nafsi yako au hata nafsi za watu wengine. Maandiko yanaposema linda sana moyo wako, lazima ujue mfumo mzima wa silaha zinazo weza kutumika kuipigia hiyo mioyo moja kombora ni macho yako au macho ya mtu mwingine.
Kuna watu wengine wanaelimu ya kujua mambo kwa kupitia macho ya hao watu tu. Wapo, wa kiangalia macho yako tu, wanajua kuwa huyu, mwizi, huyu, mwongo, huyu, anashida, huyu, mzinzi.Nk. Wanayajua hayo kwa kutumia macho yao yakikutana na macho ya wengine. Nimewahi kwenda nchi moja ya Kiafrika. Sasa sikia, tulipofika sehemu moja tulikuta kuna kituocha ukaguzi barabarani. Niliona askari kaingia mle ndani ya basi. Lina abiria kama hamsini hivi. Yule askari alitaza sura za watu wote. Baadaye akaninyooshea mimi kidole akaniliza wewe lete pasipoti yako!!! Akawauliza na watu wengi wawili hivi. Kweli alipatia sisi wote tulikua wageni nchini mle. Ila watu tuliomo mule wote ni weusi. Macho yanguvu ya ajabu sana.
Unajua kuna watu Mungu amewapa macho ya aina furani akikutazama tu hivi wewe mwenyewe unaanza kumwambia uliiba wapi, utafikiri kakuona mpaka moyoni kumbe ni macho yake tu. Alikua hajui chochote. Haujawahi kutana na watu wa namna hii? Miaka furani niliwahi kukutana na mtoto mmoja anamacho ya ajabu. Ni makali makubwa meupeee!! Akikuangalia hivi mimi nakwambia huwezi kuwa na ujasiri wa kuangaliana naye, na alikua mtoto sijui akiwa mtu mzima itakuaje.
Nikamsimulia mke wangu kuwa leo nimekutana na mtoto mmoja yuko hivi na hivi. Mke wangu akaniambia namfahamu. Nikamwambia anamacho ya ajabu. Mke wangu akanikubalia ni kweli. Sasa macho kama macho adui anaweza kuweka pepo hapo ukashangaaa kila unayemtazama mkikutana macho tu ANAKUTAKA hapo haijalishi ni mwanamke au mwanaume.
Watu wengi hawajiulizi kuna nini machoni kwangu? Haujawahi wasikia watu wanasema, nilimpiga jicho moja tu kwishaaa!! Mungu anaposema mwanangu hakikisha hakunasi kwa kope za macho yake yaani anataka kukufundisha kuwa macho yanaweza kuwa kombora la kuiangamiza nafsi yako. Au hayo macho yako yakawa kombora analolitumia shetani kuwaangamiza wengine.
Ngoja nikuchekeshe, niliwahi kuwa na rafiki yangu, yule ndugu alikua na sura na macho ya ajabu sana. YAANI ALIKUA MWANAUME SAWASAWA!!! bahati nzuri alikua huru sana, alijitambua anasura ya aina gani, siku moja nasimuliwa alikua anaenda sehemu, sasa aliongozana na mama mmoja ambaye alibeba mtoto mgongoni, sasa yule jamaa yangu yeye alijijua kuwa kuwa sura yake na macho yake yakoje, akawa anamtazama yule mtoto. Yule mtoto akaanza kulia.
Yule mama wa mtoto hakujua kuwa kuna mtu anamfuatia nyuma yake na ndiye anayemliza mtoto mgongoni. Kwasababu yule mtoto alipomuona huyo ndugu alianza kulia, yule mama alikazana kumlazimisha mtoto wake anyamaze la sivyo atamchampa bila kutazama nyuma.
Basi Nasikia yule mama akasimama akamuuuliza mtoto wake, wewe unalia nini? Mtoto akajibu Hiyooo!! Mama alipogeuka na kukutana na sura na macho yale yeye mwenyewe akapiga kelelee za kuogopa!!! YAPO MACHO NAKWAMBIA YAMEUMBWA KIAJABU NA MUNGU NA YANATISHA. Ngoja nikuchekeshe tena. KUTANA NA WATUMISHI WA NAMNA HIYO. Nakwambia Utatubu dhambi kabla hajakuambia neno nakwambia!!! Eheheeee.
NAMNA YA KUYASHUGHULIKIA MACHO YAKO ILI ADUI ASIPATE KUUPIGA MOYO WAKO KWA KUYATUMIA HAYO MACHO
ANZA KUFANYA MAOMBI MAALUMU YAHUSUYO MACHO YAKO AU YA MTU MWINGINE
Unaweza kusema nafanyaje hapo mtumishi ili nikabiliane na macho yangu yasitumike kuniangamiza moyoni mwangu. Au yasiangamize nafsi za wengine? Maandiko yanatupa maarifa yanasema hivi."Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako."(Zaburi 119:37).
Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa mfalme Daudi alijua kuwa macho yake yalikua yakitumiwa vibaya na adui, ALIKUA AKITAZAMA VISIVYOFAA. Yaani moyo wake uliambatana na macho yake yaliyokua yakitamani mabaya. Mfalme Daudi akaanza kufanya maombi maalumu. Maombi hayo yalikua maalumu kwa ajili ya kushughulikia macho yake. Aliomba Mungu amgeuze macho yake yaanze kuangalia vinavyofaa.
Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa Mungu anaweza kuyageuza macho ya mwanadamu na yakaanza kuangalia au kuchuja mabaya na mema na YAKAWA YANAPITISHA MAMBO MEMA ILI MOYO WA HUYO MTU UYAANDAMIE MAMBO MEMA.. Hata wewe leo hii unaweza kuanza kuomba maombi ya mfumo huo ili macho yako hayo yasitumike kuuharibu moyo wako.
Unajua ukianza kuyaombea hayo macho, utashangaa kutatokea badiliko kubwa kwenye eneo la KUTAZAMA KWAKO TUNAITA MAONO AU MFUMO MZIMA WA AKILI ZAKO. Si unajua kuwa macho ni mlango wa ufahamu wa mtu? Sasa ili ufahamu wako au akili uliowekwa ndani ya moyo uwe sawasawa lazima MACHO YAKO YASHUGHULIKIWE MNO.
Watu wengi hawaoni fursa zile ziletwazo mbele zao, hawaoni NJI ZA MAFANIKIO YAO, wanaona mabaya tuuuuu!!! Kwasababu macho yao hayajawa sawa. Ngoja nikuambie, mapepo yanaweza kukaa kwenye macho ya mtu, na yakasababisha ASIONE SAWASAWA NA ASIPOONA SAWASAWA TAYARI YANAKUA YAMEFANIKIWA KUUDHIBITI MOYO WAKE.
Yaani mfumo mzima wa mawazo yake, fikra zake, kutafakari kwake, ufahamu wake( akili) zinakua zimefungiwa ngomeni. Kuna masomo shetani hapendi watu wayasikie kabisaaa. Moja ya masomo ni kama hili. Adui anatafuta sana aone mfumo mzima wa akili za watoto wa Mungu unaharibiwa. Wameokoka sawa, lakini kwenye eneo la kuwaza kwao atahakikisha hawawazi vizuri. Na moja ya njia atakayoitumia kuwaondolea mawazo hayo ni kuziba na kuuharibu mlango unaopitisha mfumo mzima wa ufahamu wao yaani macho.
Anza kila mara kumuomba Mungu aanze kuyalinda, kuyageuza macho yako. Unaweza kusema mbona naona? Mimi nakwambia usishangae unaona kama mfalme Daudi alivyokua anaona njia zisizofaa tu. Maandiko yanasema hivi." Neno la BWANA likanijia tena, kusema, Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi."(Ezekiel 12:1-2)
Hao watu walipewa macho kabisaa, si vipofu, lakini Biblia inasema walikua hawaoni. Kama walikuwa hawaoni maana yake mfumo mzima wa maisha yao kiuchumi kiroho ulikua mbaya. Mioyo yao ilikosa kupokea mawazo mema(mimi nayaita mawazo ya Nuru) walipokea mawazo ya giza tu si hawaoni? Lakini kuna kitu cha kuangalia hapo, ni hiki walikua na macho lakini hawaoni. Sijui wewe ukoje? Usishangae huoni sawasawa!!! Anza kuomba Mungu ayageuze macho yako ili uanze kuona vyema.
Mtume Paulo alilijua sana jambo hili ndiyo maana katika maombi yake mengi alijua namna ya kuliombea kanisa kwa Mungu ili Mungu ashughulikie macho ya hao ndugu yatiwe nuru. "Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;"(Waefeso 1:17-19).
Macho yako hayo yanatakiwa yashughulikiwe ili moyo wako uliobeba mfumo wa akili hisia na utashi usichanganywe na macho ambayo ndiyo ufunguo wa ufahamu wa mtu. Ebu anza leo hii kufanya agano na macho yako kama Ayubu alivyofanya. YAAMBIE KILA MARA HAYO MACHO YAKO KWA KUPITIA MAOMBI NININI HUTAKI YAANGALIE. YAAMBIE MSIMAMO WAKO NI KUYAANDAMA YAFAAYO YALIYO YA MUNGU WALA SI YA DUNIA. YAAMBIE YANASIKIA!!! Fikiria yanaweza beba tamaa nk maana yake yaweza sikia kabisaaa.
Lazima uanze kuyaambia unanisikia? Usiseme nimeokoka, hakuna anayebishana na wewe katika kuokoka kwako, ninachotaka uwe mkamilifu moyoni mwako na ili uwe mkamilifu lazima ujifunze kumuomba Mungu Ayatengeneze macho yako hayohayo!!! Kemea kila nguvu ya pepo iliyoko kwenye macho yako au ya watoto wako nk. Usikubari adui ayatumie macho yako kuwatengenezea wengine anguko.
Unajua Mungu anao uwezo wa kuyatumia macho yako hayohayo uanze kuyaangalia mambo ya rohoni. Ngoja nikupe mfano huu mmoja wapo katika mambo mengi Mungu aliyonionyesha. Nakumbuka Siku moja nilikwenda kwenye kanisa furani, na ilikua ni siku ya alhamisi kuu, kesho yake ilikua ni siku ya ijumaa kuu. Siku hiyo nilipoingia mle ndani kulikua na watu wengi mno. Na ilikua ni siku ya meza ya Bwana. Sasa sikia. Nilipoingia mle ndani macho yangu haya yaliona watu wengi, watumishi wachungaji walikua wengi sana.
Sasa sikia tuliambiwa tusimame na ibada ifunguliwe kwa maombi. Kiongozi mkuu wa kanisa lile alianza kuomba, nilifumba macho. Ghafra, macho yangu yakafumbuliwa kwa nguvu. Si mimi niliyafumbua nilishangaa tu yamefumbuliwa. Unajua niliona watu wengi waliomo mle ndani tokea kichwani mpaka miguuni ni mifupa. Ni kama wafu waliokufa zamani na imebaki mifupa tu ila wanasema. Niliogopa sana nika kaa chini.
Unajua niliona watu waliona nyama hizi na wamevaa nguo walikua wachache sana. Kanisa lile likijaa linabeba watu elfu sita niliambiwa. Sasa watu niliowaona ni watu wachache sana. Na wengi humo wameokoka lakini ndivyo nilivyoona. Baada ya kumaliza ibada ile, nilimuuliza Mungu nini maana ya maono yale. Alinifundisha hivi watu hao HAWANA UZIMA.
Alianza kunifundisha kuhusu maneno haya."Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu."(Yohana 5:25-29).
Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuna wafu wa aina mbili wametajwa, kuna wafu wasikiao SASA. Na kuna wafu watakaosikia wakiwa makaburini. Hao wafu wasikiao sasa ndiyo hao ambao niliwaona siku ile. Wakisikia neno la Mungu na kulishika watakua hai SASA. Ndiyo hao unaosikia hata wakifa kimwili bado wako hai maandiko yanasema HAWAFI. Ninachotaka kukufundisha hapo ni hiki macho yangu haya ndiyo yaliona waziwazi.
Anza kuombea macho yako hayo usishangae UTAONA HATA VILE WENZIO UKIWAAMBIA NAONA HAWEZI KUONA KWASABABU NI VIPOFU. Ila wanamacho. Unajua upo uwezekano wa kumuona msichana kwa uzuri tofauti nawengine wamuoanavyo msichana. Wewe chukua wanaume kumi waletee msichana yuko nusu uchi. Waulize unaona nini? Eheheee. Ni wachache macho yao YATAONA UTUKUFU WA MUNGU KWA HUYO MSICHANA!!! Macho ya watu wengi yamebeba tamaaa. Hawawezi kuona yafaayo, wataona mabaya tuuuuu!!
Fikiria kidogo, wewe umeokoka KWANINI UNAPATA SHIDA AKIPITA MWANAMKE? Lazima kama mwalimu niseme kitu, UKIONA UKO HIVYO FAHAMU KUNA TATIZO MACHONI PAKO. Ndiyo maana moyo wako unavutwa kwenye ubaya tuu. Unajua nikwambie maandiko yanasema tukikaa kwenye neno la Mungu tutawekwa huru kwelikweli. Huwezi niambia uko huru KAMA MACHO YAKO HAYAJAWEKWA SAWA NA MUNGU. Utapata shida sana. Na usishangae utaishi kitumwa kwelikweli.
Unajua maandiko yasemavyo ikimbieni zinaa, watu wengi hawamuulizi Mungu tunaikimbiaje zinaa? Angalia mfano. Mfalme Daudi alifanya uzinzi kwasababu macho yake yalimtazama mwanamke aogaye, macho yake yakabeba tamaa, akajikuta ameyaandamia macho yake. Akazini. Angalia mistari hii uone."2kawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho."(1Samweli 11:2)
Macho yake hayakua vizuri. Na moyo wake ukayaandamia yale mabaya ambayo macho yalipendezwa nayo. Unajua mfalme Daudi baadaye alikuja kugundua tatizo lake lilikua wapi. AKAANZA KUOMBA MUNGU AYASHUGHULIKIE MACHO YAKE. Aliombea mfumo mzima wa Macho yake ugeuzwe na Mungu.
Kama unataka leo hii uanze kuikwepa zinaa haukwepi kwa kufumbia macho wasichana. Unaanza kuikwepa kwa kujua ninini ufanye ili nguvu ya zinaa ISIKUPIGE MOYONI. Shughulikia mlango wa hiyo zinaa uko wapi utagundua unaanzia machoni NDIPO UNAPOTAKIWA UHAKIKISHE MUNGU ANAPATENGENEZA. Sikia Bwana Yesu ndiye fundi wa kushughulikia vipofu.
Nenda kwake mwambie BWANA MIMI NIKIPOFU SIONI MEMA NAONA MABAYA TUUUUUUU!!! Nikimuona msichana macho yangu hubeba tamaa mbaya. NAOMBA YAGEUZE NISIYAONE YASIYOFAA. Anza maombi ya Ameeen ameeen hiyo mara kwa mara. Utaona namna utakavyoanza kuukimbia uzinzi mapema kabisaaa.
Ngoja nizungumze na wewe. Wewe leo hii unataka umtumikie Mungu, umewahi jiuliza swali wateja wako wakubwa ni kina nani? Jibu zuri ni wanawake. Siyo siri, wanawake ndiyo watu wawajiao sana watumishi. Wanaume wengi hufa na tai zao shingoni. Hawana mpango wa kuombewa ombewa, shida zao wanafikiri wao pekee ndiyo mabingwa wa kuzimaliza kumbe hakuna lolote.
Sasa kama macho yako wewe mtumishi ni mabovu, utapata shida sana sana.!! Utajikuta unanajisika moyoni kila siku kwa kuwaangalia vibaya hao wanawake. ANZA LEO KUWEKA AGANO NA MACHO YAKO ILI YASITUMIKE KUKUHARIBIA MOYO WAKO.
Mungu akubariki sana
Wako
Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment