Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana. Ni imani yangu kuwa wewe ni mzima na umekua ukibarikiwa na somo hili tulilopewa na Mungu kwa wakati huu.
Ebu tusogee mbele kidogo. Baada ya kujifunza eneo la hofu kuwa ni silaha hatari ambayo adui anaweza kuitumia katika shambulizi la moyo wako. Ebu tuliangalie jambo lingine ambalo linaweza tumika katika kuiharibu nafsi yako kabisa. Kumbuka nilikufundisha mwanzo kabisa kuwa, Mungu anapotufundisha mimi na wewe tuhakikishe tunalinda mioyo yetu ni kwasababu ndani ya moyo Mungu ameweka mambo mengi sana ya thamani.
Msikilize asemavyo." Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima."(Mithali 4:20-23).
Ukiipitia hiyo mistari utaona wazi kuwa uzima wa aina yoyote umo ndani ya moyo. Na nilikufundisha kuwa Huko ndani ya moyo pia Mungu ameweka ndani ya huo moyo mfumo mzima wa akili yaani mawazo fikra kutafakari hisia na utashi vyote hivyo vimewekwa huko. Sasa shetani akitaka kukuvuruga kwenye mfumo mzima wa akili na uzima mwilini fahamu atatafuta njia mbalimbali za kuivuluga hiyo nafsi yako au moyo wako. Kitu kingine anachoweza kukitumia kuivuluga nafsi yako ni hii ANAWEZA KUTUMIA MAZINGIRA UNAYOISHI AU WATU WA KARIBU NA WEWE
Ukisoma maandiko matakatifu utagundua kuwa mtu aliyepewa moyo wenye akili, hisia, na utashi anaweza kuwa na akili au busara au hekima moyoni mwake kwa kutegemea mahali anapoishi au kwa kutegemea watu anao ambatana nao. Mazingira unayokutana nayo yanaweza kukubadilisha mtazamo au mawazo yako kabisaa kama haujawa makini.
Maandiko yanasems hivi."20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia."(Mithali 13:20). Sikiliza, hekima hukaa moyoni. Biblia inatufundisha kuwa Mungu akimpa mtu hekima eneo hekima itakakokwenda kukaa ni moyoni. Angalia mistari hii" Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza;"(Kutoka 31:6).
Sasa sikia nikufundishe. Maandiko yanatupa ufahamu kuwa unapoenda au unapoketi mahali penye mazingira ya watu wenye hekima au akili au mawazo mazuri fahamu ni rahisi wewe kujikuta moyoni mwako unakua na hekima au akili au maarifa, mawazo yako huko moyoni YATAKUA MAZURI. Maandiko yanasema ukiambatana na mpumbavu fahamu UTAUMIA..
Anaposema mpumbavu maana yake asiye na hekima moyoni au mtu asiye na mawazo mazuri yazaayo akili kubwa au nyingi.
Sasa sikia unaweza ukajikuta leo hii umeshambuliwa moyoni mwako na ukaumia kabisaa kwasababu ya mtu au watu unaoambatana nao au mazingira ya hapo mahali unapoishi panaweza kuwa kombora atakalolitumia shetani kuiumiza nafsi yako kabisa na ukajikuta unajeraha moyoni kabisa.
Ngoja nikupe mfano huu uone. Watu wengi sana leo hii HAWANA KITU KIPYA AU MAWAZO MAPYA MIOYONI MWAO KWA SABABU YA MAZINGIRA WANAYOISHI TU. Angalia mistari hii uone hiki ninachokuambia. " Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika."(Yeremia 48:11).
Ukiipitia hiyo mistari utaona kitu cha ajabu sana. Mungu anamzungumzia Moabu , amemtazama Moabu tokea ujana wake amemuona yuko vilevile HANA KITU KIPYA ANA HARUFU ILEILE. Yaani mawazo yake akili zake ni zile zile hazijabadilika. Mungu amegundua ni kwanini Moabu hana kitu kipya moyoni mwake ni MAZINGIRA ALIYOKULIA AU ANAYOISHI.
Huyo ndugu tokea amezaliwa hakuwahi kutoka mahali hapo, Mungu anasema huyo jamaa hata jela hajawahi kwenda!! Yupo hapo hapo hajifunzi kitu kipya anakutana navyo vitu vile vile alivyovizoea akutana na watu walewale wenye mawazo yaleyale.Mtu wa namna hawezi kuwa na maendeleo yoyote. Mtu wanamna hiyo hawezi kuwa na akili kubwa.
Ngoja nikuulize swali unafikiri huyo mtu anaweza kupata wazo zuri jipya? Umewahi kutana na wazee ambao walizoea maisha yale ya kipindi cha mwalimu na wanaishi leo hii? Umewahi kuongea nao? Umewahi kutana na mawazo yao?
Umewahi kukutana na watu waliozoelea miaka kumi ya utawala wa raisi aliyepita? Na bado wanaharufu ya maisha ya utawala uleeeeeee uliopita umewahi kuyasikia mawazo yao? Eheheee. Mimi nakwambia shetani anaweza KUKUFANYA UWE NA MAISHA FURANI YA NYUMAAAAAA WAKATI WENZIO WANAISHI MIAKA MINGINE KUMI YA UTAWALA MWINGINE. Kabisaaa!!!
Ukinielewa utaona kwanini hawa ndugu walikuwa watawala katika taifa la Israeli waangalie hawa watu."Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao."(1Nya12:32). Watu hao mioyo yao ilikuwa salama kweli, walikua na ufahamu au akili ya MAZINGIRA WALIYONAYO NA WALIJUA YAANI AKILI YA NINI KINATAKIWA KIFANYIKE KWA MAFANIKIO YAO KATIKA MAZINGIRA HAYO HAPO PAMEITA NYAKATI HIZO.Ufahamu wao wa kujua nyakati hizo ni nyakati gani ulikua mkubwa
Ukiangalia watu mia mbili tu ndiyo walikua vizuri mioyoni mwao, hao wengine adui aliishambulia mioyo yao akili zao hazikujua kitu kipya nini katika kipindi wanachokutana nacho na kwa kuwa walikua hawana wazo lolote lile hata utashi wao unakosa cha kutenda. Mpaka wapatikane watu wenye akili au ufahamu wa kujua katika mazingira haya watu wanatakiwa wafanye nini
Ngoja nikuonyeshe mfano huu labda utanielewa na maanisha nini. Katika nchi yetu watawala wana miaka mitano mitano ya kutawala na wengi wamebahatika kuwa na vipindi viwili yaani miaka kumi. Sasa angalia, utaona shetani anachofanya ni kuwashambulia watu ili WABAKI KWENYE UTAWALA ULIOPITA .Sikia,AKILI ZAO HAZIVUKI KUINGIA KATIKA MIAKA MINGINE KUMI WALIYONAYO SASA. Wengi wanakuja kushituka baada ya mtawala waliyenaye kuondoka madarakani. Ndiyo wanaanza kuziona fulsa walizoshindwa kuziona na kipindi hicho tayari wamekua wamechelewa.
Hivi haujawahi kusikia misemo hii WATU WANAMKUMBUKA MTAWALA ALIYEPITA? Na wamepita watawala wengi nchini utakuta mtu anamkumbuka yuleee wazamani analia na machozi, sikia UKIONA WATU WANAKUA NA TABIA HIYO FAHAMU BAADA YA MTAWALA ALIYEKO MADARAKANI KUONDOKA WATAMKUMBUKA NAYE NA WATALIA TUUUUUU!!!
Mazingira unayoishi adui anaweza kuyatumia kukuumiza kabisa. Ngoja nikupe mfano huu wa ajabu kidogo. Siku Moja nilikutana na rafiki yangu mmoja, tukawatunazungumza mambo mengi tu, moja ya jambo tulilolizungumzia ni namna ya watu waliona AKILI NYINGI WANAVYOWEZA KULOGWA NA MAZINGIRA WALIYONAYO NA WAKAJIKUTA HAWAZITUMII VEMA AKILI ZAO NA KWENYE JAMII WANAJIKUTA WAKO SAWASAWA NA WATU WENYE AKILI NDOGO
Unaweza kujiuliza swali hivi kuna watu wenye akili kubwa na ndogo?
Angalia mistari hii. "Aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu; Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake."(Mithali 17:18). Huyo mtu ukiangalia si kuwa hakua na akili, anazo ila anazo kwa kiwango kidogo ndiyo maana anasema aliyepungukiwa. Neno kupungua maana yake hazipo kwa kiwango kilichotakiwa ambacho ni kuwa nazo nyingi.
Adui anaweza kuishambulia nafsi iliyo na akili kwa kiwango kikubwa kwa kuitengenezea mfumo wa mazingira ya akili hiyo isitumike kwa kiwango kile ilitakiwa itumike. Na ukiona mwenye akili hana uwezo wa kuzitumia akili zake vema au kwa kiwango kile alichonacho fahamu moyo wake umepigwa. Yaani adui kainua kijiinuacho na kuifungia ngome akili kubwa ya huyo mtu mwenye akili.
Ngoja nikupe mfano huu. Ebu wewe kaa tafakari uone mazingira yanavyowabana wasomi wengi utaona hata usomi wao hauna faida kwao na hata kwa jamii. Utawakuta watu ni maprofesa watu hawa mimi nawaita wabunifu na wataalamu waliobobea, nenda kaangalie wengi kazi wazifanyazo nikazi ambazo hawakustahili wao kuzifanya kabisaa. Mtu mtaalamu kama huyo unampa kazi ya kusaini makaratasi tuuuu!!! Hiyo kazi si hata mtoto wa darasa la saba anaweza kuifanya jamani? huyu mtu mbunifu mtaalamu kwanini asipewe nafasi ya kukifanya kile atakiwacho kufanya kutokana na uwezo mkubwa wa akili yake au UFAHAMU WAKE?
Wao walitakiwa wafanye kazi KUBWA kuliko hizo wazifanyazo. Ngoja nikuchekeshe utashangaa leo hii unasoma magazeti unakuta profesa anafanya mambo, anajadili mambo, hata mtoto wa darasa la saba hawezi fanya. Unajiuliza swali ninini kime mkuta huyu? Unakuja gundua ni mfumo wa mazingira anayoishi!!! Kama unafikiri nakutania wewe watumbukize hawa watu kwenye mazingira ya siasa utaona hiki ninachokuambia.
Huko wengi wanapoteza mno kiwango cha UJUZI MKUBWA WA AKILI YAO. AKILI YAO HAIFANYI KILE WALICHOTAKIWA WAKIFANYE. Wanajikuta wakifanya mambo mepesi mno. Wengine hata heshima yao hupotea kabisaaaa!!!!
Siku moja nilikua naangalia tv na nikawa naangalia bunge moja la nchi moja ya Afrika. Unajua siku ile niliona wabunge wale wakijadiliana mambo na kubishana kwa ugomvi kabisa. Hoja yenyewe ilihusu masuala ya mikopo, unajua nipokua nazisikiliza zile hoja zao na nilishangaa sana nilipokuja kugundua hao watu ni wasomi kwelikweli, huyo wanaemlaumu ni msomi kweli ni profesa.
Nilijiuliza maswali mengi sana. Moja ya swali lilikua hivi profesa anahitajika kweli awe msimamizi wa mikopo? Profesa? Kweli hakuna watu wanaoweza kuifanya hiyo kazi mpaka awe profesa? Swali lingine lililonikaa moyoni mwangu hivi kwanini huyu jamaa profesa aliikubalikuifanya hii kazi? Fikiria Huyu jamaa awe yeye anafuatilia nani kapewa mkopo nani hajapewa nani kaludisha mkopo nani hajaludisha Tunamdai, Eheheee!!!
Unajua Roho Mtakatifu alinifundisha kitu cha ajabu sana hapo. NILIONA NAMNA YA MFUMO WA MAZINGIRA TULIYONAYO AFRIKA YANAVYOWEZA KUZIBANA NAFSI ZA WATU AMBAO DUNIA INAWAHITAJI WAKAJIKUTA WAKIFANYA MAMBO AMBAYO HAWAKUSTAHILI WAYAFANYE KABISAA!!!
Shetani akitaka leo hii kuiharibu nafsi yako iliyobeba utajiri wako mkubwa na wa jamii, anaweza kuyatumia mazingira yawe ya kazi, unapoishi, unaposhinda ili kukiharibu kile ulichonacho moyoni usiposhituka fahamu ndiyo umepigwa hivyo!! Wewe fuatilia hii Afrika utagundua hiki ninachokuambia, utashangaa hao wenye akili wengi wamekumbana na kashfa ambazo zimewaharibia kabisa sifa zao, na ukichunguza baadaye utagundua kilichowaliza ni mfumo wa mazingara ya kazi waliyoamua kuifanya ndiyo umetumika kuzipigia nafsi zao na kuwaacha wakiwa wameumia.
Ngoja niseme kitu hapa. Adui akitaka kuiangamiza nafsi yako nakuhakikishia anaweza kutumia KAZI TU. Si kila kazi inayokuja mbele yako ukubali kuifanya hata kama inamasrahi ya kiwango gani. Jaribu kuiangalia hiyo kazi inanifaa kutokana na nilichona nacho moyoni?
Maandikoyanasema hivi."Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo."(Mhubiri 4:6). Lazima ujifunze kuangalia je! Kazi hii itanipa faida lakini taabu yake itakuaje? Fikiria leo hii unapata kashfa na elimu yako hiyo kashfa itakayodumu kizazi hata kizazi.
Watu wengi sana wanakulupukia nyazifa furanifurani hawaangalii mazingira ya hizo kazi je! Hawabanwi MOYONI YAANI KIWANGO CHA UJUZI WAO (Akili) kitatumika ipasavyo! Huwezi kuniambia kuwa unajua si anatafuta fedha bwana? Ukiona unamawazo moyoni mwako ya mfumo huo fahamu kuna tatizo moyoni mwako.
Watu wengi wenye akili kwa kutojua wamejikuta wanabuluzwa na wasio na akili kisa WAMEKUBALIANA NA MAZINGIRA WALIYOYAKUTA HAPO AMBAYO WASIO NA AKILI NI WAZOEFU NAYO!!! na leo nikwambie ukweli kabisa kama hujui kuna siku utasimama mbele za Mungu na utatoa hesabu ya kazi ukiyofanya duniani. Mungu hawezi kukaa kimya wakati anaona anakupa uwezo mkubwa mno wa kufikiri ili utatue matatizo ya watu wake na wewe unakubari kufanya kazi ambayo akili yako inadumaa na unaangalia tu.
Ngoja nikuulize swali hili muhimu sana hivi kazi ya mbunge ninini? Hivi hii kazi inamuhitaji profesa? Au daktari? Au mhandisi? Fikiria kidogo huyo mhandisi abanwe huko kwenye siasa. Nakwambia ukweli atajikuta tu anatumika tofauti kabisa na uwezo alionao. HUYU MTU ANAKITU TOFAUTI NA MAZINGIRA ALIYONAYO KATIKA KAZI ZAKE. Na wengi nakwambia wakiingia huko wanapoteza uwezo wa taaluma yao kabisaa. Wengine wanashindwa hata kutoa ushauri wa utaalamu wao si wanabanwa na siasa waliyoikuta hapo?
Labda hunielewi vizuri vikiria wewe ni mtaalamu unajua kabisaa hii barabara au hili daraja libatakiwa liweje linagharimu shilingi ngapi nk. Unatoa hoja zako za kitaalamu unakutana na watu si wataalamu kabisaa na hiyo kazi wanakuambia hapana fanyahivi nahivi kisa ni mtu mwenye nafasi furani. Wewe Mtaalamu( mwenye ufahamu mkubwa) unakubali unafalifanya daraja hilo linakatika baada ya siku chache tu, unafikiri ninani ataumia moyoni mpaka huku nje ni huyo mtaalamu au hao waliomwambia kalinenge hivi hivi? Nani anabeba mashitaka? Nani ataonekana hafai? Naona sasa unaanza kunielewa ninapokuambia adui anaweza tumia mazingira ya kazi tu kuipiga nafsi ya mtu mwenye akili na akamtengenezea jeraha moyoni kubwa tu.
Najua ni ngumu kunielewa leo lakini kaa tafakari kwa kina utakiona hiki ninachokufundisha kwa uwazi kabisaa. Unajua bahati mbaya sana sisi wanadamu hatujitambui ni kina nani na tuliumbwa tufanye nini kwa ajili yetu au jamii. Usipojitambua nirahisi kutafuta kazi NYEPESI YENYE FEDHA FEDHA ZA KIUEPESI WEPESI HIVI NA HESHIMA HESHIMA HIVI.
Lakini ukijtambua wewe ninani huwezi tafuta kazi nyepesi ambayo huumizi akili yako katika kuifanya. Mimi nakwambia nchi hii inawatu ambao ni vichwa kwelikweli yaani WANA AKIKI NYINGI SANA.. Usishangae hicho kichwa kimoja tu utapanga vichwa vya wazungu kumi bado hawaingii kwa kichwa hicho kimoja tulichonacho nchini humu. Unaweza bisha, kakini fanikiwa kutoka nje ya chi hii kaa huko au kaa na hao waitwao wazungu utawasikia wasemavyo.
Sasa nenda kaangalie ninini kimewabana hawa ndugu tuliojariwa kuwa nao humu nchini? Utagundua ni mfumo wa mazingira waliyopo( YAANI MAHALI) WENGI HAWAPO MAHALI WALIPOTAKIWA WAWEPO. (KIUTENDAJI) HAWAFANYI KILE WALICHO TAKIWA WAKIFANYE.
Wanapoteza nafasi yao na sifa zao wanaonekana ni watu wa kawaida tu kumbe siyo kabisaa.
Watu wengi wanavitu vikubwa mioyoni mwao lakini haviwasaidii wao na jamii kwasababu tu HAWAVITUMII. Wewe fuatilia leo hii uone unakuta kila mchungaji anataka asome weeee , awe na shahada nyingi tu nk. Nenda kaangalie hiyo elimu yao kama inawasaidia wenyewe na huko kanisani, wewe nenda kaangalie, Utapata jibu. Kuna madaktari wengi maaskofu na wachungaji angalia walichonacho kama kimekua ni msaada kwa kanisa. Utaona hakuna lolote
Utaona hawakitumii kwa ufanisi kile walichonacho kisa MAZINGIRA. Wewe njoo na hiyo shahada yako ukutane na baraza la kanisa ambalo limeketi kwenye mazingira furani na lina mfumo wake na limeuzoelea usishangae BARAZA HILO LIKAMBANA HUYU NDUGU MCHUNGAJI AKAJIKUTA YUKO KAMA WALEWALE WATU WA BARAZA Eheheee. !! Mpaka unashindwa kuelewa hiyo digrii ipo au imekufa?
Mazingira yanaweza kutumiwa na adui kuipiga akili ya mtu mwenye akili kabisa. Asiposhituka anajikuta amekufa na mawazo yake mazuri kweli ila hayakumsaidia yeye na hao watu wengine. Ndiyo maana Mungu anasema linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo
Pia adui anaweza kuipiga nafsi yako kwa kukuinulia marafiki ambao Hawata kushauri jambo lolote la maana. Ukiwa unawakubalia tuuu usishangae wewe na wao wote mnakua sawasawa. Siku moja niliwahi kwenda mahali furani ni kijijini sana tu, eneo hilo niliwakuta wenyeji na eneo lile mtu aliyekua akiaminika kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko wote alikua ni mwalimu. Wale watu waliponifahamisha kuwa huyu ndiye mwalimu mkuu, na niliona walimuheshimu mno yaani walimpa nafasi ya juu mno.
Binafsi mimi niliona mwalimu huyo na hao watu wa eneo hilo wanaomuona huyo mwalimu ndiye mwenye uwezo mkubwa niliona wako sawasawa tu. Sikuona tofauti yoyote aliyokuwa nayo yule mwalimu na hao watu. Nilipoongea naye niligundua adui alitumia mazingira yale aliyoyakuta pale yule mwalimu kumbadilisha kabisaa yule mwalimu msomi. Unajua watu wa eneo lile wameendekeza mno pombe, wavivu, nk . Niliona yule mwalimu alipofika pale akajikuta amebanwa na hayo mazingira akafanana kabisaaa na watu wa maeneo yale. Yaani muda niliokua naongea naye alikua nayeye kanywa pombe. Niliona nyumba yake ameshindwa kuitunza. Nyumba yake nzu ilifanana kabisaa na nyuma za wale wenyeji kwa muonekano.
Nikaenda mahali pengine niliwakuta wenyeji wa maeneo yale hawatofautiani ni mazingara yale ya kwanza. Cha ajabu, mwalimu mkuu niliyemuta hapo nilimuona kabisaa yupo tofauti hata na wale wenyeji. Hakubanwa na mazingira yale wala hakuifuata ile tabia ya wenyeji. UNAMUONA KABISA HUYU MSOMI MWENYE AKILI. Akili yake haikuchakachuliwa na mazingira yale. Ukiangalia nyumba yake nzuri, kajiwekea sola, analima mashamba yake mengi tu mazuri, unaona hata mazingira ya shule yake ni tofauti na yule mwingine. Unajua hata watu wakaribu yake wenyeji unawaona tuu wako tofauti na wale wa kukeee!! Ukiona hivyo unajua tu AKILI YA HUYU NDUGU IKO VIZURI HAIJASHAMBULIWA KWA KUTUMIA MAZINGIRA.
Sikiliza nikwambie, Usipojifunza leo hii kutokukubali akili yako igeuzwe na mazingira mabaya unayokutana nayo nakwambia ukweli mazingira hayo yatatumika kugeuza mfumo mzima wa mawazo yako fikra zako na kutafakari kwako na ushishangae unakuja kushituka umeumia vibaya mno nafsini mwako.
Mimi nakwambia ukweli ukienda na watu wenye akili utashangaa mawazo yako yanabadilika utawaza maendeleo, ukiambatana na walevi na ukabanwa na mawazo yao ya kilevi, utashangaa utajikuta nawewe umekua hivyohivyo!!!!! Umewahi kutana na mtu ambaye anaambatana na mtu mwenye mawazo ya chinii? na bahati mbaya akakubaliana na huyo mtu mwenywe mawazo ya chini!! Mimi nakwambia kila siku utashangaa ndiyo anakua chini tuuuu!!!
Ngoja nizungumze na wachungaji wale ambao makanisani mwao wanautaratibu wa kuhama kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine. Nakwambia ukweli. Unaweza leo hii ukawa mchungaji na ukapelekwa mahali furani usipokua makini utashangaa mazingira unayokwenda kuishi na watu utakaokwenda kukutana nao huko adui akayatumia mazingira hayo kuishambulia nafsi yako na ukajikuta tayari mfumo wote wa akili zako umeharibiwa kabisaaa!!! Huwazi kama ulivyokua unawaza unajikuta unawaza kama wenyeji uliowakuta hapo wawazavyo!!!
Pia shetani anaweza kutumia rafiki kabisa kuishambulia nafsi yako na akaiharibu akili yako kabisaa, lazima uwe mjanja sana, ujue kiwango cha akili cha mtu unayeambatana naye kikoje. Ili wazo akupalo kabla ya kukulupuka kulifanyia kazi uwe unajua limetokea kwa mtu wa aina gani. Fikiria kidogo mfano huu. Adamu maandiko yanasema hakudanganywa. Aliyedanganywa ni mwanamke, angalia mistari hii." Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa."(1Timotheo 2:14)
Kwa mujibu wa maandiko hayo unaona wazi kuwa akili za Adamu zilikua nzuri kabisa wala hazikuchakachuliwa na udanganyifu. Angalia kitu cha ajabu kabisa, mwenye akili nzuri akapokea wazo kutoka kwa mtu aliyepungukiwa akili kwa kudanganyika na huyo mwenye akili timamu akala lile tunda na akajikuta ameumia vibaya mno nafsini mwake na mwilini mwake, kifo kikawa sehemu ya maisha yake,
Na baadaye akafa kweli, Umewahi jiuliza tatizo lilikua wapi? Moja ya tatizo lilikua ni namna Adamu alivyokosa umakini wa kupokea mawazo kutoka kwa mtu anaenda naye kipindi kile alikua ni mke wake. Hata leo wapo kina Adamu wengi sana. Hujawahi sikia watu wanasema. Yule ndugu ni mtu mzuri sana anayempoteza ni mke wake!!! Maana yake ni hivi. Hayuko makini katika habari za kupokea mawazo kutoka kwa mke wake, kila amwambiacho yeye anakibeba tu. hachambui mchele na mawe anakula tuuuu!!!
Hata huko makanisani, utawakuta watu wenye akili nzuri tu, wanabeba mambo bila kuyaangalia yana kuwa sumu kubwa kwenye mioyo yao na kwa jamii na familia.. Ukiwauliza kwanini unafanya hivi? Anakuambia mtumishi katuambia. Yaani wamepokea wazo kutoka kwa mtumishi. Halichunguzi wanabeba tuuu. Muulize mbona Biblia haisemi hivyo? Ndiyo anashituka eti eeeee!!!! Jifunze kuangalia kilawazo limetoka kwa mtu aliyedanganyika au la? Ukiona wazo hili limetoka kwa mtu aliye danganyika fahamu ukilifuata litakua bomu ndani ya moyo wako. Litazilipua akilizako na utashi wako na hata hisia zako.
Ndiyo maana Biblia inatufundisha hivi."Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Naamini umenielewa. Mungu akubariki sana."(Mdo 17:10-11). Hakikisha unachunguza maandiko usiwe mtu wa kukibeba kila ukisikiacho bila kukichunguza.
Mungu akubariki sana tuonane tena katika kipindi kijacho
Wako
Mr Steven & Mrs Beth Mwakatwila

No comments:
Post a Comment