Monday, 23 January 2017
ELIMIKA KWA SOMO HILI...WAYA UPI UUGUSE??
Siku moja Bogi Benda akiwa safari, gafla gari yake ikazimika. Alipojaribu sana kuwasha tena bila mafanikio akagundua kuwa mfumo wa umeme unashida. Akafungua bonet ya gari na kujaribu kushika hapa na pale, kuchomeka nyaya vizuri n.k lakini alipojaribu tena holaaaa!! Baada ya kufanya kila aliloweza kwa zaidi ya saa nzima bila mafanikio, Ikabidi asalimu amri atafute msaada, akafanikiwa kupata fundi ambaye ni mtaalamu wa umeme wa magari.
Fundi alipofika alifungua bonet baada kama ya dakika 6 hivi akamwambia Bogi Benda aingie kwenye gari awashe.. Hureee!! Gari likawaka. Bogi was happy now!
Bogi: Asante saana, yaani leo ningelala hapa
Fundi: Usijali mzee, ndio maana watu kama sisi tupo
Bogi: Haya niambie pesa ngapi nikulipe?
Fundi: huku akitabasamu, "Laki moja tu mzee"
Bogi: Whaaaaaat?!! Laki!! kwaajili ya nini?? Yaaani kugusagusa waya tu hapo unataka laki?!!
Fundi: Sio hivyo boss, Kugusagusa waya sio hela nyingi, ni 2,000/= tu, ila kujua waya upi niuguse ndio 98,000/=.
Somo:
Mara nyingi huwa tunaangalia kile kitu cha mwisho alichofanya mtu kabla ya matokeo, na tunafikiria hicho ndio "kilichomtoa". Utasikia "jamaa ile tenda ndio iliyomtoa" Au alipoanza kufanya biashara ya kuuza samaki ndio ilimtoa, huko kwingine alikuwa anapoteza Muda. Ukweli ni kwamba kilichomtoa sio hiyo biashara au ile tenda, ili ni majumuisho ya mchakato aliopitia ambao ndio uliomuandaa kwaajili ya hiyo tenda/biashara. Vyote alivyopitia vilisaidia kumjengea tabia, ujuzi, hekima anayohitaji kufanikiwa.
Baada ya kuwa amekusanya elimu, ujuzi na uzoefu wa kutosha mambo kwake yanaonekana ni kama just a click of a button.
Fundi umeme wa gari alitumia miaka kwenda shule na kufanya kazi gereji ili kujenga ujuzi wa kujua waya upi auguse.
Take time to build value in yourself, by learning and practicing. One day watu watashangaa utakapogusa waya sahihi.
Ndio maana kuna watu kwenye maisha wanafanya kitu "kidogo" wanalipwa pesa nyingi, na wewe unafanya kitu "kikubwa" (labda unafanya kazi masaa mengi kuliko wao) lakini kamwe huwezi kuwasogelea kwenye kipato wanachopata. Watu huwa hawalipwi kwa kuangalia MUDA, ila kwa THAMANI wanayoiweka ndani ya huo muda,
It's a value within a person that attracts the value we see(money).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment