Friday, 20 January 2017

NILIMUOA DADA YANGU

Mtunzi Jimmy Luoga

EPISODE:9

Ilipoishia tuliona Liz akisua kuitikia swali la Padre kama alikubali kuolewa na kijana Erick pale kanisani na kupelekea minong'ono kutokea kwa waumini mbalimbali pale kanisani.Je Liz alikubali kuolewa na Erick?,

SASA ENDELEA..........................
Mapigo ya moyo yaliongezeka na kunifanya niwe kama mgonjwa wa moyo mwenye shinikizo la damu, kwa mbali niliona pumzi ikitaka kuniishia, nilimtazama Liz kwa macho ya upole lakini hakuweza kunitazama macho bali niliweza kuuona mchozi ukitiririka katika mashavu ya Liz, Padre alikohoa kidogo kisha akajitutumua na kuuliza kwa sauti kubwa kuliko mara zote, waumini wote walitulia kimya kwa kuona nini ilikuwa hatma ya ndoa yangu na Liz msichana niliyetokea kumpenda hasa, "ndi....o.....na....na....na...ku...bali" lilikuwa jibu la Liz na kusababisha kanisa zima lilipuke shangwe, nderemo na vifijo mara baada ya Padre kuuliza swali hilo kwa mara ya tatu na mwisho.Nilijikuta nikimkumbatia Liz kwa nguvu na kumshukuru kwa kubali kuwa mke wangu wa ndoa kwani niliamini kifo pekee ndicho kingetutenganisha, mara baada ya tukio hilo zoezi la kuvishana pete lilichukua nafasi, nilishangaa nilipoanza kumvisha pete Liz kidole chake kilitetemeka hasa, nami pia mkono wangu ulitetemeka zaidi.Baada ya dakika kadhaa zoez hilo lilikamilika, Padre alipokamilisha ibada familia zote mbili wakiwemo na wale wazazi wangu wa bandia kutupongeza kisha msafara wa kuelekea nyumbani kwangu ulianza, Foleni ya magari kama thelathini uligota pale Mwenge mara baada ya gari lililoongoza msafara kugonga mtu, nilijaribu kuuliza kulikoni tulisimama kwa muda mrefu mahali hapo?, ndipo dereva wa gari langu alisema kuwa kuna Mama mmoja wa makamo kagongwa na gari na kujeruhiwa vibaya.Mara baada ya kupata habari hiyo nilitaka kuteremka kwenda kutazama kulikoni lakini msimamizi wangu alinikataza kuwa haikupendeza kwa mimi bwana harusi kufanya vile, baada ya dakika kadhaa msafara uliendelea kama kawaida.Tuliwasili nyumbani majira kama ya saa saba mchana, kwakuwa tuliandaa chakula watu walijumuika katika chakula kisha mimi na Liz tulipata muda wa kuzungumza mawili matatu kule chumbani kwetu.Nilimuuliza Liz kwanini alipata wakati mgumu kujibu kama alikubali kuolewa na mimi alinijibu kuwa hata yeye mwenyewe hakujitambua ni wakati gani aliulizwa swali hilo, kwani hakuweza kujitambua muda wote mpaka tulipotoka kanisani, nilikumbatiana mke wangu Liz kisha tukapigana mabusu kadhaa na kurejea sebuleni mahali ambapo tuliwaacha wasimamizi wetu.Baada ya lisaa limoja tulienda kupiga picha na kupitiliza moja kwa moja ukumbini ambako tayari giza lilikuwa limeanza kuchukua nafasi yake, niliendelea kuitunza siri yangu kuwa mimi nilikuwa Erick na sio Daniel japo hata upatikanaji wa cheti changu cha ubatizo kilinipatia wakati mgumu na kuamua kuhonga pesa nyingi na kuniwezesha kufunga ndoa ile.Shughuli za ukumbini zilitumia kama masaa nane na ilipotimu saa tisa kasoro usiku tulipelekwa Serena Hotel kwa mapumziko, usiku wa siku hiyo tulikuwa tumechoka na hata tulipofika kitandani hakuna aliyekuwa na hamu na mwenzake, nakumbuka tulipokuwa kwenye mafundisho ya ndoa Padre mkufunzi alitusisitiza kuwa usiku huo mara baada ya kufunga ndoa, tendo la ndoa ndiyo lingehitimishwa chumbani na kukamilisha mustakhabali wa ndoa yetu, lakini tulipogusa tu kitanda usingizi mzito ulituchukua.Nikiwa usingizini ndoto ya mchana ilinirudia, kwa wakati huo niliota mimi nikiwa ndio yule dereva niliemgonga mama mmoja wa makamo, nilipoteremka garini ndipo nilipoweza kumuona Mama yangu mzazi akiwa amepoteza fahamu, niliomba msaada akimbizwe hospitali mara moja lakini Mama alinitazama kwa shida kisha alikata roho, nilijikuta nikipiga kelele za kuomba msaada lakini nilishtuka Liz akiniuliza kulikoni.Nilipojitazama nilikuwa nimekaa kitako pale kitandani jambo ambalo lilinifanya nijiulize niliamka muda gani, "Erick mume wangu una matatizo gani tena?" nilibaki nimeduwaa macho nimeyatoa pima, niliamua kumficha mke wangu kwani mpaka wakati huo bado nilimficha juu ya maisha yangu halisi.Nilimpoteza maswali yake kwa kumpapasa hapa na pale mwisho tulibaki watupu pale juu ya sita kwa sita tukipeana mahaba mazito yaliyotufanya sote tugune kwa raha tulizozipata.Japo tulikuwa na uchovu wa mchana kutwa Liz alinionyeshea ufundi wa hali ya juu na kujikuta nikipiga goli mbili mfululizo na kisha kuendelea na usingizi.Pale hotel ilikuwa ni kula na kufanya tendo la ndoa mfululizo takribani kwa mwezi mzima, ndipo tuliporejea tena nyumbani.Baada ya siku kadhaa dalili za wazi kuwa mke wangu alikuwa mjamzito ziliweza kuonekana na kunifanya nijisikie furaha maradufu.Nakumbuka siku ya Jumamos nilikuwa sijaenda kazini kwani tayari nilishaajiriwa na serikali katika hospital ya Muhimbili, nilimkumbuka yule Mama aliyegongwa na gari hivyo nilijaribu kumpigia Mwenyekiti wa kamati ya harusi yangu ambaye alikuwa miongoni mwa wale mameneja wa kampuni zangu.Alinieleza kuwa bado yule mama alikuwa hospitali akitibiwa, nilimuomba anielekeze wodi na chumba alicholazwa naye akafanya hivyo, nilimuaga mke wangu kisha nilianza safari mpaka pale hospitali.Nilipofika moja kwa moja niliingia chumba nilichoelekezwa, niliingia pale ndani nakumkuta Mama huyo akiwa amegeukia ukutani kauchapa usingizi.Nilisogea mpaka pale kitandani kisha nikageuka ili niondoke nikitarajia kurudi tena baadae, lakini nilipofika karibu na mlango nilisikia sauti ya yule Mama ikiniita "karibu Baba mi nipo macho", niligeuka na kupelekea kugongana macho na yule Mama, yule Mama alinitazama kama vile alishtushwa na ujio wangu pale, nilishangaa yule Mama akitupa mashuka kando na kusimama kisha akaanza kupiga hatua na kunifuata nilipokuwa nimesimama mimi, muda wote huo nilikuwa nimesimama nikimtazama kwani niliambiwa tatizo la huyo alipoteza kumbukumbu.Kama mtu aliyekuwa anachunguza kitu alinisogelea mpaka nilipokuwa nimesimama kisha akanishika mkono wangu wa kulia "Daniel ni wewe mwanangu Daniel? oh! siamini macho yangu" moyo uliniripuka kwa furaha kwani hata mimi nilipigwa na butwaa kusikia Mama huyo akilitaja jina langu ambalo nilianza kulisahau, Wapenzi wasomaji Mama ni Mama nilijikuta nikimkumbatia Mama yangu ambaye alikuwa anabubujikwa machozi ya furaha, "Daniel mwanangu nilijua umeliwa na wanyama wakali kumbe bado upo hai?" maneno ya Mama yangu mzazi yalinirudisha kwetu Tunduru usiku niliokimbia pale nyumbani na kujikuta nikitokwa na machozi.Daktari wa zamu aliingia pale wodini na kunikuta nimekumbatiana na Mama huku sote tukiwa tunalia, "kulikoni Doktor Erick?" nilikuwa nafahamiana nae hivyo nilimueleza kwa kifupi, hata yeye alijikuta akifuta mchozi kutokana na kuguswa na simulizi yangu, "pole sana Doktor Erick, sasa kwakuwa umeomba uende na Mama sisi tunampatia ruhusa ila hata mimi nimeshangaa kama Mama amekukumbuka, kwakweli Mama yako alipoteza kabisa kumbukumbu" yalikuwa maneno ya huyo Daktari wa zamu ambaye alijulikana kwa jina la Peter.Mara baada ya kupewa ruhusa safari ya Tegeta nikiwa na Mama yangu ilianza huku njiani akinisimulia alikomuacha Dada yangu Lilian, Mama alianza kunisimulia kwa masikitiko, alisema hivi; mara baada ya mimi kukimbia usiku ule alijaribu kupapasa Baba na kugundua kuwa alishakata roho, kwakuwa na yeye aliogopa tuhuma za mauaji aliingia chumbani kwake haraka kisha akachukua kiasi kidogo cha fedha ambacho aliweka akiba akambeba Lili mgongoni na kutokomea porini, Mama alifuta mchozi huku nami nikimbembeleza na kumpa moyo kuwa mimi mwanae nipo kwaajili yake, aliendelea kwa kusema; baada ya kufika porini aliweza kwa mbali kusikia kelele za watu na filimbi zilizoashiria ualifu kutokea pale nyumbani,hivyo watu walijaribu kumtafuta lakini hawakufanikiwa kumkamata kwani tayari alishatokomea porini, nilijisikia vibaya kwani mimi nilijiona ndiye nilikuwa chanzo cha mfarakano wa familia yangu, jambo jingine niliumia sana kwa kumuua Baba yangu bila kutarajia kwani pamoja na tabia yake ya ulevi na kumpiga mama usiku wa manane kila alipokunywa pombe, Baba yetu alitupenda sana na kutupatia malezi bora, Mama  aliendelea baada ya kufanikiwa kutembea kwa mguu takribani usiku mzima alifanikiwa kuingia wilaya ya Songea mjini na hapo ndipo alipokata risiti ya kusafiria na kuingia Jiji la Dar es salaam, maisha magumu aliyoishi Mama ndani ya Jiji hilo yalinitoa machozi, alisema ilifikia hatua baada ya kuona maisha ni magumu aliamua kwenda katika nyumba moja nje na kumtelekeza Lilian ambaye alidai mpaka wakati huo alipokuwa anazungumza na mimi hakujua mahali ambapo  alikuwepo, nilijikuta nikifuta machozi kwa awamu nyingine baada ya kupewa taarifa kuwa dada yangu hakujulikana mahali alipo.Nilimuhaidi Mama kumtafuta dada yangu kwa udi na uvumba mpaka nimtie machoni, nilimuuliza Mama kwa wakati wote huo mpaka anapata ajali alijishughulisha na nini?, ndipo aliponieleza kuwa mara baada ya kumtelekeza Lilian alifanikiwa kuolewa na kuzaa watoto wawili wakike ambao waliishi na Baba yao mara baada ya kuachana, maisha yalizidi kumuwia vigumu na kupelekea yeye kuwa ombaomba mpaka ajali ilipomkuta.Wakati huo tayari tulikuwa tumebakiza hatua chache kuikuta nyumba yangu.....

Je nini hatma ya simulizi hii? Toa maoni yako, Ungana nami toleo lijalo.

No comments:

Post a Comment