Wednesday, 28 December 2016

MADHARA YA MATUMIZI YA SINDANO ZA KUZUIA MIMBA


Madhara
Matumizi ya sindano za kuzuia mimba huweza kuleta madhara kwa baadhi wa wanawake. ikumbukwe kuwa sio kila mwanamke anayetumia njia hii atapata madhara kutokana, ni baadhi yanaweza yakawatokea. Unapopata madhara yoyote kutokana na matumizi ya sindano hizi, onana na daktari wako kwanza.
  • Kupata hedhi kwa muda mrefu zaidi ya kawaida. Hali hii inaweza kutokea kwa mtumiaji hasa miezi ya mwanzoni. Mzunguko wa hedhi huweza kubadilika na kupata hedhi katikati ya mzunguko.
  • Kukosa hedhi.
  • Hailindi dhidi ya magonjwa ya zinaa na VVU. Hii ni kwa wanawake wote watakaotumia njia hii. Hivyo ni muhimu kuzingatia njia za kukukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na VVU kama kondomu.
  • Kuchelewa kupata ujauzito. Inawezea kuchukua miezi 6 – 12 kuweza kupata ujauzito mara baada ya kuacha kutumia sindano hizi. Sindano huwa hazisabibishi ugumba!
  • Kuongezekam uzito au kunenepa. Hii huweza kutokea kwa baadhi ya wanawake, na mara nyingi pale anapotumia sindano kwa miezi 6 au zaidi.
  • Mifupa kulainika. Hii ni kutokana na kutumia njia hii kwa muda mrefu, na mifupa hurudi sawa pale sindanno zinapoachwa.

No comments:

Post a Comment