Wednesday, 22 February 2017

HATIMAYE ALIYEFUKULIWA NA MAMA YAKE AZIKWA UPYA MKOANI MBEYA

Shughili za Mazishi kwa mara ya pili zikiendelea makaburini huko Mbalizi, Mbeya

Hatimaye serikali imeingilia kati sakata la Luth Segeleti(52) mkazi wa Shigamba Mbalizi aliyefukua mwili wa mtoto Baraka Mfwango (22) aliyefariki februari 15 na kuzikwa februari 16 na kufukuliwa na mama Mzazi kwa madai ya kumfufua februari 18 mwaka huu ambapo serikali imeamua kuzika upya baada ya mama huyo kuridhia kufuatia Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoa wa Mbeya Mchungaji Edwin Urio kukutana naye katika kituo cha Polisi Mbalizi.
Naye Neema Mfwango dada wa marehemu aliyefuatana na mjomba wake ameshukuru kwa uongozi kuchukua jukumu la kumzika ndugu zangu yake. Kwa upande wake Mchungaji Edwin Urio amesema kuwa Luth si muumini wa Kanisa hilo bali alifika kanisani hapo mwaka mmoja uliopita kwa ajili ya maombi. 
Kwa upande wa Mchungaji Lauden Mwafongo aliyeendesha Ibada ya mazishi amesema Luth Segeleti si muumini wa Kanisa lake bali alimfahamu akija kwenye maombi kama watu wengine wanavyokuja na kwamba alitoa huduma ya mazishi kama Mchungaji na si muumini. Wakati huohuo ,Kikao kilichofikia muafaka wa mwilio huo kuzikwa tena kiliongozwa na Afisa Tarafa ya Usongwe Sadat Mtwale,Diwani wa Nsalala Kissman Mwangomale maarufu kama KK , ndugu wanne wa marehemu na mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi Debora Mrema ambapo Afisa Tarafa ameonya juu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Baadhi ya wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba Serikali kuwa makini na imani potofu zinazoleta uvunjifu wa amani . Luth aliomba radhi kwa wakazi wa Shigamba Mbalizi na viongozi wote kwani amedai imani ndiyo iliyomfikisha hapo na hakushauriwa na mtu yeyote. Mazishi yamefanyika nje kidogo ya mji wa Mbalizi tofauti na kaburi lile la awali kwa kuhudhuriwa na ndugu wanne wa Luth Segeleti pamoja na viongozi wa Serikali huku mvua kubwa ikinyesha.

No comments:

Post a Comment