MTUNZI: Jimmy Luoga
SIMU NA:0755714395
SEHEMU YA 6
ILIPOISHIA: Tulimuona Rose akiwasili Dodoma pamoja na wazazi wake, lakini akiwa katika hotel ghafla macho yake yanazibwa na mikono ya mtu asiyemfahamu aliyesimama nyuma yake.Je ni nani ameziba macho ya Rose ungana nami katika sehemu hii 2017 mwaka mpya!
SASA ENDELEA........
Mtu huyo aliyeniziba macho hakuongea chochote kama sekunde kadhaa, nilijaribu kuipapasa mikono ya mtu huyo huku nikajaribu kubashiri kwa majina mbalimbali.Lakini mtu huyo aliendelea kukaa kimya."Umewataja wote lakini mimi pekee ulinisahau sio?.." haikuwa sauti ngeni katika ngoma ya masikio yangu, nilijukuta nikiinuka toka kwenye kiti nakumkumbatia mtu huyo kwa furaha, "Alice my friend I missed you so much!.." sauti kubwa ilitoka kinywani mwangu na kufanya watu wote pale Hotel watuangalie kwa mshangao.Alice pamoja nami tulijikuta tukibubujikwa machozi ya furaha huku tukiendelea kukumbatiana, kwani ni muda wa miezi kadhaa tulipotezana toka tulipohitimu kidato cha sita pale Kilakala."Rose rafiki yangu kipenzi I missed you too..!" Alice alinijibu huku akiwa ananitazama usoni huku akijifuta machozi ya furaha.Nilimkaribisha Alice kitini kisha tukaendelea na maongezi ya hapa na pale bila kusahau kupongezana kwa jitihada tulizozifanya mpaka kuitwa Bungeni Dodoma.Mhudumu alijongea mpaka katika meza yetu kisha akamsikiliza Alice alichoagiza na kutuacha tukiendelea kuongea hili na lile."Vipi Rose umefanikiwa kuonana na Emmanuel?.." nilishituka kuulizwa swali hilo na msichana huyo kwani siku zote pale shuleni sikuwahi kumueleza jambo lolote kuhusu Emmanuel, "Vipi mbona umeshtuka hivyo shoga yangu..? " aliniongezea swali lingine wakati huo nilikuwa namalizia kumeza funda la juisi iliyokuwa kinywani."Emmanuel ulimfahamia wapi shoga yangu..?", nilimuuliza Alice aliyekuwa akinitazama huku akiwa anatabasamu."Unajua nilimfahamu kijana huyo kupitia zile barua zenu mlizokua mnaandikiana, japo ulijitahidi kunificha lakini ulisahau kuwa mimi na wewe tulikuwa tunahifadhi vitu vyetu kwenye sanduku moja..", Alice alihitimisha.Nilijikuta nikitazama chini kwa aibu kwani kwa hilo niliona nilikuwa mbinafsi kwa rafiki yangu ambaye nilipendana naye sana, "samahani sana Alice, nilifanya yale yote kwa siri kwasababu sikupenda nikukwaze rafiki yangu..".Alice aliniambia kuwa alishanisamehe hivyo haina budi tuendelee na mambo mengine.Jina la Emmanuel lilirudi upya katika akili yangu mara baada ya kutamkwa na Alice, japo nilishapoteza usichana wangu na kijana ambaye sikumpenda toka moyoni kama Emmanuel. Nilijikuta nikianza kutamani kumuona mvulana huyo japo nafsi ilinisuta kuwa sikumfanyia jambo jema la kupoteza usichana wangu,"Emmanuel na John nilikutana nao waliniambia kuwa tutakutana kwenye rehearsal katika Ukumbi wa Bunge jioni.." .Nilifurahi kusikia hivyo kwani ijapokuwa nilishapoteza usichana wangu nilitamani kumuona Emmanuel.
**********************
Majira ya saa kumi Jioni mimi pamoja na Alice tulikuwa tukiingia lango kuu la Bunge, "enhe ninyi ni wakina nani na mna shida gani..?" lilikuwa swali toka kwa Askari tuliyemkuta pale langoni.Tulipomjibu alituelekeza kwenye mapokezi ambako tulipewa vitambulisho vya kuvaa shingoni kisha moja kwa moja tukapelekwa ukumbi wa Bunge, mara baada ya kuingia pale ndani, niligongana macho ana kwa ana na Emmanuel.Sote kwa pamoja tulijikuta tukitajana majina bila kujielewa, Tulikimbiliana na kukumbatiana.Watu wote pale ukumbini walipigwa na butwaa huku wakituangalia kama vile filamu ya kihindi, "Rose mpenzi nilikukumbuka sana..." kwa mara ya kwanza niliitwa jina hilo kutoka mdomoni mwake.Nilijikuta nikishindwa kujibu huku machozi yakinitiririka mashavuni kwani niliamini Emmanuel alikuwa na mapenzi ya dhati nami, lakini suala la kupoteza usichana wangu bila kutarajia ndicho kilichoniumiza zaidi.Emmanuel baada ya kuona nabubujikwa na machozi alitoa leso yake, kisha akaanza kunifuta machozi."Vijana nadhani mmesalimiana vya kutosha naomba msogee hili tuendelee na zoezi linalofuata.." Ilikuwa sauti ya mkufunzi ambaye alitakiwa kutufundisha namna tutakavyofanya siku itakayofuata wakati wa kukabidhiwa vyeti na zawadi pale ndani ya Ukumbi wa Bunge.Emmanuel alinishika mkonono huku akinitazama kwa furaha, nami nilifanya vivyo hivyo japo nafsi yangu ilinisuta kwa usaliti nilioufanya.Katika kundi lile wasichana tulikuwa watatu yaani Mimi Alice na mmoja alitokea shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora ambaye sikulifahamu jina lake.Wakati wote wa liheso Emmanuel alionesha kuwa na shauku kubwa ya kuzungumza nami lakini alikosa nafasi.Mara baada ya liheso tuliagizwa kuwahi saa mbili asubuhi ya siku ya pili, Emmanuel alinifuata kisha akaniomba tukazungumze japo kwa dakika kadhaa mahali alipofikia.Nilipomuuliza nilishikwa na bumbuwazi, kwani naye aliniambia alifikia Dodoma Hotel.Nilijiuliza kimoyomoyo ina maana Wahitimu wote tulifikia hotel moja..?" Jibu likawa ndio kwasababu wote walisema kuwa wamefikia pale Dodoma Hotel.Nilimkubalia Emmanuel lakini nilimpa sherti moja kuwa endapo nitakwenda kuzungumza nae awe peke yake, kijana huyo mtanashati na aliyeonesha kunijali zaidi alinijibu kuwa niondoe hofu.Nilimuomba anitajie namba ya chumba alichofikia naye akafanya kama nilivyomwambia.Niliagana na Emmanuel huku nikimuhakikishia kwenda kuzungumza nae majira ya saa mbili usiku baada ya chakula.Emmanuel alikubali huku akionesha shauku kubwa ya kukutana nami usiku wa siku hiyo.Mara baada ya mazungumzo ya dakika kama tano Emmanuel aliwafuata wavulana wenzake nami nikawafuata wenzangu huku safari ya kurudi hotelini ikiendelea.Nafsi yangu ilijaa hofu kubwa juu ya makutano na kijana huyo ambaye nilimthibitishia kuwa nilikuwa bikra.Nilijikuta nikikosa amani kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma, "mwanangu vipi mbona hauna raha kulikoni..?" Mama yangu aliniuliza swali hilo kama alishitukia jambo. "Hapana Mama nawaza namna kesho itakavyokua..", "sasa mwanangu badala ya kufurahia wewe unakosa raha, kula chakula kisha nenda kalale mapema sawa..?" Nikamjibu kisha nikala.Baada ya kula nilikwenda chumbani kwangu kisha nikajimwagia maji, nilipotoka maliwatoni tayari ilishatimu saa moja na nusu usiku.Nilivaa gauni langu zuri kisha nikajipaka manukato yaliyonukia vizuri, nakumbuka niliyanunua duka la Mwarabu mmoja hivi pale Mbinga mashuhuri kwa jina la Abdul Jemedar.Ilipotimu saa mbili kasoro dakika tatu nilikuwa nikibisha mlango wa chumba cha Emmanuel.....
Je, nini hatma ya simulizi hii? Ungana na Jimmy Luoga katika sehemu ya saba.
Usisahau kutoa maoni yako ni muhimu sana kwetu
No comments:
Post a Comment