Saturday, 4 February 2017

ASKARI 10 WAJISALIMISHA POLISI SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA

Sakata la dawa za kulevya limeendelea kutikisa wakazi wa jiji la dsm ambapo leo Askari 10 kati ya 12 wanaotuhumiwa kuhusika na mtandao wa dawa za kulevya wamejisalimisha kituo kikuu cha Polisi ambapo pia wasanii watano wakiongozwa na wema Sepetu nao wanaendelea kuhojiwa na Polisi dhidi ya kuhusika na uuzaji wa dawa za kulevya.

M/kiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa dsm ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa dsm Paul makonda  akizungumza katika kituo cha Polisi cha kati amesema Operesheni dhidi ya wauza dawa hizo na wasambazaji inaendelea ambapo askari wengine watatu wanaodaiwa kupokea shilingi bilioni moja kutoka kwa wauza dawa hizo wiki iliyopita.

Aidha Makonda amesema Vita ya dhidi ya dawa za kulevya itakuwa ya muda mrefu na kuwataka wananchi kuendelea kutoa Ushirikiano wa kutoa taarifa za kweli ili vyombo vya dola vichukue hatua bila kumuonea mtu.

Kamishna wa Polisi kanda maalum dsm amesema tayari askari 10 wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa dawa za kulevya wamejisalimisha polisi na kuendelea kuhojiwa lakini pia wasanii watano wakiwemo wema sepetu wameendelea kuhojiwa tangu majira ya saa tano asubuhi. 

No comments:

Post a Comment