Mtunzi Jimmy Luoga
EPISODE:10
Ilipoishia tulimuona Erick akikutana na Mama yake ambaye alipoteana naye miaka mingi toka lilipotokea lile tukio kule kijijini Kiuma, Erick ambaye kwa sasa ni daktari katika hospital ya Muhimbili anaamua kumchukua Mama yake na kwenda naye nyumbani kwake.Je nini kitatokea huko nyumbani? ungana nami katika seheme hii ya kumi.
SASA ENDELEA......
Zilibaki kama mita mia moja kufikia lango kuu la nyumba yangu ghafla niliona gari likitokea ndani ya nyumba yangu kwa kasi ya ajabu na kutupita kwa kasi ya ajabu, nilijiuliza ni nani ambaye alitoka pale ndani na lile gari sikupata jibu.Kengere ya hatari iligonga katika kichwa changu, nilipokaribia geti niliona likiwa wazi, "Mama tumefika nyumbani" niliongea kwa kujikaza kwani mpaka wakati huo sikutaka kuonyesha dalili zozote kwa mama yangu mpendwa, nilipoingia ndani niliweza kumuona mlinzi akiwa kalala pembezoni mwa geti huku akiwa anatokwa na damu nyingi sehemu ya kichwa."Nini tena kimetokea hapa mwanangu?" Mama aliuliza lakini sikuweza kumpa jibu kwani tayari nilikuwa nimeshafungua mlango wa gari na kukimbilia alipokuwa mlinzi ambaye alikuwa anarusha miguu na mikono, nilipomkaribia tayari mlinzi huyo alikuwa ameshafariki.Nilichanganyikiwa kwani nilijaribu kumuita lakini hakuitika zaidi alitoa macho ambayo nilimfumba na kusimama kisha nikakimbilia ndani,nilipoingia sebuleni nilimkuta binti wa kazi wa zamu siku hiyo akiwa amelala kifudifudi, nilimuita kwa jina lake akaitika.Namshukuru Mungu binti huyo hakujeruiwa, mara baada ya kuamka nilimuuliza aliko mke wangu Liz, jibu alilonipa lilinifnya nichanganyikiwe zaidi na kuambatana na kilio kikubwa alichokiangua Mama.Nilimtuliza Mama kuwa huo haukuwa wakati wa kulia bali ni wa kupeana faraja.Jibu alilonipa yule msichana lilikuwa la majonzi kwangu kwani alisema kuwa mke wangu alitekwa nyara na watu ambao waliziba nyuso zao, nilijiuliza maswali mengi kwanini walimteka mke wangu nilibaki bila kupata jibu kamili.Nikiwa najiandaa kwenda kituo cha Polis kutoa ripoti ghafla nilisikia mlio wa king'ora cha gali la polis likiingia ndani ya geti la nyumba yangu likiwa limebeba askari wasiopungua ishirini."Mr Erick upo chini ya ulinzi" nilishtuka kusikia sauti hiyo ya amri kutoka kwa askari ambaye alionekana kuwa mkuu wa msafara ule.Nilipotaka kuuliza kulikoni nilipigwa kibao ambacho kilinifanya nione nyota nyingi zikiwa zimenizunguka, Mama yangu alipiga mayowe na kufanya majirani na wapita njia kuja kuangalia kulikoni tena kwa daktari Erick, nilifungwa pingu na kubebwa juu juu mpaka kwenye gari la Polis.Mpaka wakati huo sikuambiwa kosa langu nini zaidi niliona askari wakiendelea kukagua sehemu mbalimbali katika nyumba yangu wakishirikiana na mjumbe wa nyumba kumi kumi, "samahani afande hivi kosa langu mimi ni lipi?" najuta kwanini niliuliza lile swali kwani nilipigwa teke la uso almanusura ning'oke meno, "we mshenzi nini? unamtorosha mtuhumiwa halafu unajifanya kuuliza kosa lako.Nilishtuka kusikia habari hiyo ngeni katika masikio yangu, nikiwa najiuliza papo hapo niliweza kupata jibu la aliyemteka nyara mke wangu Liz, japo nilihisi lakini mawazo yangu yalinituma kwa Allen ambaye alihaidi kunifanyia kitu kibaya kutokana na kushindwa kumsaidia mpaka akahukumiwa kifungo cha maisha jela.Nikiwa nipo kwenye lindi kubwa la mawazo nilishtuka nikiamrishwa kuteremka garini kwani tayari tulishafika kituo cha Polisi Oestabay, nilipelekwa moja kwa moja ofisi ya upelelezi kuchukuliwa maelezo.Nikiwa katikati ya mahojiano, Mwanasheria wangu alikuja kwaajili ya kuniwekea dhamana, japo walijifanya kutia ngumu kutokana na vifungu vya sheria na weledi wa hali ya juu wa Mwanasheria wangu ilibidi niachiwe huru na kuripoti jumatatu yake.palepale ndipo nilipotoa taarifa za kutekwa mke wangu, askari walionikamata walibaki midomo wazi, kwani ndivyo ilivyo kwa jeshi letu la Polisi wanapokwenda kumkamata mtuhumiwa hutumia nguvu nyingi kuliko akili, laiti wangenihoji palepale huenda watuhumiwa tungeweza kuwapata haraka.Mara baada ya kutoa ripoti Polisi iliniomba msamaha kwa kitendo walichonifanyia, niliondoka nikiwa nimechukua namba za simu za mkuu wa kituo na OCD wa kituo hicho.Nilipofika nyumbani Mama alinilaki kwa furaha kwani alikosa amani kabisa akijua kuwa ningefungwa, ilikuwa tayari imeshatimia saa kumi na mbili jioni niliomba niongezewe ulinzi pale nyumbani kwani nilihisi huenda aliyemteka nyara mke wangu angerudi tena.Majira ya saa moja usiku akili yangu ikiwa haijatulia nikiwaza hali ya mke wangu ndipo mlio wa simu ya mezani uliita, nilinyanyuka sofani haraka na kwenda moja kwa moja ilipokuwa simu na kisha nikaichukua na kuiweka sikioni, sauti niliyoisikia haikuwa ngeni katika masikio yangu, ilikuwa sauti ambayo niliitambua katika nyakati zote kama vile furaha, majonzi na hata hasira.Leo hii sauti hii ilikuwa katika hali ya hasira na jazba haswa "Mr Erick mdogo wangu nakupa masaa 24 uwe umenikabidhi mali zote pamoja na pesa tasilimu milioni mia moja vinginevyo mkeo utamkuta baharini akiwa anaelea" sauti na maagizo hayo hayakutoka kwa mtu mwingine bali Allen, mtu ambaye niliamini ni ndugu yangu wa kufa na kuzikana, alisahau kabisa ni kwa kiasi gani nilitumia pesa nyingi kumuhangaikia kumtoa lakini ushahidi wa daktari ndio uliotufanya tushindwe shitaka na yeye kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.Nilikubali kila alichoniambia mwisho aliniambia ni wapi ningepeleka makabrasha yote pamoja na fedha, kisha akanionya endapo nitawataarifu Polis basi mke wangu angeuawa.Pale nyumbani hapakukalika niliwaza namna ya kuchukua document zangu zote kutoka kwa Mwanasheria wangu ambazo ndizo alizihitaji Allen pamoja na pesa, nilimpigia simu mwanasheria wangu na kumuagiza aje na makabrasha yote ambayo yalihusu mali zangu zote kwani niliyapenda zaidi maisha ya mke wangu kuliko hata zile mali ambazo niliamini ningeweza kutafuta zinngine.Mara baada ya mwanasheria kuja nilizichukua zile nyaraka bila kuzungumza naye chochote tukaagana.Mwanasheria wangu alijaribu kuniuliza kulikoni lakini sikumjibu kitu zaidi niliingia chumbani na kujifungia.Usiku wa siku hiyo kwangu ulikuwa mrefu sana kwani ni siku mbili zilizopita mke wangu aliniambia ana ujauzito wa miezi miwili hivyo niliamini kama Liz angeuawa basi na mwanangu pia ningemkosa, kwakuwa Allen alishaanza kunihesabia masaa niliona kunachelewa kukucha ili niende benki kutoa fedha ambazo Allen alizihitaji na mke wangu awe salama.Nilijaribu kujilaza kitandani nipate japo lepe la usingizi lakini nilishindwa, nilibaki natembeatembea katika chumba changu.........
Je nini hatma ya simulizi hii ya kusisimua? Ungana nami toleo lijalo upate uhondo!!!!!!
Usisahau kutoa maoni yako.
No comments:
Post a Comment