Friday, 27 January 2017

NAJUTA KUKUFAHAMU

Mtunzi Jimmy Luoga.

SEHEMU:3

ILIPOISHIA:
Tulimuona msichana Rose akiwa amewasili katika shule ya Sekondari Mzumbe akiwa na wenzake kwenye shindano la mdahalo wa kiingereza.Ghafla anashikwa bega kwa nyuma na kukaribishwa kwa sauti ya upole, Je sauti hiyo ni ya nani?

SASA ENDELEA............

Nilishtuka kuonana uso kwa uso na John mvulana ambaye alikuwa akiniandikia barua, nilijikuta nikimkazia macho makali ambayo ndani yake yalijaa dharau na hasira juu yake, "Vipi Rose mbona unaonekana mwenye hasira hivyo?.." John aliuliza swali hilo kwa sauti ya upole zaidi, nilimtazama bila kumjibu neno lolote kisha nikapiga hatua chache toka pale aliposimama mpaka kwenye kundi la wanafunzi wenzangu ambao walisimama wakitutazama sisi.Nilijisikia aibu kwani pale shuleni nilikuwa miongoni mwa wasichana niliokuwa nawachukia wanaume, "vipi Rose yule kaka alikuwa anataka nini tena?.." swali la kinafiki niliulizwa na msichana mmoja aliyeitwa Maria, nilimtazama jicho kali jambo lililopelekea aendelee na mambo yake, kwa kifupi mimi ni msichana mrembo ambaye nilibarikiwa vitu vyote ambavyo mwanamke alihitajika kuwa navyo, ni mrefu pia shepu namba nane pia macho makubwa yenye mvuto wa aina yake, na kadiri nilivyokuwa nakua nilizidi kupendeza, rangi yangu ya maji ya kunde ilizidi kung'aa na kufanya hata niliporudi likizo nyumbani kwetu Mbinga wanaume kunisumbua kila nilipopita mitaani.Nilibarikiwa kuwa na miguu ya chupa ya bia ambayo iliendana na sketi ya shule niliyovaa, nazani hata baadhi ya walimu wakiume walipata shida kwani kila mara walijaribu kutupa ndoana lakini waliambulia patupu.Emmanuel ndiye mvulana aliyeichanganya akili yangu, ijapokuwa toka nizaliwe sijawahi kufanya mapenzi lakini kwa kijana huyo nilikuwa tayari kwa lolote hata kama kuruka uzio wa shule nilikuwa tayari.Niliendelea kupepesa macho huku na kule huenda ningemuona Emmanuel lakini sikuweza kumuona.Muda wa kula chakula uliwadia tukakaribishwa katika bwalo la chakula, niliendelea kumtafuta mvulana aliyeuteka moyo wangu lakini bado sikuweza kumuona Emmanuel, "Kaka samahani, kuna mvulana mmoja namtafuta sijui kama unaweza kunitafutia?..." uzalendo ulinishinda nikaona ni heri nimuulize huyo mwanafunzi aliyetukaribisha katika bwalo la chakula, "anaitwa nani huyo mvulana dadangu..". "Anaitwa Emmanuel..." nilimjibu "..Emmanuel nani kwakuwa shule hii ni kubwa kuna wakina Emmanuel kama kumi hivi?...." nilijikuta nikichoka ghafla kwani nilimfahamu kijana huyo kwa jina moja tu la Emmanuel bila ubin wake, kichwa kilipata moto mwisho yule kijana aliniomba wakati nafikiri ningekuwa napata chakula kisha nimjulishe baadaye.Kwa upande wangu chakula hakikunoga kwani niliamini kama nisingemuona Emmanuel siku hiyo huenda nisingepata nafasi ya kuonana tena na mvulana huyo.Baada ya chakula tulijongea mpaka katika ukumbi ulioandaliwa maalumu kwaajili ya mpambano wa mdahalo na wenzetu wa Mzumbe Sekondari.Mara baada ya sisi kuingia ndipo na wenzetu nao wakawa wanaingia pale ndani.Nilipigwa na butwaa kumuona mvulana niliyemtafuta kwa nguvu zangu zote akiwa anaingia na kuketi kiti kilichotazamana na mimi, furaha niliipata ilikuwa ni maradufu jambo lililopelekea nishindwe kuvumilia kitini na kumfuata Emmanuel kisha nikamkumbatia kwa nguvu na furaha zote, ukumbi mzima ulipiga makofi na moyowe ya furaha, " Emmanuel mzima rafiki?..." nilimuuliza kijana huyo ambaye alikuwa kaachia tabasamu lililonipa matumaini kuwa nayeye alitamani kuonana nami kwa muda mrefu, "nzuri Rose habari za Kilakala?...." kabla sijamjibu mwalimu alisema tumesalimiana vya kutosha sasa kila mtu akae tayari kwa Mdahalo, furaha niliyokuwa nayo ilinifanya nirudi eneo langu kwa shida kisha nikaketi huku tukiendelea kutazamana na Emmanuel.Mwenyekiti wa mdahalo wa siku hiyo aliporuhusu mdahalo uendelee bado mimi na Emmanuel tulizidi kutazamana kwa aibu na kukwepesha macho kila yalipogongana.Ilipofikia zamu ya Emmanuel kuongea ndipo nilipogundua kipaji kingine cha mvulana huyo, alikuwa na sauti nzuri yenye uwezo wa kutamka maneno ya kiingereza kwa ufasaha jambo lililopelekea kushangiliwa na umati mkubwa wa watu mule ndani, Emmanuel alichangia hoja kwa kujiamini kama vile lugha ya kiingereza ilikuwa yake.Nilijikuta nikijisahau kuwa nilikuwa upande wa kupinga na kumpigia makofi mvulana huyo.Ilipofika zamu yangu nilijikuta nikitoka nje ya mada na kumsifia Emmanuel kwa kiingereza alichokiongea jambo lililopelekea wanafunzi wa Mzumbe kunipigia makofi mengi zaidi huku wenzangu wakishikwa na bumbuwazi.Baada ya mdahalo wote tulitoka nje huku Kilakala tukishindwa kwa dondoo mbili jambo lililopelekea wenzangu wote kunikasirikia.Sikujali kwani mimi na Emmanuel tuliongozana taratibu huku tukizungumza hili na lile, mwisho niliingiza mkono mfukoni na kumkamatisha ile barua kijana huyo ambaye aliipokea na kuweka mfukoni.Nakumbuka wakati naitoa barua hiyo nilitetemeka mwili mzima kwani sikuwahi kufanya tendo kama hilo tangu kuzaliwa kwangu.Baada ya hapo niliagana na Emmanuel huku roho yangu ikiumia kwani nilitamani hata kukesha naye tukizungumza.Nilipoingia garini wenzangu waliendelea kunikalia kimya huku wakilalamika kuwa mimi ndiye nilikuwa msababishi kwa wao kushinda kwa kuingiza suala la mapenzi katika shindano, sikujali maneno yao kwani nilichokifuata kilikuwa tayari kimefanikiwa.Siku kadhaa zilipita ndipo siku moja nikiwa mstarini ghafla barua yangu iliitwa, nilikimbia mbio nikiwa na matumaini kuwa barua hiyo haikutoka kwa mwingine zaidi ya Emmanuel, niliipokea barua hiyo na kurudi kwenye mstari, kama kawaida yetu Alice aliniuliza inatokea wapi nikamjibu kuwa ilitokea Mbinga ambapo yeye akisikia inatoka huko ujua kuwa inatokea kwa wazazi wangu, hivyo hanibani ninapoifungua.Alipokwenda darasani niliifungua barua hiyo nilirusha jicho mwishoni ambapo niliona jina la Emmanuel Ngui, furaha isiyo kifani ilitamalaki katika nafsi yangu.Nilianza kuisoma barua hiyo kwa utulivu mkubwa, barua hiyo iliandikwa hivi................

Je barua hiyo iliandikwaje? tukutane Toledo  lijayo kwa maoni andika hapo chini au piga simu 0755714395.

No comments:

Post a Comment