Friday, 24 February 2017

DIAMOND PLATNUMZ AWIKA MAREKANI, MARRY YOU YAINGIA TOP 20

Diamond Platnumz  anazidi kufikia malengo aliyojiwekea mwaka huu. Video ya wimbo wake, Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, imeingia kwenye Top 20 za Vevo nchini Marekani. Chati hiyo inahusisha wasanii wapya wa Marekani.
Video hiyo sasa inapigana vikumbo na ngoma za rappers maarufu wakiwemo Desiigner na Lil Yatchy. 
“Kwahiyo @vevo ndio wameamua iwe hivyo? Top 20 New Artists Videos in the U.S na #MarryYou imo? Kwanini wanafanya upendeleo?,” ameandika meneja wake, Sallam SK

No comments:

Post a Comment