Sunday, 22 January 2017

NILIMUOA DADA YANGU

Mtunzi Jimmy Luoga

EPISODE: 11

ILIPOISHIA:
Tulimuona Erick akisubiri Kwa hamu kupambazuke ili aweze kutekeleza maagizo ya Allen ambaye alifanya uhalifu katika nyumba yake pia kumteka nyara mke wake.Je nini hatma ya simulizi hii?

SASA ENDELEA:

Majira ya saa kumi na moja alfajili nilimgongea mama mlango wa chumba alicholala kisha nilimuaga kuwa natoka kidogo kisha ningerejea baada ya muda mfupi, Mama yangu alinitazama usoni akaweza kugundua jambo fulani kisha akaniuliza "mwanangu Daniel upo sawa kweli?", niliitikia Kwa kichwa kisha nikaongeza na tabasamu kuwa nilikuwa sawa kabisa "Mimi najua haupo sawa, kwani naamini mkeo ndio faraja kubwa katika nafsi yako, hivyo najua unakwenda kumtafuta lakini Mungu akutangulie Kwa yote" Mama alikohoa kidogo kisha akaaendelea " naomba mara tu utakapofanikiwa kumpata mkeo uje nae moja Kwa moja hapa nyumbani ili niweze kumpatia baraka zangu" Mama alimaliza huku akitiririkwa na mchozi.Nilijikuta nikimkumbatia mama yangu huku nikitiririkwa pia na mchozi kwani mpaka wakati huo sikujua Allen alimpeleka wapi Liz.Niliagana na mama kisha nikaingia chumbani kuchukua begi ambalo nilihifadhi vile vyeti vya mali zangu kisha nikatoka moja Kwa moja mpaka sehemu ya kuhifadhia magari, nilichukua gari ambalo nililiita la masafa marefu Prado rangi nyeusi kisha nikaanza safari bila kujua nilikokuwa nakwenda.Nikiwa njiani simu yangu iliita, niliichukua haraka nikizani huenda Allen ndiye alikuwa akipiga.Lakini jina la Mwanasheria wangu ndilo niliona juu ya kioo cha simu yangu.Sikuhitaji kupokea simu hiyo kwani sikupenda kuzungumza naye lolote kwa wakati huo, majira ya saa kumi na mbili asubuhi nilikuwa Barabara ya Shekilango nikielekea Kariakoo.Nikiwa kwenye mwendo mkali ghafla simu yangu iliita tena, ilikuwa ni namba ngeni kabisa iliyonifanya nipunguze mwendo kisha nikaipokea simu hiyo na kuweka sikioni "Upo wapi?" ndiyo nilichoulizwa awali, nilimjibu kuwa nilikuwa Barabara ya Shekilango "Sasa njoo moja Kwa moja mpaka huku Feli kisha tutakupa maelezo zaidi" sikuweza kuhoji kwani ilikuwa ni sauti ngeni kabisa katika masikio yangu, pia iliashiria ukali. Niliongeza kasi ya gari langu kuelekea huko Feli. Ndani ya nusu saa nilishawasili pale Feli kwani siku hiyo ilikuwa jumapili hata foleni ya magari ilipungua Kwa kiasi kikubwa.Mara baada ya kuwasili pale Feli nilisimamisha gari mkabala kabisa na lango kuu la kuingilia kwenye ofisi za Pantoni la Kivukoni, simu yangu iliita tena Kwa namba ileile ya awali "Acha kila kitu humo humo ndani ya gari kisha usikate simu teremka garini Kwa kufuata kile nitakachokueleza" sauti hiyo iliamuru lakini jambo la kuacha kila kitu ndani ya gari bila kumuona mke wangu Liz ambaye nilimpenda kuliko hata mali zangu nilihisi kukosa vyote hivyo nilihoji "Mkuu nitawezaje kuacha hati za mali zangu bila kumuona mke wangu Liz?", "Kijana fuata Maelekezo vinginevyo utampoteza mkeo ambaye yupo salama salmini, hebu sikia sauti yake ilivyo mwororo..." ni kweli niliweza kusikia sauti ya mke wangu Liz ikiniita Kwa kilio, "hebu tazama mbele yako!.." niliweza kumuona mke wangu akiwa amesimama na vijana watatu ambapo mmoja aliishika simu dhahiri niliweza kugundua Kijana huyo ndiye aliyekuwa akizungumza na mimi.Nilijikuta nikiteremka garini na kuanza kupiga hatua kuelekea upande aliokuwa mke wangu na wale watu, yule mmoja wao aliniamuru kuwa nisimame palepale Kwa dakika mbili kisha akamuachia mke wangu ambaye alinikimbilia haraka, nami nikafanya hivyo tukakutana katikati na kukumbatiana Kwa furaha, mlio wa gari langu lililokuwa linakuja Kwa kasi nyuma yangu lilimfanya Liz anisukumie pembeni kisha gari hilo lilimkuta yeye uso Kwa uso, lilimgonga na kumtupa katikati ya Barabara akiwa anavuja damu.Nilipiga kelele Kwa mshituko kisha nikaanguka chini na kupoteza fahamu, nilipokuja kushtuka niliona nimezungukwa na kundi kubwa la watu ambapo baadhi yao walikuwa wakinipepea na mashati yao."Ameamka! Ameamka! Ameamka!" zilikuwa ni sauti za watu mbalimbali katika eneo lile, "Pole sana bosi, unajisikiaje Kwa sasa?" ilikuwa ni sauti ya Mwanasheria wangu "Mke wangu Liz yupo wapi?" nilijikuta nikiuliza huku nikilengwalengwa na machozi machoni mwangu, Mwanasheria wangu hakujibu bali alinisihi niingie kwenye gari lake, niliporusha macho pembeni niliona damu nyingi zikiwa zimetapakaa katika eneo lile lote, nilishtuka zaidi nilipoiona maiti ya Allen ambaye alitobolewa na risasi tumboni." Ni nini kimetokea hapa ndugu yangu?" nilijaribu kuuliza lakini safari ulishaanza, Mwanasheria wangu hakujibu kitu.Nilipenda kujua hali ya mke wangu pia hata hilo hakulijibia.Nilizidi kuchanganyikiwa kwani mpaka wakati huo sikujua nini kilimpata mke wangu, gari lilipoingia ndani ya nyumba yangu nilisikia kilio cha Mama yangu mzazi.Niliingia ndani kuuliza kulikoni, nilimkuta Mama kaikumbatia picha ya Liz hivyo nikajua kuwa mke wangu Liz alishafariki. "Daniel! Daniel! Daniel! umemuoa dada yako Elizabeth!" nilijikuta napata kizunguzungu na kuanguka chini Kwa mara nyingine, nilivyopata fahamu nilijikuta nikiwa hospitalini kuu ya Taifa Muhimbili, Mama alisogea mpaka nilipokuwa nimelala "Pole sana mwanangu, wa kulaumiwa ni mimi sio wewe wala Elizabeth.." alishindwa kuendelea tukajikuta sote tukilia, "Mama nimekusamehe Liz yupo wapi?.." swali hilo lilikuwa gumu kwa wote waliokuwa mule ndani ya wodi niliyolazwa "Mama Mbona hamnijibu Elizabeth yupo wapi?" ndipo Mwanasheria wangu aliposogea karibu nami na kuanza kunisimulia. "Erick ndugu yangu siku uliyonipigia simu kuwa ulikuwa unahitaji hati zote za Mali zako nilipigwa na butwaa, hivyo nilianza kukufuatilia tokea usiku ule Kwa ushirikiano na askari polisi, baadaye tuligundua nini ulitarajia kufajnya hivyo nilikuletea hati feki, na asubuhi ulipoianza safari sisi tulikuwa nyuma yako bila wewe kutambua, na hata baada ya ajali ya... hapo alishindwa kuunganisha neno nazani aliwaza atumie neno mke au dada yangu, kisha aliendelea ...ajali ya Liz ilisababishwa na Allen ambaye alishambuliwa na risasi na askari polisi". alisita kidogo kisha aliendelea "pole sana Erick kwani Liz hatunaye tena duniani, nilijikuta nikianza kulia kama Mtoto mdogo kwani Liz ijapokuwa alikuwa ni dada yangu Lakini Kwa kipindi chote nilichoishi naye nilishamzoea kama mke wangu, Nilijikuta nikilia na kutamka maneno NILIMUOA DADA YANGU"

************MWISHO*************

No comments:

Post a Comment